Wednesday, August 10, 2011

K-MONDO KULA SHAVU BSS

K-MONDO SOUND kazini

MANGUSTINO a.k.a TICHA MANGU kazini

MANGUSTINO katika Pozi
Bendi ya Muziki ya K-MONDO SOUND ya jijini DSM inaendelea na Show zake kama kawaida katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kutokana na maombi ya Mashabiki wao kuwataka waendelee kuwapa burudani.


Akizungumza na Blog hii Rais wa bendi hiyo RICHARD MANGUSTINO amesema wameamua kuendelea na Show zao kama kawaida kutokana na maombi ya mashabiki wao wengi ambapo watakuwa wakipiga mara tatu kwa wiki yaani Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.


Ameongeza kuwa pamoja na kuendelea na Show lakini pia watakuwa wanafanya mazoezi makali kwa ajili ya kufanya vizuri katika Shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Search(BSS) ambapo wana mkataba wa kupiga LIVE nyimbo ambazo zimekuwa zikiimbwa na Washiriki wa shindano hilo, halikadhalika mazoezi hayo yanahusisha pia maandalizi ya Mwanamuziki wao Vumi a.k.a "Queen of the Night" ambae amechaguliwa katika mashindano ya Tuzo za Afrika Mashariki na Kati, ambayo yatafanyika Septemba mwaka huu jijini Nairobi-Kenya.

2 comments: