Tuesday, August 9, 2011

DUH!!! BOB RUDALA, KUTOKA UBWANA AFYA HADI UANAMUZIKI

BOB RUDALA(Pichani)
Katika kile ambacho sikukitegemea kabisa wala kukifikiria kabisa katika hisia zangu leo ndo nimefunguliwa masikio yangu!!!!


Kumbe Bob Rudala kabla hajawa mwanamuziki alishawahi kuwa Bwana afya wa Manispaa moja hapa hapa jijini Dar Es Salaam, lakini kutokana na mapenzi yake katika Muziki ndo hivyo mwisho wa siku ikabidi abaki kwenye muziki tuu...


Story iko hiviii, tangu alipokuwa mdogo alikuwa anapenda sana muziki hivyo alikuwa akitumia muda wake mwingi sana kusikiliza muziki wa aina tofauti tofauti na alipofikia umri mkubwa kiasi akatengeneza Gitaa lake na kuwa anajifunza kulipiga, hali ambayo haikuwa ikimpendeza baba yake ambae alikuwa akitaka asome na baadae kumshauri ajiunge na Chuo cha afya kwa sababu baba yake pia alikuwa bwana Afya wa Manispaa hapa Dar, nae akatii akajiunga na chuo huko wilayani Newala mkoani Mtwara.

Alipomaliza masomo yake na kurejea Bongo akaendelea na kazi ya ubwana afya wakati huohuo akiendelea pia na mambo yake ya muziki na kuendelea kujifunza kupiga Gitaa kila anapotoka kazini,  hali ambayo ilikuwa ikimchukiza sana baba yake ikabidi awe anapiga Gitaa lake kwa siri, lakini kama unavyojua mapenzi ya mtu hayazuiliki siku moja akavunja ukimya na kuzungumza na mzazi wake kuwa anaomba aache kazi hiyo ya Ubwana afya ili aendelee na Muziki na mwisho wa siku baba akaelewa, ndo hivyo kama unavyoona anaendelea na muziki hadi leo na anaifurahia kazi yake... 


Ameongea mengi sana Bob Rudala lakini uhondo wa ngoma wanasema uingie mwenyewe ucheze hivyo msikilize mwenyewe kwenye Afrobeat wiki hii kupitia Eatv pekeeeee!!!

No comments:

Post a Comment