Thursday, August 18, 2011

GURUMO ALIA NA WANAOIBOMOA TWANGA PEPETA


 Maalim Gurumo akiwa na Asha Baraka
Nguli wa muziki wa dansi nchini ambae pia ni kiongozi wa Msondo ngoma music Band, Maalim Gurumo amesikitikia kitendo cha baadhi ya wamiliki wa bendi hapa nchini kuchukua wanamuziki kutoka Bendi ya Twanga pepeta ili kuidhoofisha bendi hiyo.

Gurumo amesema mmiliki wa Bendi hiyo Asha Baraka ni mtu mwema sana ambae astahili kufanyiwa vitendo vinavyofanywa na watu hao vya kuchukua wanamuziki hao.
Gurumo alisema:"Wamiliki wa bendi zingine wamekuwa wakimchukulia wasanii wake huyu dada ili waidhohofishe bendi yake lakini hawamtendei haki wanampiga vita bure tu ni mtu mwenye huruma sana"

  Mwanzoni mwa mwaka huu kiongozi wa bendi ya Extra bongo Ally Choki alikomba wanamuziki tisa wa Twanga pepeta na hivi karibuni kumchukua Aisha Madinda ambae alikuwa akipamba safu ya wanenguaji kwa umahiri wake wa kucheza.

No comments:

Post a Comment