Tuesday, August 16, 2011

FEROOZ AJA NA STYLE YA MNANDA

FEROOZ katika pozi
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini FEROOZ aliyetamba na vibao kama starehe, bosi na kamanda akiwa na kundi la Daz nundaz na hatimaye kupotea kwenye gemu kwa miaka kadhaa, sasa amerejea na style ya mnanda huku akiwaahidi mashabiki wake kuwa amerudi upya na vitu kibao vikali.

Akizungumza jijini Dar Es Salaam  FEROOZ, amesema baada ya kimya cha muda mrefu sasa amerejea tena na tayari ameshatoa kitu kiitwacho "Ndege mtini" chenye style ya mnanda alichokifanya katika studio ya Hammy B chini ya Producer Pancho. 
Aidha Video ya wimbo huo inatengenezwa katika Studio ya Visual Lab chini ya Adam Juma.

No comments:

Post a Comment