Thursday, August 18, 2011

NDOA YA MERCY JOHNSON KAMA KAWA

Mercy pichani akifanya shopping kwa ajili ya harusi yake

Ndoa ya mwigizaji nyota nchini Nigeria MERCY JOHNSON bado iko palepale ingawa kulikuwa na uvumi uliojitokeza siku chache zilizopita kuwa haitofungwa tena kutokana na mwanamke mmoja aliyetambuliwa kwa jina la LOVELY OKOJIE kujitokeza wiki kadhaa zilizopita na kudai kuwa yeye ni mke halali wa Prince Odianose Okojie ambae ni mume mtarajiwa wa Mercy Johnson na amezaa nae watoto wawili.

Taarifa ya mwanamke huyo ambayo ilileta utata kwa mashabiki wa Mercy ulimwenguni wakifikiri kuwa ndoa hiyo haitafungwa tena, imepata ufumbuzi baada ya Mercy mwenyewe kutambua utata huo na hatimae kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hilo ambao unasema "mahusiano baina ya Prince Odianose Okojie na Lovely Okojie yalivunjika miaka mitano iliyopita na mipango ya ndoa ya Mercy johnson na Odi imekuwa wazi kwa muda mrefu.
Odianose kweli ni baba wa binti wa kwenye picha inayosambazwa kwenye mtandao wa kompyuta lakini kuna shaka kama pia ndiye mzazi wa mvulana. Lakini pia Odianose ni mwana wa mfalme hivyo anaweza kuoa mke zaidi ya mmoja kwa mujibu wa sheria za kimila.
Wakati tukiachwa kuamua nani yuko sahihi na nani amekosea, mipango ya ndoa kati Mercy na Odi ipo palepale na itakuwa hafla ya siku nne ambayo itaanza Agosti 25 mpaka 28, 2011. taarifa hiyo iliitimisha

Ufafanuzi wa ndoa hiyo unaonyesha kuwa patakuwa na ndoa ya mahakamani Agosti 25, Engagement siku inayofuata ya Agosti 26, ndoa ya kanisani Agosti 27 ikifuatiwa na sherehe ya shukrani Agosti 28.



No comments:

Post a Comment