Thursday, August 18, 2011

MASHAUZI CLASSIC KUTAMBULISHWA RASMI JUMAMOSI HII


Kundi jipya linalokuja juu kupitia Tasnia ya muziki wa Taarab nchini "MASHUZI CLASSIC MODERN TAARAB" linatarajiwa kutambulishwa rasmi kwa wadau, Jumamosi hii katika kambi ya kundi hilo iliyopo Kinondoni jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza jijini Dsm mlezi na Mshauri mkuu wa kundi hilo Bwana Juma Mbizo amewaomba wadau wa Kundi hilo na wapenzi wa Taarab kwa ujumla kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya utambulisho ili kuona kile wanachokifanya wakiwa kambini pia kutoa ushauri wa nini kifanyike ili kuboresha kundi hilo kabla ya uzinduzi rasmi ambao utafanyika siku ya Eid Mosi.

Nae mmiliki wa kundi hilo Isha Ramadhan makongo a.k.a Isha Mashauzi au Jike la Simba kama ambavyo mwenyewe amekuwa akijiita amesema ameamua kuanzisha kundi lake hilo baada ya kupata mafanikio katika kipindi cha muda mfupi na kuona kuwa anaweza kujitegemea kwa kuwa na kundi lake.
Isha Mashauzi amejipatia umaarufu kwa kipindi kifupi katika Tasnia hii ya muziki wa Taarab akiwa na kundi la Jahazi Modern Taarab linaloongozwa na Mzee Yusuph baada ya kutamba na vibao "hayanifiki" na "ya wenzenu midomo juu" na baadae kuja na wimbo wake binafsi unaoitwa "Mama nipe radhi" ambao uliteka soko la Taarab hususan kwa upande wa akina mama.

No comments:

Post a Comment