KOPI KALE


Mambo ya Police Jazz Band hayo pande za Kilwa Road Pub JKT, anaitwa Afande Hamza mmoja kati ya waimbaji
Huyu nae ni muimbaji ila kwa bahati mbaya sikuweza kupata jina lake, hapo kila mmoja alikuwa busy hivyo kupata majina ya watu wote inakuwa tafrani kidogo
Huyu anaitwa Afande Salum, yeye pamoja na kupiga Drums lakini pia ni mcheza Show mahiri sana lakini siku hii sikuweza kupata picha wakati anacheza ila wakati mwingine nitajitahidi nitaweka
Anaitwa Mariam a.k.a mafta halisi ya kitanzania ni mcheza show pia, kama ulikuwa hujui kwamba maafande nao wanaweza kukata nyonga basi angalia Afrobeat wiki hii ili ujionee mwenyeweeee usingoje kusimuliwa
Tukakutana na huyu kaka cha ajabu hatumfahamu lakini yeye anatufahamu wote mimi na mdogo wangu hapo kati anaitwa Khadija.