Thursday, June 30, 2011

MSONDO NGOMA MUSIC BAND KUWEKA KAMBI NDANI YA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO

(PICHANI juu na chini ni Baadhi ya wanamuziki wa Msondo ngoma wakionyesha vitu vyao jukwaani)

Bendi kongwe ya muziki wa Dansi nchini, (MSONDO NGOMA) Baba ya muziki,IJUMAA hii inatarajia kufanya onyesho maalum lijulikanalo kwa jina la MTANZANIA JIVUNIE katika kijiji cha Makumbusho JIJINI DAR ES SALAAM.

Meneja wa Bendi hiyo SAID KIBIRITI amesema onyesho hilo maalum limeandaliwa na bendi yake kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji cha MAKUMBUSHO, na Baada ya hapo bendi hiyo itakuwa ikipiga Show katika kijiji hicho kila siku ya IJUMAA

MAALIM GURUMO(Kiongozi wa Bendi)

Bendi ya Msondo ngoma kwa sasa inatamba na kibao kipya kijulikanacho kama SULUHU kilichotungwa na SHABAN DEDE, Hivyo idadi ya nyimbo mpya za msondo kufikia TANO ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ALBUM yao mpya

SAID MABERA(Mpiga gitaa la Solo wa MSONDO)

KIBIRITI amewaomba wapenzi wa Bendi hiyo kujitokeza kwa wingi ili kuipa SUPPORT Bendi yao hiyo


ROMARIO kazini

Wednesday, June 29, 2011

JAMANI TUTOE SUPPORT KWA NGOMA ZETU ZA ASILI


(Hapo juu na chini ni kikundi cha Jivunie kikitoa burudani )
Kuna tabia za baadhi ya watu kuona kuwa ngoma za asili ni kitu cha ajabu sana na wale wanaopenda kuhudhuria maonyesho ya ngoma hizo ni washamba au watu waliopitwa na wakati.
Mi nafikiri wenye haya mawazo ndo washamba na wamepitwa na wakati kwa kuthamini vitu vya kigeni, jamani utandawazi usitufanye tudharau vya kwetu tutakuwa watumwa.. Jamani badala ya kumalizia Weekend zetu kwenye CLUBS mbalimbali kila siku basi si vibaya siku moja moja tukipita kwenye hizo ngoma..
Kuna vikundi vingi tu vya ngoma ambavyo vinatoa burudani katika sehemu mbalimbali kama vile kijiji cha MAKUMBUSHO na ukipita utakuta wazungu kibaaoo na wabongo wa kuhesabu, tubadilike jamani na tuwape Support ndugu zetu hawa........     PICHA KWA HISANI YA michuzi.blogspot.com

Tuesday, June 28, 2011

MAPACHA WATATU NDANI YA STEJI MOJA NA WAKALI WA BONGO FLEVA

Band ya muziki wa Dansi iliyojipatia umaarufu mkubwa bongo MAPACHA WATATU inayoongozwa na JOSE MARA, KHALID CHOKORAA na KALALA JUNIOR wanatarajia kufanya onyesho kali kwa kushirikiana na wakali wa Bongo Fleva  JUMAPILI Tar 03.07.2011
Akizungumza na Blog hii muandaaji wa Show hiyo Kali Suleiman Semunyu amesema wana Bongo Fleva hao watakaoangusha Show na Mapacha Watatu ni ALLY KIBA alietamba na vibao vikali km Mac Mugan, Cinderella, Hands across the World alioshirikiana na wakali kibao akiwemo R-KELLY na nyinginezo.
ALLY KIBA
 BARNABAMsanii mwingine ni ELIAS BARNABAS a.k.a BARNABA kutoka THT aliyetamba na vibao vingi km Mbalamwezi, SMS vingine vingi

WAKONGWE WA MUZIKI TANZANIA KUTOA ALBUM YA NYIMBO ZA ZAMANI

(Abdul Salvador a.k.a Father Kidevu)
Wanamuziki wakongwe Tanzania wamejipanga na kuamua Kutoa Album ya nyimbo za zamani, akizungumza na kipindi cha AFROBEAT cha EATV mmoja kati ya wanamuziki hao aliyetamba enzi hizo kwa umahiri wake wa kupiga Kinanda kwa kutumia kidevu ABDUL SALVADOR a.k.a FATHER KIDEVU amesema nyimbo watakazorekodi ni zile zilizotamba miaka ya 1961 mpaka 1991, wameamua kufanya hivyo katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania. Ameawataja baadhi ya wakongwe waliomo katika mpango ni pamoja na Kanku Kelly, Mzee Gururmo,, John Kitime, King Kikii, Ndalla Kasheba na wengineo.
Father kidevu na Kanku Kelly wa KILIMANJARO CONNECTION
Wazee wakiwa mazoezini
Babu njanje mazoezi yakiendelea
Mzee Gurumo wa MSONDO NGOMA
King Kikii na Ndalla Kasheba
Baadhi ya Wakongwe wa Muziki TZ katika picha ya pamoja

VIMWANA MANYWELE 2011 WATAMBIANA

Wakati shindano la kumsaka Manywele kimwana wa Twanga pepeta likielekea katika hatua ya Fainali, Vimwana  kumi  walioingia katika hatua hiyo wameibuka na kutambiana kuwa kila mmoja ndiye mwenye uwezo na vigezo vya kuibuka na ushindi
Nae Matron wa Vimwana hao ambae pia ni kimwana mstaafu wa mwaka 2007 ambae alishika nafasi ya pili HUSNA IDD a.k.a SAJENT amesema hana mashaka na vimwana hao kwa kuwa kila mmoja amefanya maandali ya kutosha na yeyote kati yao anaweza kunyakua ushindi
Kwa upande wake Mratibu wa shindano hilo MAIMARTHA JESSE amesema kila kitu kimekamilika ikiwa ni pamoja na zawadi ya duka la vipodozi lenye thamani ya Shs Mil. 5, kinachosubiriwa ni siku ya mpambano ili zijulikane mbivu na mbichi. Fainali hiyo ya manywele kimwana wa Twanga pepeta itafanyika Tar 08.07.2011 katika ukumbi wa Ubungo Plaza kwa UDHAMINI mkubwa kabisa wa AFROBEAT ya EATV na  AFROSUNDAY ya EAST AFRICA RADIO

Monday, June 27, 2011

AKUDO IMPACT KUTAMBULISHA NYIMBO ZAO MPYA

Bendi ya muziki wa Dansi, Akudo Impact a.k.a Vijana wa masauti wanatarajia kutambulisha nyimbo zao mpya zipatazo tano hivi karibuni
Akizungumza na kipindi cha AFROBEAT kupitia EATV kinachokwenda hewani kila JUMAMOSI saa 1 Kamili JIONI, Rais wa Bendi hiyo CHRISTIAN BELLA amesema AKUDO bado iko imara tofauti na uvumi uliopo kuwa inaweza kuvunjika.
Bella ameongeza kuwa mashabiki wasisikilize maneno hayo ambayo hata yeye (BELLA) hajui yametokea wapi na wakae tayari kupokea nyimbo zao mpya zikiwemo umejificha wapi na umefulia ambazo zinatamba katika vituo mbalimbali vya Redio hapa nchini.....    ILI KUZISIKIA NYIMBO HIZO, FUATILIA AFROSUNDAY YA EAST AFRICA RADIO KILA JUMAPILI SAA 12 KAMILI JIONI



NDOTO YA JAYDEE NA MTUKUDZI YATIMIA

Mwanadada anaetisha katika Game ya muziki BONGO ambae pia ni mmiliki wa Machozi Band, LADY JAYDEE amekamilisha ndoto yake baada ya kufanya ngoma na Mwanamuziki mkongwe kutoka Zimbabwe OLIVER MTUKUDZI, Ngoma hiyo ambayo ipo jikoni inafahamika kwa jina la MIMI NI MIMI imerekodiwa usiku wa Jumatatu iliyopita.

Lady Jydee na Oliver Mtukudzi kazini

Mazoezi inafaa pia siku moja nawe uweze kulichezea

Mazoezi muhimu kabla ya kuanza kazi

Mzungu kichaa nae alikuwepo

Siku za hivi karibuni JAYDEE NA MTUKUDZI waliwahi kufunguka kupitia Ting'a namba wani kwa Vijana EATV katika kipindi cha Afrobeat kila mmoja akidai kuwa ana ndoto ya kupiga kolabo na mwenzake

PICHA kwa Hisani ya Ladyjaydee.Blogspot

NAPE APOKELEWA KWA FURAHA MKOANI LINDI

Katibu wa NEC Itikadi na uenezi CCM, NAPE NNAUYE  akikabidhi Kabrasha kwa Mwenyekiti wa CCM kata ya Mtanda Mh.Issa Malocho katika mkutano wake na Wajumbe wa mashina katika ukumbi wa Lindi Oceanic Hotel, Lindi Mjini
Wajumbe wa mashina wa KATA zote 18 za wilaya ya Lindi wakifuatilia kwa umakini mkubwa KIKAO hicho
NAPE NNAUYE akijumuika kutoa burudani na kikundi cha sanaa ya ngoma alipofanya mkutano wa Hadhara katika uwanja wa Fissi mjini Lindi
Nape akiwapungia mkono kwa ishara ya kuwaaga wanachama wa CCM waliohudhuria mkutano
NAPE kiwahutubia wananchi wa Kilwa

NAPE akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Bw. Ally Mtopa wakati wa mkutano wake wilayani Kilwa

PICHA KWA HISANI YA LINDI PRESS CLUB(LPC)

Thursday, June 23, 2011

M-NET YAZINDUA AFRICA MAGIC SWAHILI


M-NET AFRICA wameanzisha kituo kipya cha kurushia matangazo ambacho kimezinduliwa jana kinachofahamika kwa jina la AFRICA MAGIC SWAHILI.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa M-NET Biora Alabi, kituo hicho kitakachoanza rasmi Julai mosi kitakuwa kikirusha matangazo yake kwa Lugha ya kiswahili ili kuikuza Lugha hiyo, lakini pia itaonyesha Filamu na muziki wa Kiswahili tu.

Wawakilishi wa M-NET katika kukamilisha uzinduzi huo

Waalikwa waliohudhuria hafla hiyo ambayo imefanyika katika hotel ya MOVENPICK


Upande wa Tasnia ya Filamu nao hawakubaki nyuma walikuwepo kuwakilisha, hapo juu ni JB moja kati ya waigizaji ambao wananifurahisha sana

Aunt Ezekiel nae kama kawaida yake hapendi kuhadithiwa lazima ajionee mwenyewe.

Kanumba The Great mmoja kati ya waigizaji bongo nae alikuwepo, hapo akifafanua jambo


The Greatest nae akiwakilisha akiwa na Cloud

Mama lao katika movie Suzan Lewis nae akiwaongoza wanae

Mtu maarufu kwa kuiga sauti za watu Steve Nyerere nae akitema cheche zake

KWA WALE WAPENDA MOVIE ZA KIBONGO KAMA MIMI KAZI NI KWENU JAMANI KUIFUATILIA TU AFRICA MAGIC SWAHILI

Saturday, June 18, 2011

HALI YA BAMBO BADO NI TETE

Muigizaji na mchekeshaji mkongwe bongo ambae kwa sasa ni muajiriwa wa EATV kupitia ZE COMEDY SHOW, Dickson Makwaiyo a.k.a Bambo, ambae wiki iliyopita aliripotiwa kupata ajali ya pikipiki na kusababisha kuvunjika kwa mfupa sehemu ya goti hali yake bado si nzuri.
Pichani juu ni pikipiki na gari iliyosababisha ajali ya Bambo

Hali ya Bambo ilikuwa inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji lakini katika hali isiyo ya kawaida habari zilizotufikia leo zinasema kuwa Bambo alianza kutokwa damu masikioni na baadae kufanyiwa uchunguzi zaidi na majibu zaidi yatapatikana kesho


Mtanga na Kicheko kutoka ZE COMEDY ya EATV wakimjulia hali Bambo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini DSM.