Friday, August 19, 2011

FERGUSON AWATULIZA MASHABIKI KWA MDUDU

Rapa mahiri anayetingisha bongo kupitia Bendi ya Extra bongo "Wazee wa kizigo" SAULO JOHN (FERGUSON) pichani, amewahakikishia mashabiki wake kuwa yeye ni mkali kwa kuja na style yake mpya inayoitwa mdudu ambayo imeanza kutumika jumamosi iliyopita katika ukumbi wa Meeda Sinza, Jijini Das Es Salaam.

 Rapa huyo ambae alitamba na bendi ya Twanga pepeta kabla ya kutimkia Extra Bongo amesema ameibuka na Rap hiyo ili kuwahakikishia mashabiki wake kuwa yeye ni mkali na haishiwi style na kuongeza kuwa style hiyo imewakuna mashabiki waliokuwepo Meeda siku ya jumamosi ambapo anaamini kuwa Rap hiyo itapokelewa vizuri na mashabiki kama ilivyokuwa kwenye Rap ya Mimi ni chuma, Nasikia baridi, Ulinibania na nyingine nyingi.

Wakati huohuo bendi ya Extra bongo mwanzoni mwa wiki hii imefanya Video ya wimbio wao wa Watu na Falsafa uliotungwa na Banza Stone ambapo mpaka sasa bendi hiyo imeshakamilisha kurekodi nyimbo za Album yao ya pili.

No comments:

Post a Comment