Thursday, August 18, 2011

CHAMELEONE AREJEA UKRISTO




Hatimaye mwanamuziki Jose Chameleone kutoka Uganda amerejea katika dini yake ya ukristo siku 6 tangu alipobadili dini na kuwa muislamu.

Chameleone ameweka bayana kama ifuatavyoNilihudhuria sala ya Ijumaa na mke wangu Daniella alikua anajua,ili niwe karibu na mungu,lakini ilipokelewa kwa hisia tofauti na kushangaa jinsi alivyopokelewa msikitini hapo na kuishia kutoa shahada,neno ambalo linamtambulisha mtu aliyeigia kwenye dini ya kiislam na kuahidi kuamua kurudi kwenye dini yake ya zamani...alizungumza hayo nyumbani kwake Seguku,Entebbe Road-Uganda alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Aliongeza kuwa“Bado nampenda Daniella na wala sijaachana nae wala siwezi kuishi bila yeye na kukiri kuwa aliishi kwa shida siku hizo 6 ambapo kwa sasa amerudi kwenye dini yake ili aelewane na familia yake na wakwe zake

Pia alionesha simu yake alipokuwa anampigia mke wake Daniella bila ya kuzipokea ambapo pia alibadili caller tune yake iliyokuwa na wimbo wa Chameleone na kuweka wimbo wa Judith Babirye wa Mukama Wanjagala, lakini pia Chameleone alikuwa kwenye mtihani mkubwa kutoka kwa baba yake,Mzee Mayanja na Mashangazi  na baba yake alitamka kuwa hamtambui Jaffar Gadaffi ila anamtambua na Joseph Mayanja.

Chameleone Jumapili hii atahudhuria kanisani ambapo alifunga ndoa na Daniella,Mutunga Binna Church na mwisho alimalizia kwa kusema....my family is so important,I love my God but this thing of converting,and leaving all my family in a mess,still it won’t please my God”....

No comments:

Post a Comment