Monday, August 29, 2011

MASHAUZI CLASSIC YASHAURIWA KUBADILI JINA

Kundi jipya la Muziki waTaarab nchini lenye maskani yake kinondoni jijini Dar Es Salaam (Mashauzi Classic) linaloongozwa na Isha Ramadhani a.k.a Isha Mashauzi limeshauriwa kubadili jina hilo na kutafuta jina lingine litakalotafsirika kirahisi ili kusaidia kundi hilo kupata umaarufu mapema.

Ushauri huo umetolewa na Waziri mkuu Mstaafu Bw. John Samwel Malecela (pichani) kwa madai kuwa, kwa mtazamo wake anadhani kuwa jina hilo haliwezi kuteka haraka soko la muziki kibiashara na kushauri kuwa jina hilo libadilishwe.
Akizungumza jijini Dar Es Salaam mlezi wa kundi hilo ambalo linatarajiwa kuzinduliwa rasmi siku ya Eid Mosi katika ukumbi wa Travel Tine jijini Dar Es Salaam Bw. Juma Mbizo (pichani) amesema, baada ya kutoa ushauri huo Malecela amependekeza kundi hilo litumie majina ya Mwanasesele au Mzalendo na kuongeza kuwa uzuri wa kundi ni pamoja na jina na hata kibiashara suala la jina lina umuhimu mkubwa ambapo alitolea mfano Bendi ya African Stars "Twanga pepeta" kuwa limefanikiwa kuteka soko la burudani kwa kuwa jina lake linauzika.
Hata hivyo Juma Mbizo alisema kuwa si lazima ushauri huo ufuatwe kwa kuwa inafahanika kuwa jina hilo la Mashauzi limetokana na jina la kisanii la Mmiliki na Mkurugenzi wa kundi hilo ambalo hata hivyo Malecela hana uhakika kama litateka soko la Mashabiki kwa kasi.




No comments:

Post a Comment