Monday, August 15, 2011

MSECHU ANG'ARA TUSKER PROJECT FAME "ALL STARS"


PETER MSECHU (TANZANIA)

DAVIS NTARE (UGANDA)

ALPHA RWIRANGIRA (RWANDA)
Hatimaye shindano la TUSKER "ALL STARS" lililoanza June 26 mwaka huu limefikia tamati jana August 14 kwa washiriki watatu kuibuka kidedea.


Walioibuka kidedea kwa ushindi katika shindano hilo ni PETER MSECHU kutoka Tanzania (mshindi wa pili TPF- 4), DAVIS NTARE kutoka Uganda (mshindi TPF-4) na ALPHA RWIRANGIRA kutoka Rwanda (mshindi TPF-3).


Washindi hawa watatu wamepata shavu la kuperform Stage moja na Wasanii wa kimataifa baadae mwaka huu nchini kenya.


Washiriki wengine katika Shindano hilo mwaka huu walikuwa ni Hemed Suleiman kutoka Tanzania, Caroline Nabulime na Amileena Mwenesi kutoka Kenya, Bernard Ng'ang'a na Patricia Kihoro kutoka Kenya ambapo walikaa wiki 8 kabla ya shindano hilo kumalizika.


Habari kwa Hisani ya Chini ya Carpet

No comments:

Post a Comment