Friday, August 12, 2011

WIKI HII KWENYE AFROBEAT

Najua unamkumbuka sana Marehemu Bi. NASMA KHAMIS KIDOGO basi wiki hii tutakukumbusha kwa kukupa burudani ya wimbo wake unaoitwa MAMBO IPO HUKU kwenye sehemu ya ujumbe wa leo.



BOB RUDALA atakueleza kuhusu wapi alipotoka mpaka kufikia alipo sasa na maisha yake ya muziki kwa ujumla, pia ataeleza sababu za yeye kuhama INAFRIKA BAND na kuhamia KALUNDE BAND na mengine mengi tuuu.. Haya yote ni kwenye sehemu ya CHEKECHA.
    Hawa wanaitwa TCE ni kikundi cha ngoma za asili wanapatikana maeneo ya Ubungo, watoto wana kipaji cha hali ya juu sana kuanzia kucheza, kupiga ngoma mpaka Sarakasi.. Hawa utawaona kwenye sehemu ya KWACHU KWACHU.

Hii inaitwa CASSAVA BAND, wengi wao hapa ni wakemavu wa macho lakini kazi yao ni balaa, utawaona kwenye kipengele cha COPI KALE ambapo watakuimbia wimbo unaoitwa muziki ni wa nani wa kwake Dr. REMMY ONGALA.
         Huyu anaitwa Mzee YUSUF IDD ni mmoja kati ya wanamuziki wa zamani na wiki ndo atakuwepo   kwenye sehemu ya pili ya COPI KALE akielezea kuhusu wimbo huo wa Muziki ni wa nani, kwa jinsi anavyoufahamu yeye na kipindi hicho ilikuwaje ulipokuwa ukipigwa katika sehemu mbalimbali?????

Kwenye HABARI NYEPESI NYEPESI tutakuwa na JUICE YA MACHUNGWA kutoka DIAMOND MUSICA akituelezea kuhusu mipango ya bendi yao katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani na hapo baada ya Ramadhani
Pia TWAHA atawakilisha DAR MODERN TAARAB kuhusu mipango yao katika kipindi hiki na baada ya Ramadhani pia ambapo wao wana mpango wa kufanya ziara katika mikoa mbalimbali hapa nchini mara baada ya Ramadhani kumalizika na maandalizi ya uzinduzi  Album zao mbili.
Kwa hayo na mengine mengi tu usikose kuangalia kipindi chako bora kabisa hapa Afrika Mashariki cha habari na burudani kutoka barani Afrika, JUMAMOSI hii saa 1 jioni...  AFROBEAT ya EATV PEKEEEE.... USIKOSEEE!!!!!!!









No comments:

Post a Comment