Thursday, August 4, 2011

EXTRA BONGO KUENDELEA NA SHOW WAKATI WA RAMADHANI

PENTAGON-MWANAMUZIKI EXTRA BONGO

Baadhi ya wanamuziki EXTRA BONGO na Mkurugenzi wao  ALLY CHOKI
Bendi ya Muziki wa Dansi nchini EXTRA BONGO, imesema itaendelea kutoa burudani katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambapo watakuwa katika ukumbi wa Meeda Sinza, kila Jumamosi.


Akizungumza na Blig hii mwishoni mwa wiki kati ukumbi wa Meeda mmoja wa waimbaji wa Bendi hiyo anayefahamika kwa jina la PENTAGON amesema, wameamua kufanya hivyo ili kuwafanya mashabiki wao washushe Futari yao kwa kupata burudani angalau mara moja kwa wiki.


Amesema pamoja na kupiga Show mara moja kwa wiki lakini pia watautumia muda huo pia kwa kutengeneza nyimbo mbili zilizobaki ili kukamilisha Album yao wakati huohuo watakuwa wakifanya Video za nyimbo zao tatu ambazo bado hawajafanya Video.

No comments:

Post a Comment