Tuesday, October 30, 2012

USAFIRI WA TRENI JIJINI DAR ES SALAAM WAANZA

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe (katikati) akiwasili kupanda treni kituo cha Tazara kuelekea mjini kufanya uzinduzi.
Treni ikiwasili Kituo cha Ubungo Maziwa.
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ndani ya treni.
Tangazo la treni jijini Dar.
Kwa usafiri wenye utulivu kama huu kwa nini usijisomee kwenye treni.
Ukaguzi wa tiketi ndani ya treni.
Usafi wa Ndani ya Treni.
Baadhi ya Maeneo yakiendelea na Matengenezo.
Tiketi zikikatwa ndani ya treni.

Hapa ndipo wanapotangaza na kutoa burudani ndani ya treni.
Baadhi ya abiria wakishuka na kupanda kwenye treni.
Baadhi ya abiria wakiingia kwenye treni.
Ulinzi ni Mkali.
 

Monday, October 29, 2012

MAPACHA WATATU WAKAMILISHA ALBUM YA PILI WAUKACHA WIMBO WA KALALA JUNIOR



Bendi ya Mapacha Watatu imekamilisha nyimbo za albamu ya pili ikiwa imeachana na wimbo wa Kalala Junior wa 'Mtoto wa Paka' uliotunga kabla ya kuikimbia.

Akizungumza jijini DSM, Khalid Chokoraa ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa bendi hiyo alisema kuwa wameachana na wimbo wa Kalala kwa vile utaratibu wao hauruhusu kutumia wimbo uliotungwa na mwanamuziki aliyewakimbia.

"Ana uhuru wa kutumia wimbo wake huko aliko kwani ndivyo utaratibu wetu ulivyo, hatuwezi kurekodi wimbo wa mwanamuziki ambaye amechana nasi," alisema na kuendelea:

"Zipo nyimbo zetu ambazo tumekamilisha kwa ajili ya albamu ya pili ambazo ni ‘Wosia wa Babu’, ‘Naonewa’, ‘Chanzo Wanaume’, ‘Yarabi Nafsi’, ‘Mjasiriamali’, ‘Mjasiriamali', 'Sumu ya Mapenzi remix', 'Wivu' na  'Wosia wa Babu'.

Alisema kuwa kilichobaki sasa ni mipango ya kushuti video za baadhi ya nyimbo hizo ili zianze kurushwa kwenye vituo mbalimbali vya runinga kama sehemu ya utambulisho wa ujio wa albamu hiyo.

Aidha, Chokoraa alisema bendi hiyo haina ubaya wowote na Kalala Junior na kwamba wanaendelea kuheshimiana kama kawaida licha ya kwamba amewaacha na kurudi Twanga Pepeta.





Twanga Pepeta yakubali matokeo

 
Wanenguaji wa Bendi ya  Twanga Pepeta

Ni zaidi ya wiki mbili sasa tangu mwimbaji wa bendi ya Twanga Pepeta, Uncle Vena aingie mitini, uongozi wa  kampuni ya ASET inayomiliki bendi hiyo umesema kuwa hauhangaiki kumtafuta.

Kwa mujibu wa meneja wa kampuni hiyo Hassan Rehan, awali walikuwa wakimtafuta mwimbaji huyo lakini sasa wameona hakuja haja ya kufanya hivyo na badala yake wanaendelea na kazi kama kawaida.

"Tunajua kwamba ameondoka kwenye bendi akiwa na mkataba wa miaka mitatu, lakini hata hivyo hatuna budi kuachana naye kwani tumejitahidi kumpigia simu, lakini alikuwa hapokei na sasa haipatikani kabisa," alisema Rehan.

Meneja huyo alisema kuwa Twanga Pepeta ina wanamuziki wengi na wenye uwezo mkubwa wanaoendelea kufanya kazi kama kawaida lakini akaongeza kuwa iwapo mwimbaji huyo akijitokeza watamdaka kwa sababu ameondoka akiwa na mkataba wa miaka mitatu ya kuitumikia bendi hiyo ambao aliusaini mwanzoni mwa mwaka huu.

Mwimbaji huyo aliyeibuliwa na Mwinjuma Muumin akiwa naye kwenye bendi yake ya Bwagamoyo Sound, alijiunga Twanga Pepeta mwaka juzi baada ya bendi hiyo kufa.

Uncle Vena ambaye hadi sasa haijafahamika alikotimkia, ameshiriki kikamilifu kurekodi nyimbo za albamu ya 12 ya bendi hiyo ambazo ni 'Mapambano ya Kipato', 'Nyumbani ni Nyumbani',  'Ngumu Kumeza', 'Mwenda Pole Hajikwai', 'Shamba la Twanga' na 'Walimwengu Hawana Jema'.

Norman, Menynah Out Epiq BSS

Norman Severino
Zikiwa zimesalia  wiki mbili kufikia fainali za shindano la Epiq Bongo Star Search, mchuano umezidi kuwa mkali baada ya wiki hii washiriki wawili, Norman Severino na Menynah Atik kuaga mashindano.

Washiriki hao wameaga na kuwaacha watazamaji midomo wazi, hali inayoonyesha shindano hilo limefikia patamu, kwani kila mshiriki aliyebaki ni mkali.

Kutoka kwa washiriki hao kuliwashtua hata majaji wenyewe, ambapo jaji Master Jay aliwatupia lawama Watanzania kwa kushindwa kuwapigia kura washiriki wenye vipaji.

“Hivi Watanzania mnajua kushindwa kupiga kura kwenu kuokoa washiriki wenye vipaji ndiko kulikofanya tumpoteze mshiriki mwenye kipaji kama Norman?" alisema Master Jay wakati akitangaza Norman ndiye anayeaga mashindano hayo.

Wanachi waliofika kushuhudia shindano la Jumapili katika studio za EBSS zilizoko Budget Hotel Kunduchi, nao walionekana kuzizima ghafla huku baadhi ya washiriki nao wakionekana kutokwa machozi, na kuzidi kutishika kwa hali ile.
Menynah Atik

Jaji mkuu wa shindano hilo, Ritha Paulsen, aliwapa changamoto watazamaji kuwa kusikitika tu hakutasaidia washiriki wanaowapenda kubaki kwenye nyumba bali ni kura.

“Leo majonzi yametawala lakini ndo hivyo mimi nawasisitiza kila siku, ili mshiriki unayempenda asikutwe na hali hii… inabidi umpigie kura. Kura yako ndo kitu pekee kitakachomuokoa mshiriki ambaye wewe unaamini anastahili kuendelea kuwapo kwenye mashindano haya na mwishowe aje kuibuka mshindi wa shindano hili,” alisisitiza Ritha.

Washiriki wengine walioingia katika Danger Zone wiki hii ni Godfrey Kato mwenye namba za ushiriki EBSS 01, Husna Nassoro mwenye namba EBSS 02, Nshoma Ng’hangasamala mwenye namba EBSS 07 na Walter Chilambo (EBSS 12). 

Watanzania wameombwa kupiga kura kuwaokoa washiriki wanaowapenda kwa kuandika EBSS unaacha nafasi kisha unaandika namba ya mshiriki kwenda 15530.



 

Friday, October 26, 2012

TINO ATANGAZA KUACHANA NA FILAMU ZA MAPENZI

Msanii nguli wa filamu nchini Hisani Muya maarufu kama Tino anatarajia kuzindua Movie yake mpya aliyoipa jina la CID ambayo imefanywa kwa style ya "Action" zaidi.
Uzinduzi huo unaotarajiwa kufanyika leo katika ukumbi wa Business Park uliopo Victoria utafuatiwa na Uzinduzi wa Project yake mpya ya kusaka vipaji vya waigizaji wachanga yaani Movie Star Search.
Akizungumza na Blog hii Tino amesema ameamua kuanzisha Project hiyo baada ya kugundua kuwa kuna vipaji vingi sana mtaani lakini vinashindwa kuibuliwa kutokana na vijana hao kukosa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao hivyo.
Pamoja na uzinduzi wa Filamu na Project yake hiyo pia Tino atatangazwa rasmi kuwa Balozi wa kituo kimoja cha watoto Yatima kilichopo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Aidha Tino amefunguka kuwa kuanzia sasa ameachana Rasmi na Filamu za mapenzi na kujikita zaidi kwenye filamu za Action.

Thursday, October 25, 2012

HIZI NDIZO ZAWADI ZA WASHINDI WA FAINALI ZA REDDS MISS TZ 2012

Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency,waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga, akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza zawadi za Mshindi wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2012. Kulia ni Meneja wa Kinywaji cha Redds, Victoria Kimaro.
Kampuni ya TBL kupitia kinywaji chake cha Redds Original ambao ndio Mdhamini mkuu wa shindano la Redds Miss Tanzania 2012, leo tunatangaza zawadi kwa washiriki wote wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam jana  Mkurugenzi wa Kampuni ya LINO INTERNATIONAL AGENCY Hashim Lundenga amesema katika fainali za shindano la Redds Miss Tanzania 2012 zitakazofanyika tarehe 3 Novemba 2012 katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel, (Ubungo Plaza) jijini Dar es salaam ambapo ni shindano linaloshirikisha washiriki 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.

Katika maelezop yake, Lundenga amesema zawadi hizo zitakuwa kama ifuatavyo
1) Mshindi wa Kwanza atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 8,000,000/- Pamoja na gari
2) Mshindi wa pili atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 6,200,000/-
3) Mshindi wa tatu atapata zawadi ya pesa taslmu shs: 4,000,000/-
4) Mshindi wa nne atapata zawadi ya pesa taslimu shs; 3,000,000/-
5) Mshindi wa tano atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 2,400,000/-
6) Mshindi wa sita hadi wa 15 kila mmoja atapata shs: 1,200,000/-
7) Washiriki wengine wote waliobaki kila mmoja atalipwa shs: 700,000/-
Katika shindano hilo ambalo ndani yake kuna mashindano mengine madogo [Fast Tract] tayari washiriki 3 wameshajipatia tiketi ya kuingia katika
 [Top 15 Finalist]
Washiriki hao ni Lucy Stephano – Miss Photogenic
Magdalena Roy – Top Model
Mary Chizi – Top Sport Woman
Shindano dogo lingine limepangwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 26 Oktoba 2012 la kumtafuta mrembo wenye Kipaji. Miss Talent.
Na tarehe 28 Oktoba 2012 atapatikana Miss Personality.
Nae Meneja wa kinywaji cha Redds Original Bi Victoria Kimaro amesema huu ni wakati sahihi wa kumpata mshindi biomba mwenye vigezo sahihi hivyo kuwataka wapenzi wote wa tasnia ya urembo na wapenda maendeleo kote nchini kujianda kupata tiketi za kushudia fainali hiyo mapema ili kuweza kupata fursa ya kupata burudani mbalimbali.Kwa kweli shindano la mwaka huu tunatarajia kuwa litafana sana hasa kwa kuzingatia kuwa maandalizi yote yameshakamilika kwa kiwango kikubwa na sisi kama wadhamini wakuu tunahakikisha kuwa mwaka huu kila atakaefika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza atakuwa na jambo la kusimulia kwa sababu ni shindano la kipekee.
Shindano hili la Redds Miss Tanzania 2012 linadhaminiwa na
.Redds Original,Star TV,Giraffe Hotel.

Tuesday, October 23, 2012

Lulu arejeshwa Rumande

 

 Msanii maarufu wa filamu nchini, Elizabeth Michael a.k.a LULU, (Katikati), akielekea kupanda basi la magereza kwenye viwanja vya Mahakama ya Hakimu Kkazi Kisutu, baada ya kesi inayomkabili ya kutuhumiwa kumuua msanii mwenzake, Hayati Steven Kanumba, kuahirishwa tena na hivyo mwanadada huyo ambaye umri wake unaleta utata ataendelea kusota rumande hadi hapo kesi yake itakapotajwa tena
LULU akielekea kupanda gari tayari kwa safari ya Segerea kunako mahabusu.

Monday, October 22, 2012

M's East Africa 2012 Tz yaanika Mrembo wake

 

Mrembo anayekwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye kinyang'anyiro cha Miss East Africa mwaka huu  ni mwanadada JOCELYNE DIANA MARO (22).

Mlimbwende huyo alipatikana ndani ya mchakato ulioendeshwa na kamati maalum ya kuratibu zoezi hilo, kwa zaidi ya miezi mitatu iliyopita na kuwashinda warembo wengine 148 waliojitokeza kutaka kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss East Africa 2012

 Maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri na yapo kwenye hatua za mwisho ikiwa ni pamoja na kukamilisha taratibu zote za BASATA ili kufanikisha mashindano hayo yatakayofanyika tarehe 07 December, 2012 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.
Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu tayari yameanza kuvuta hisia za watu wengi barani Africa kufuatia kiwango cha juu cha warembo wanaowania taji hilo.

Nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine zilizoalikwa kushiriki ni pamoja na Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan, Malawi, pamoja na visiwa vya Seychelles, Madagascar, Reunion, Comoros, na Mauritius.

Mashindano ya Miss East Africa yanalenga kukuza ushirikiano na kutangaza utamaduni wa Afrika Mashariki, pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania kama Nchi wenyeji wa mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa Afrika.
 
Mashindano ya Miss East Africa yanamilikiwa na kuandaliwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam,.

DAR LIVE YACHANUA NA MSAKO WA THE MIC KING, TMK WANAUME NA EXTRA BONGO

Si lingine bali ni lile shindano la kumsaka Mfalme wa Mic (The Mic King), AfroKija bila kuchelewa ilikuwa ndani ya tukio lililowika ndani ya Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem na kuwapa wawakilishi wapatao 12 wa Wilaya ya Ilala, huku burudani ya kufa mtu ikishushwa na Kundi zima la Wanaume TMK ikiwemo na Bendi ya Exrta Bongo.

                      

Kundi zima la TMK Wanaume likionyesha staili yao ya Mapanga Shaaa jukwaani.


 
Washiriki 12 waliopenya katika shindano hilo wakiwakilisha wilaya ya Ilala.

Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ali Choki (kulia) akiwa na wanenguaji wake jukwaani.

 
Memba mzee wa kundi hilo, Bibi Cheka (kushoto) akimwaga mistari jukwaani. Kulia ni Temb


Mmoja wa washiriki wa The Mic King akionyesha uwezo wake jukwaani.

...The Mic King akiendelea kusakwa.

Majaji wa The Mic King, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ (kushoto), John Dilinga ‘DJ JD’, na Sister P wakifuatilia shindano hilo.

 Mmoja wa washiriki akionyesha ufundi wa kurap.


Wanenguaji wa Extra Bongo wakionesha mambo jukwaani kuinogesha Dar Live.

Msanii anayesumbua na songi la Mwanayumba ndani ya gemu la Bongo Fleva, Chegge Chigunda, akimsaka ‘Mwanayumba wake’ jukwaani.

 Mkali wa kundi wa TMK Wanaume, Amani Temba, akiwaimbisha mashabiki wake kwa kutumia kipaza sauti.

                                       
          Zao jipya la Kundi la TMK Wanaume, mwanamuziki    
                     Getruda, akionyesha  uwezo wake jukwaani.

Aisha Madinda asaka kibarua




Aisha Mbegu 'Madinda' akiwa kikazi zaidi  hapo ni kabla hajaokoka

 Kwa sasa mnenguaji huyo anasali ndani ya Kanisa la Kilokole la Zoe lililopo maeneo ya Tabata hapa Jijini, kwani alisema kwamba ameanza kusaka kibara kwenye maofisi mbalimbali kupitia vyeti vyake.


Hiyo ni baada ya kuamua kuokoka, mnenguaji aliyejizolea umaarufu  kwenye muziki wa dansi Aisha Mbegu 'Madinda', alisema kwamba kwa sasa anasaka kibarua kingine cha kufanya huku akimtumikia Mungu.

Kwani aliweza kujisalimisha kwenye  kanisani mara tu baada ya kusumbuliwa na miguu kwa muda mrefu, na kufanikiwa kupona ndipo akaona ni bora aachane na kazi ya muziki wa kidunia ili atafute kibarua kingine cha kufanya.

"Tangu niombewe nimepona kabisa na sasa miguu imetulia na nimeona niachane na muziki ili nitafute kazi nyingine ambayo haiwezi kuniingiza kwenye matatizo," alisema mnenguaji huyo.

Mbali na hilo anamshukuru mtu aliyempa ushauri wa kwenda kwenye kanisa hilo, ambalo amedai kuwa limemsaidia kupona maradhi yake ya miguu na kwamba anaendelea kwenda katika kanisa hilo kila Jumapili.

"Kwa zaidi ya miaka miwili nimekuwa nikisumbuliwa na miguu kila ninapopanda jukwaani kucheza, lakini baada ya kwenda kuomba nimekuwa fiti ndio maana nikaamua kuacha muziki ili nifanye kazi nyingine," alisema.


Friday, October 19, 2012

Wolper aathiriwa na Uchumba

    
                               
                               Jacqueline Wolper katika moja ya pozi zake


Ni yule Msanii  kutoka kiwanda cha filamu Bongo,  Jacqueline Wolper  amesema kutokana na tabia aliyoonesha aliyekuwa mchumba wake, Abdallah Mtoro ‘Dallas’ amekoma na hatorudia kumtangaza mchumba hadharani.

Akizungumza na kituo kimoja maarufu cha runinga jijini Dar juzikati, Wolper alisema amejifunza mengi kutokana na tabia aliyoionesha Dallas baada ya kumtangaza kuwa ni mchumba wake.

“Dallas alipokuwa mbali alionesha mapenzi ya dhati ndiyo maana nikampenda na nikamtangaza hadharani lakini alipokuja karibu tabia zake hazikunifurahisha ndiyo maana nikamuacha,” alisema Jacgueline.