Thursday, December 22, 2011

SALUTE KWA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA TANZANIA KWA KAZI KUBWA WALIYOIFANYA

Wakizunguka huku na kule katika kuangalia usalama
Hawa nao wakiwa wameshuka kwenye magari yao

Kikosi cha kutuliza Ghasia na Jeshi la wananchi wakihakikisha mambo yanaenda sawa(Walifanya kazi kubwa sana hawa jamaa)
Askari wa Jeshi la wananchi TZ (JWTZ) wakiendelea na shughuli ya uokoaji
Askari akiongoza watu kupita katika enneo hilo

Picha hizo zote zinaonyesha namna vikosi vya ulinzi na usalama vikisaidia zoezi la uokoaji wa watu waliopatwa walioathirika na mafuriko katika eneo la Jangwani jijini Dar Es Salaam, ambapo pia Askari hao walifunga utumiaji wa barabara hiyo kwa vyombo vya moto kwa muda mrefu mpaka pale maji yalipokauka, halikadhalika watembea kwa miguu pia walizuiwa kutumia barabara hiyo kwa muda kwa ajili ya usalama wao.

Kwa kweli tunapaswa kuyashukuru sana majeshi yetu kwa namna yalivyoonyesha uzalendo kwa kuacha shughuli zingine zote na kuingilia kati suala hili la maafa ya mafuriko.. SALUTE KWAO.

Nilikuwepo eneo la tukio lakini kwa kazi maalum, hivyo nikashindwa kupiga picha lakini namshukuru Ankal michuzi kwa kuniwezesha mimi kupata Picha kupitia michuzi.blogspot

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AMEWAASA WANANCHI KUTOA MISAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO

Baadhi ya waathirika wa mafuriko wakisubiri kuokolewa

Nyuma ambayo imeathirika kutokana na mafuriko hayo

Hapa ni Airport DSM hali ilivyokuwa jana

Hali bado ni tete na baadhi ya watu wakijaribu kuokoa maisha yao na ya watoto
Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Said Mecky Sadick akizungumza na vyombo vya habari.
Hali bado ni tete katika jiji la Dar Es Salaam kama ambavyo vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kuhusiana na janga la mafuriko lililoathiri Familia nyingi sana kwa kupoteza makazi yao na maisha ya ndugu zao kutokana na mvua iliyonyesha kwa siku ya tatu leo mfululizo.

Kama ambavyo tunafahamu linapotokea janga kama hili panahitajika misaada mingi sana kama vile maji, chakula, mavazi, n.k. hivyo Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Bw. Said Mecky Sadick amewaomba wale wote wenye lengo la kutoa msaada wapeleke misaada hiyo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iliyopo Ilala Boma jijini Dar Es Salaam.

Bw. Sadick amezungumza hayo wakati wa mahojiano maalum aliyoyafanya na East Africa Radio katika walipotaka kufahamu mambo mbalimbali yanayoendelea kutokana na maafa hayo yaliyoikumba Taifa.

Picha kwa hisani ya Eatv no.1 Youth Channel

Tuesday, December 20, 2011

KANUMBA ADAIWA KUPOTEA KWENYE MISITU YA YANGADOU REINFOREST HUKO CONGO

Kuna habari zimeenea kwenye mitandao kuwa Movie star wa Bongo Steven Kanumba (Pichani)amepotea huko katika misitu inayofahamika kama Yangadou Reinforest Jamhuri ya watu wa Kongo, alipokuwa akishoot Movie mpya inayoitwa Mother Land.
Habari hiyo imeendelea kusema kuwa Kanumba alipotea kwa saa 24 tangu siku ya Dec 19, 2011 baada ya kugombana na Director wa Movie hiyo na yeye (Kanumba) kuamua kuondoka katika eneo hilo ambalo walikuwa wameweka kambi kwa ajili ya Kushoot Movie hiyo na mpaka masaa 24 baadae alikuwa hajaonekana hali iliyopelekea wenzake kuanza kumtafuta kwa kutumia Helikopta bila ya mafanikio lakini pia inasemekana kuwa katika misitu hiyo kuna kundi la waasi ambao wanaishi na wamekuwa wakipoteza maisha ya watu mara kwa mara.

Baada ya kuisoma habari hii ilibidi nimtafute Kanumba kwa njia ya simu ili kufahamu ukweli wa jambo hili na mwenyewe akathibitisha kuwa yeye yupo hapa hapa Bongo na taarifa hizo siyo za ukweli.. Nimeshusha pumzi sasa baada ya kuongea nae maana mmh niliogopaaa.

BENDI TANO ZILIZONIKUNA MWAKA 2011

African Stars Twanga pepeta bado wako kileleni kwa kushika namba moja kutokana na nyimbo zao walizoziipua hivi karibuni za "Dunia daraja" utunzi wa Charles baba na"Penzi la shemeji" ya kwake Muumini Mwinjuma
Extra Bongo wazee wa kizigo wameshika namba mbili kutokana na Umahiri wao wawapo stejini lakini pia kwa nyimbo zao za "Mtenda akitendewa" na "Fisadi wa mapenzi"

Bendi changa kabisa hapa Bongo ya Mapacha watatu nayo imeshika namba tatu kutokana na Wimbo wao Shika ushikacho na Gari bovu utunzi wa mpiga kinanda wao Erasto Mashine
Salute kwao Akudo Impact kwa nuimbo zao "Umefulia" na "Umejificha wapi" ambazo zimewapa nafasi ya tatu katika chati hii
Fm Academia "wazee wa Ngwasuma" wameshika nafasi ya tano kwa nyimbo zao Heshima kwa mwanamke na Usiku wa giza

Jamani huu ni mtazamo wangu tuu inawezekana na wewe una Bendi zako ambazo unaona zimekukuna zaidi...kwa hiyo masela msijenge chukiiii!! hahahaha

Monday, December 19, 2011

MCT YATOA MAFUNZO KWA WANA EATV


Picha zote hapo juu zinaonyesha wanasemina wakifuatilia mafuzo kwa umakini
Mmoja kati ya wawezeshaji Bi. Haura Shamte mwandishi wa habari wa siku nyingi
Siku ya Jumamosi ya Dec 17, 2011 MCT kwa kushirikiana na EATV waliandaa mafunzo kwa wafanyakazi wa EATV na Radio yaliyolenga kuwakumbusha wafanyakazi wake baadhi ya mambo yanayohusiana na Tasnia nzima ya habari.

Tulijifunza  vitu vingi sana maana wanasema Elimu haina mwisho ingawa kuna watu wana uzoefu mkubwa sana wa hii kazi ya habari lakini nao walipata nafasi ya kukumbushwa baadhi ya vitu muhimu ambavyo havipaswi kusahaulika katika kazi.

Baadhi ya vitu hivyo tulivyojifunza ni pamoja na Namna ya kuandika habari, Ipi stori na ipi siyo stori, maana kuna baadhi ya waandishi wao wanajiandikia tu hata hawaangalii uzito wa hiyo habari,Interview Techniques na hili nalo pia ni muhimu sana maana ukiangalia na kusikiliza vipindi vyetu vingi hapa nchini utaona aibu kutokana maswali yanayoulizwa inaonyesha wazi kuwa watu wamesahau au hawajui namna ya kuuliza maswali.

Pia tulipata bahati ya kufahamu tofauti ya Mwandishi na mtangazaji maana siku hizi mtu akiwa mtangazaji anaitwa mwandishi lakini je hii ni sahihi?? Jibu ni kwamba inategemea maana wanasema mtu yeyote ambaye yuko kwenye Media ni mwandishi sababu wakati mwingine anashiriki kwa njia moja ama nyingine katika upatikanaji wa hiyo habari na wakati huo huo anaweza asiwe mwandishi pia.

Jamani tulijifunza vitu vingi saaaaanaaa nikisema niandike vyote hapa nitawachosha wadau ila Mafunzo haya yataendelea pia Jumamosi ijayo na tutaendelea kufahamishana yale tuliyojifunza.

Monday, December 12, 2011

SEUN KUTI NDANI YA TAMASHA LA AFROBEAT EXPLOSION

Mwanamuziki Seun kuti pamoja na kundi lake liitwalo Egypt 80 Band wanatarajia kufanya onesho katika Tamasha la Afrobeat Explosion Jumamosi ya Tar 24 Dec 2011 katika ukumbi wa Terra Kulture, Tiamiyu savage kuanzia saa 2 usiku,  kiingilio kitakuwa N3000 kwa Single na N5000 kwa Double..
Haya wapenzi wa burudani hizi hii inawahusu sana na sasa kazi ni kwenu

Thursday, December 8, 2011

VYOMBO VYA HABARI VINACHANGIA KUUPOTEZA MUZIKI WA ASILI

John Kitime
Mwanamuziki mkongwe nchini Tanzania John Kitime amepeleka kilio chake kwa vyombo vya habari kuwa ni moja kati ya vitu vinavyochangia katika kuupoteza muziki wa asili

Akizungumza na kipindi cha Afrobeat katika kumbukumbu ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara, na muziki wetu Tanzania Kitime alisema hayo pale alipoulizwa kwa upande wake anafikiri ni nini kinachangia kupotea kwa muziki wa asili wakati muziki wa kisasa unapanda, alisema Muziki huo haujapotea kwa sababu kuna vikundi vingi vya Muziki wa asili kama vile ngoma ambavyo vinatumbuiza katika sehemu mbalimbali lakini havisikiki kwa sababu vyombo vya habari haviutangazi na badala yake unatangazwa muziki huo wa kisasa ambao unaonekana kuwa upo juu lakini si kweli, ila ukweli ni kwamba muziki wa asili haupewi nafasi ya kutangazwa au kupigwa kwenye vyombo vya habari.

Akizungumzia kuhusu tungo za sasa hivi kuzungumzia zaidi suala la mapenzi, Kitime alisema hilo linatokana na malezi ya watoto wa sasa hivi si kama ya zamani ambapo wakati huo vijana walifundishwa kuwa Lugha ya Staha tofauti na sasa hivi vijana wanaona kawaida kutamka maneno makali hasa ya mapenzi hadharani bila Staha kutokana na namna walivyolelewa na wazazi wao na jamii inayowazunguka, akaongeza kuwa uwingi wa Studio pia unachangia tofauti na zamani ambapo studio ya kurekodia ilikuwa moja tu ya RTD ambapo ilikuwa kabla wimbo wako hujaurekodi lazima upitiwe ili kuangalia maneno uliyoyatumia na kama kuna tatizo uanaambiwa urekebishe ndipo unarekodi na kama haueleweki kabisa hauruhusiwi kurekodi lakini sasa hivi watu wako kibiashara zaidi hawazingatii mashairi.

Kuhusu suala la maendeleo ya muziki amesema sasa hivi kuna maendeleo makubwa sana kwa sababu hata jamii yenyewe imekubali kuwa muziki ni kazi kama kazi zingine ndiyo maana sasa hivi kuna wanawake wengi sana wanafanya kazi hiyo tofauti na zamani ambapo mwanamke akionekana kwenye jukwaa la muziki anaonekana ni mhuni jambo ambalo liliwakatisha tamaa wanawake wengi ingawa walikuwepo wachache waliojitoa.

The kilimanjaro Band ilivyoutangaza mlima Kilimanjaro

The kilimanjaro Band
Waziri Ally wa Kilimanjaro Band akifanya vitu vyake

 Naamini ulikuwa hufahamu hata jina la Kilimanjaro Band ( Wananjenje) lilitokana na nini, sasa leo nakufahamisha japo kwa uchache tu kuhusiana na Bendi hiyo.
Kilimanjaro Band hapo mwaka 1973 wakati inaanzishwa iliopewa jina la Revolution Band na ikaendelea kufahamika hivyo mpaka mwaka 1989 Band hiyo ilipopata Safari ya kwenda Uingereza ndipo hapo Idea ya kubadili jina ilipokuja na jina lililofikiriwa ndo lilikuwa hilo The Kilimanjaro Band ikidaiwa kuwa jina la mwanzo la Revolution Band limekaa kizungu zaidi kwa hiyo hata huko waendako wenyeji wangewashangaa ndipo wakaamua kuiita Kilimanjaro wakiwa na maana ya kuutangaza mlima Kilimanjaro.
Na kama mawazo yao yalivyowatuma ndivyo ilivyokuwa maana walipofika huko wenyeji walishangaa sana kusikia Bendi ya Tanzania inatumia jina hilo wakiamini kuwa Mlima huo upo nchini Kenya, hivyo ikabidi wao(Kilimanjaro Band) waanze kuwaelimisha watu kuwa wadhaniavyo siyo sahihi kwani mlima huo upo kwenye ardhi ya Tanzania, ndipo wakaanza kufahamu na ndo hivyo mpaka leo inafahamika hivyo ingawa kuna baadhi ya watu bado wanaamini kuwa mlima huo upo nchini Kenya, hivyo sisi kama Watanzania tunapaswa kutumia nafasi tunazozipata kwa kuutangaza mlima wetu huo na Nchi yetu kwa ujumla..
Maelezo haya ni kwa mujibu wa Wazri Ally mmoja kati wa wanamuziki wa The kilimanjaro Band a.k.a wana njenje ambae aliyaeleza haya yote alipokuwa akizungumza na kipindi cha Afrobeat kinachorushwa na Eatv ambapo tulitaka kufahamu mambo mbalimbali kuhusiana na muziki ndipo pamoja na mengi aliyotueleza tukayapata na hayo kuhusu Bendi yao na akaongezea kuwa jina la Njenje lilitokana na wimbo ule unaoitwa Njenje ambao ulivuma na kupendwa sana na bado unaendelea kupendwa mpaka sasa, hivyo kutokana na mapenzi ya watu kwa wimbo huo ndipo wakaibatiza Bendi hiyo kwa jina la Njenje.