Tuesday, October 25, 2011

LUNCH NJEMA JAMANIIII!!!!

Kaaaazi kwelikweli badala ya kula kaamua kuingia kwenye sahani na yeye!!!

UNAMKUMBUKA MAREHEMU FRANCO???

Picha zote hapo juu zinamuonyesha Marehemu Franco katika matukio mbalimbali ya shughuli yake ya Muziki

Jina lake halisi lilikuwa ni Francois Luambo Makiadi lakini alikuwa maarufu kama Franco Luambo, alizaliwa July 6, 1938 katika kijiji cha Sona-Bata huko DRC  na kufariki October 12, 1989 akiwa na watoto 18.

Alianza kupenda muziki akiwa na umri mdogo sana na alipofika umri wa miaka 7 alitengeneza Gitaa lake ambalo alikuwa akilipiga sokoni ambapo mama yake alikuwa akifanya biashara ya mikate kwa lengo la kuwavutia wateja.

Muziki wake kwa mara ya kwanza ulirekodiwa na kuwekwa kwenye Tape na mpiga Gitaa Paul Ebengo Dewayon ambae baadae alimchukua na kuanza kumfundisha namna ya upigaji wa Gitaa kitaalamu na mara ya kwanza alianza kupiga show akiwa na Band ya Dewayo akiwa na umri wa miaka 12. Lakini pamoja na kupiga Gitaa na vyombo vingine, Franco alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuimba kama unavyoona kwenye picha akiimba na wakati huo huo anapiga Gitaa

Mwaka 1953 alitoa wimbo wake alioupa jina la Bolingo na ngai na Beatrice(My love for Beatrice) na baadae mwaka 1956 alianzisha band iliyoitwa OK Jazz ambayo baadae ilibadilishwa na kuwa TP OK Jazz, Band ambayo ilikuwa kutoka wanamuziki 6 mpaka 50 miaka 30 baadae ambapo iliendelea kuwa juu na kutengeneza album zaidi ya 150 ambapo kila album iliweza kuuza zaidi ya Kopi 50,000.

Nimekuletea habari hii leo katika kukumbuka miaka 22 tangu kifo cha mwanamuziki huyu ambae amechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa Dansi barani Afrika.. 

R.I.P FRANCO

YVONNE CHAKACHAKA NA YOUSSOU N'DOUR KUTOA WIMBO UNAOELIMISHA KUHUSU MADAWA FEKI

Yvonne Chakachaka(Princess of Africa)

Youssou N'dour


Wanamuziki Nguli barani Afrika, Yvonne Chakachaka na Youssou N'dour wanatarajia kuzindua wimbo wao mpya walioupa jina la "PROUD TO BE" ukiwa na lengo la kuielimisha jamii ya Afrika kuhusiana na Madhara ya matumizi ya madawa Feki.

Uzinduzi wa wimbo huo utafanyika October 27, 2011 katika Hotel ya Hilton jijini Nairobi, Kenya. Yvonne Chakachaka anayefahamika pia kama Princess of Africa atafanya Onyesho saa 11:00 asubuhi ambapo pia atashiriki katika mkutano na waandishi wa habari.

Kutoka kwa Afrokija: Madawa haya Feki yanaweka maisha yetu hatarini, hivyo tunatakiwa kuwa makini na dawa hizi ili kujiepusha na madhara yanayoweza kutokea maana si wote ambao hupoteza maisha, tumeshuhudia ndugu zetu wengi tu wakipata ulemavu wa kudumu na hata maradhi ya muda mrefu kutokana na matumizi ya dawa hizo Feki, Hivyo tunapaswa kuwa makini!!

Kwa habari zaidi, tembelea:www.safemedicines.org

Monday, October 24, 2011

THE GREAT KUPAKUA "BECAUSE OF YOU" WIKI IJAYO

Maneno ya Kanumba mwenyewe "Inaitwa ''BECAUSE OF YOU'' kutoka KANUMBA THE GREAT FILM,nimeigiza mimi,Rose Ndauka,Thea,Grace Mapunda,nk,Mtunzi ni Rose Ndauka na amekamua vilivyo mpaka nikahisi naigiza na msanii wa nje na si Rose niliyemzoea.......BECAUSE OF YOU.....kama kawaida yangu kubadilika ukitazama movie hii utaona mabadiliko sana mojawapo ni hakuna scene ndefu ndefu za kupoteza mda yaani kifupi hakuna scene inayokaa zaidi ya dakika moja na zote zina speed,hakuna uongeaji mwingi kwa characters wameongea kidogo tu ila vitendo kwa sana.Pata nakala yako original bila kuazima au kukodisha.....
Wadau tupo tayari kuipokea tuone hayo uyasemayo ndivyo ilivyo au Lugha ya kibiashara tuuuuu???

WEMA NA DIAMOND NINA MACHACHE KWA AJILI YENU

Sarakasi za 'Love-Cartoon' kali star wa Bongo Flava,Naseeb Abdul aka Diamond baada ya kutangaza kummwaga Wema Sepetu (Miss TZ 2006-2007) kwa sasa zimefunguliwa upya kuwa busara za mama mzazi wa Diamond,Sanura Khassim ziliokoa jahazi kwa kumlazimisha mwanaye arudiane na Wema ili mambo yasiharibike....
Imefunguliwa kuwa baada ya Wema kupiga simu na 'kulia lia' kwa mkwe kuwa atakunywa sumu,Mama Mkwe aliwaita Wema na Diamond na wajomba zake nyumbani kwake,ili wazungumze na baada ya mvutano wa muda mrefu,wajomba na Mama walikomaa Diamond alinywea akasalimu amri mbele ya wakubwa na kurudiana na lovi-davi wake aliye-make sana headlines kwa kutoka na Ma-Star wa bongo kuanzia....Steven Kanumba, Charles Baba,Hartmann Mbilinyi na Jumbe Yusuf.

SOURCE: chini ya carpet

Kutoka kwa Afrokija: Mi nadhani hivi vitu ambavyo vinaendelea kwa sasa ni vya kudhalilishana, kama mmeamua kupendana basi mtulie na muonyeshe hayo mapenzi yenu kuliko kuanika mambo yenu kila siku, coz kuna Couples nyingi tu hapa bongo lakini hatuoni wakidhalilishana kama mnavyofanya nyie, Binafsi naamini kuwa endapo unampenda mwenzi wako utamlinda na hutopenda apate aibu na kudhalilishwa kila kukicha hata kama amekukwaza.. Nampenda sana Wema pamoja na yote yanayomtokea ila Diamond unapaswa kutunza heshima ya mwenzako usichukulie udhaifu wake wa kukupenda kwa kumtia aibu kwenye vyombo vya habari kila kukicha.

Friday, October 21, 2011

MKUBWA NA WANAWE NDANI YA AFROBEAT JUMAMOSI HII

Kijah na mkubwa Fella katika Interview

Baadhi ya wanawe Fella kulia ni Aslay ambae anakimbiza kwa sasa na wimbo wake naenda kusema huyo mwngine ndo yuko mbioni kutoka lakini yeye ni upande wa Taarabu

Hapa wanawe wakiwa Stejini, kitu ambacho kilinishangaza ni kuona Aslay akiimba Taarab yaani huko ndo anakaza zaidi ya huku ambako tumemzoea.. Jamani huyu mtoto ana kipaji cha hali ya juu namtabiria mazuri na atafika mbali sana coz siyo tu ana kipaji ana nidhamu na heshima ya hali ya juu sana tofauti na watoto wengine

Hii picha haikuwa nzuri kwa sababu ya mandhari yenyewe, ni Leah Moudy na Band yake mpya ya Q-Band ambayo anaimiliki yeye na mchumba wake Siz -Q, nao pia utawaona kwenye Afrobeat Jumamosi hii.
Ili kuona mengi kuhusiana na hayo niliyokudokezea hapo juu usikose kuangalia Afrobeat hapo kesho Jumamosi saa moja jioni..

Thursday, October 20, 2011

WIKI ILIYOPITA NILIAHIDI KUWALETEA PICHA ZAIDI ZA SHOW YA PAMOJA KATI YA EXTRA BONGO NA KHANGA MOJA NDEMBENDEMBE!!! HAYA SASA KAZI KWAKO

Banza stone na Rogert Hegga
Banza Stone(Mwalimu wa waalimu)
Mkurugenzi Ally Chocky
Jamani huyu ndo anatufanya mashabiki tufurahie burudani, siyo kila siku waimbaji tuuu tuwakumbuke na hawa pia
Vijana wakiwa kazini hawana masihara maana ndo wanapopatia heshima hapo
Ikafika zamu ya dadaz sasa
Mamaa Aisha madinda
Mamaa Otilia mutoto ya Lindiiiiiii
Ukitaka kuwafaidi zaidi pita pale pande za Meeda kila Jumapili
Mashabiki nao wakaingia kati kucheza, maana wanasema utamu wa ngoma nawe uingie ucheze
Ikafika tym ya khanga moja sasa, hapo unaambiwa kila mmoja alipagawa maana hawa wadada wa hatariiiiii, mmh
Jamani kukaa mbele nako kuna raha na karaha zake, nilimuonea huruma huyu baba sasa kama hakuaga nyumbani ndo balaa linapozuka
Jamani kama ni mzuka basi wa huyu dada ni hatarii maana umempanda hadi balaa
Mwishoni nikakutana na Aisha, hapo tukisalimiana na kupongezana kila mmoja kwa kazi anayoifanya, tukafanya kainterview kidogo
Tukauza sura kama unavyoona then safari ya kurudi home ikaanza

Monday, October 17, 2011

SAKATA LA MGOMO WA WANACHUO WA IMTU UNIVERSITY HATMA YAKE NI LINI????

Baadhi ya wanachuo wa IMTU wakiwa kwenye moja ya maandamano ya mgomo huo

Geti kuu la kuingilia kikuu cha afya IMTU kilichopo mbezi Beach

Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Dr. Shukuru Kawambwa

Sakata hili lilitolewa miezi michache iliyopita na vyombo mbali mbali vya habari kuhusu mgomo huu wa wanachuo hawa.

Ni jambo la kusikitisha sana kuona nchi ambayo ina upungufu mkubwa wa Madaktari, kushindwa kuumaliza mgomo wa Madaktari Wanafunzi ambao sasa umekamilisha miezi miwili, kundi hili la wanachuo limekuwa likikusanyika nje ya Makao Makuu ya Wizara ya Elimu kwa vipindi tofauti bila hitimisho la mgomo huu.

Kwa kutambua umuhimu wa wataalam hawa tunaziomba mamlaka zilizopewa dhamana ya kusimamia na kuongoza  ziumalize mzozo huu ambao madai yao ya msingi ni kulipa Ada kwa Tshs na si US Dollar na pia kulipa ada kubwa tofauti na vyuo vingine vya binafsi (private).

Sisi kama wanafunzi ambao tunaathirika na mgomo huu Bado tuna imani na Serikali ya Mh.Jakaya kikwete na watendaji wake wote, Katibu Mkuu Wizara ya elimu,Tanzania Commision of Universities na Higher Education Student Loan Board tunawaomba waumalize mzozo huu. 
Pesa nyingi zimetumika za walipa kodi kupitia loan board kuwakopesha wanafunzi hawa Tunahitaji sasa wote kwa pamoja kulishughulikie hili tatizo ili tuweze kuendelea na Masomo na mwisho twende kujenga taifa letu changa lenye upungufu mkubwa wa Madaktari.

Source mdau: Henry Kapinga
Mkuu wa mkoa wa lindi, Bw. Ludovick Mwananzira akipata maelezo
kuhusiana na mafuta ya ufuta katika banda la chama kikuu cha ushirika
mkoa wa lindi(Ilulu) alipokuwa akikagua mabanda ya maonyesho ktk
kilele cha siku ya chakula duniani kitaifa mkoani lindi

Wakuu wa wilaya za mkoa wa lindi wakisikiliza hotuba ya
maadhimisho ya siku ya chakula mkoani humo, kutoka kulia,Bi Hawa
mchopa ,mkuu wa wilaya ya Ruangwa,Elias Goroi-Nachingwea na mwisho
mkuu wa wilaya ya Liwale, Paul Chiwile

Mkuu wa mkoa wa lindi akipata maelezo kutoka kwa
wajasiriamali wa manispaa ya lindi

Wadau wa habari nao wakiwa wanaokota baadhi ya
matukio jirani na wakuu wa idara za halmashauri (huyu wa kwanza kulia hapa anaitwa Mwanja Ibadi)

Afisa kilimo wa wilaya ya Lindi Bw. Matunda akikagua Mashine ya kusaga muhogo
Wakazi wa mji wa Lindi waliojitokeza siku hiyo wakishuhudia baadhi ya wasanii waliotumbuiza kwenye maadhimisho hayo

Wadau wakifuatilia matukio kwa umakini kabisa jamani wadau (wa kwanza kushoto hapo ni mama yangu mkubwa)

Maadhimisho ya siku ya chakula duniani kitaifa yamefanyika
mkoani LINDI jana kwa lengo la kutoa nafasi ya kutafakari jinsi jamii
katika ngazi zote zinavyoweza kuhakikisha uzalishaji na upatikanaji wa
chakula cha kutosha chenye lishe bora  kwa wakati wote na kwa bei
nzuri kwa wote.


Akihutubia katika Maadhimisho hayo jana, Kwa niaba ya Waziri wa kilimo na Chakula,Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Ludovick Mwananzira amewataka wakazi wa mkoa huo kuacha matumizi mabaya ya chakula kidogo kinachopatikana na badala yake kutumia kwa uangalifu ili kuondoa tatizo la njaa linaloweza kuukumba mkoa huo.


Sambamba na hilo Mwananzira alieleza jinsi Tanzania ilivyokumbwa na
mabadiliko ya bei za vyakula kunakochangiwa na bei za mafuta na
Nishati nyinginezo.

Naye Msaidizi Mwakilishi mkazi wa shirika la chakula na kilimo la
Umoja wa Mataifa(FAO), Bw Gerald Runyoro akitoa taarifa ya Umoja huo
alielezea sababu zinazosababisha kuwepo kwa watuwenye njaa zaidi ya Bilioni moja
Duniani.

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa mkoa huo Licha ya kuishukuru Wizara
kwa kupanga maadhimisho hayo Mkoani Lindi hawakusita kueleza masikitiko yao kwa kutokuwepo kwa hamasa juu ya Maadhimisho hayo yaliyokuwa na wawakilishi na wakazi wachache waliohudhuria.


Maadhimisho hayo pia yaliambatana na maonyesho ya vitu mbalimbali vya
chakula huku Kauli mbiu ya Maadhimisho ya siku ya chakula duniani kwa
mwaka huu,  ikisema "Bei za vyakula kutoka kuyumba hadi kutengemaa".


Habari hii imeletwa na: Mdau Abdulaziz Video kutoka Lindi

JE UNAWEZA KUMPATA MTU MWENYE MAPENZI YA AINA HII KATIKA DUNIA YA LEO?

Wapenzi na wachumba katika dunia hii ni wengi sana, lakini wakweli ni wangapi kati yao? Ni watu wangapi ambao husema kweli katika mapenzi yao? Ni wangapi ambao humaanisha wanachokisema? Ni wangapi ambao wanaweza kuendelea kubaki na wapenzi wao pindi wapenzi hao wanapopata matatizo kama vile ulemavu au ugonjwa usiotibika?

Hii ni stori pekee ya mapenzi ya kweli niliyowahi kuisikia...........

Huyu mama ni mtu mwenye bahati sana ( Anaitwa Rosemarie "Rose" Siggins)

Huu ni mfano mzuri wa Familia ya kuigwa

Kwa kweli kwa namna hii huyu mama anaweza kuishinda hali yake ya kuwa mlemavu na kujihisi yuko sawa na wengine

Ni mama wa watoto wawili kama unavyoona na anafurahia maisha na familia yake

Mama na wanae
Akimnyonyesha mwanae mwenyewe 

Matembezini na familia
Wakiwa shopping na maisha yanaendelea anaenjoy zaidi ya wewe ambae umetimia

Pamoja na yote mwisho wa siku jukumu la kumlea mtoto wake linamsubiri na anaweza kulimudu kama kawaida, kama umegundua ana kama kabaiskeli hivi kakutembelea

Kiukweli huu ni mfano mzuri sana wa kuigwa kwa huyu baba na kama wapenzi wote tungekuwa hivi basi maisha yangekuwa na furaha na yasiyo na stress wakati wote, lakini upande wa pili huku ni full stress aiseh mpaka wengine wanadiriki kusema wao mapenzi basi lakini mwisho wa siku wanagundua kuwa haiwezekani na yataka moyo kumudu uamuzi huo na hatimae wanarudi tena kundini... Ila kikubwa ambacho nimejifunza katika ulimwengu huu wa mapenzi ni uvumilivu na kuaminiana tu basi hiyo ndiyo dawa ya kutibu ugonjwa huu wa stress katika suala zima la mapenzi.

UJUMBE HUU UENDE KWA WOTE WALIO KWENYE NDOA NA WALE AMBAO WAKO KWENYE UHUSIANO WA KAWAIDA TU, MAANA KUNA KITU CHA KUJIFUNZA HAPO KWETU SISI SOTE!!!!

Thanks my Boy Andrew Zomari kwa habari hii.