Friday, August 19, 2011

BOB HAISA AWAFUNDA WANANDOA

Mkali wa muziki ya miondoko ya mduara aliyetamba na vibao kemkem kama vile Nipe mgongo, ubeleko na nyingine nyingi tu BOB HAISA amesema baada ya kukaa kimya kidogo sasa amerejea kwa style ya kutoa funzo kwa wanandoa ambapo mapema mwezi huu ametoa Album yake iliyobeba jina la "Meza ya wanandoa"

Akizungumza na blog hii leo asubuhi BOB HAISA amesema ameamua kuja kwa style hiyo baada ya kugundua kuwa nyimbo za style hiyo ndizo zenye soko na hupendwa na watu wengi sana ambapo zimekuwa zikipata promo kwa kuwa hutumiwa zaidi kwenye mkusanyiko wa watu kama vile harusi, kitchen party na sherehe zingine zinazohusiana na masuala ya harusi.

Akizungumzia album yake hiyo ya Meza ya Wanandoa, amesema ina nyimbo 10 zenye mafundisho ya maisha ya ndoa ikiwemo BHATOJA SHISHO (inayozungumzia kukutana kwa wazazi wa pande mbili za mume na mke) ambayo ilitoka mwaka 2000 lakini haikupata umaarufu kwa kipindi hicho na badala yake imekuwa ikipendwa sana kwa sasa akasisitiza kuwa wimbo huo ndio uliompa msukumo na ushawishi wa kuja na Album yenye ujumbe huo wa ndoa na kuweka wazi kuwa Album zake zote zijazo zitabeba ujumbe huo wa ndoa.

Ameongeza kuwa Album hiyo anaisambaza mwenyewe kwa kushirikiana na wauzaji wa mitaani na maduka mbalimbali jijini Dar Es Salaam, uamuzi uliotokana na kukwepa wanyonyaji wa kazi za wasanii.

Amezungumza mengi sana lakini utamsikia zaidi kupitia AFROBEAT SOON, hivyo usikae mbali na Runinga yako ya EATV.. Kumbuka AFROBEAT ni kila jumamosi saa moja kamili jioni

1 comment: