Tuesday, August 2, 2011

KASSIM MAPILI AMLILIA MARIJANI RAJABU

MZEE KASSIM MAPILI

MAREHEMU MARIJANI RAJAB
Mkongwe wa Muziki wa Dansi, Mzee KASSIM MAPILI ameonyesha hali ya kumlilia Mwanamuziki ambae amechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa Muziki wa Dansi hapa nchini, Marehemu MARIJANI RAJABU.


Akizungumza na kipindi cha Afrobeat kinachorushwa na Eatv kupitia kipengele cha COPI KALE ambacho huzungumzia muziki wa zamani, mzee MAPILI amesema katika wanamuziki ambao hatoacha kuwakumbuka na kuwalilia ni pamoja na Marehemu Marijani kwa kuwa alikuwa nguzo ya Muziki wa Dansi hapa nchini si tu kwa kuwa na sauti nzuri na yenye kuvutia bali pia kwa umahiri wake wa kutunga nyimbo zenye ujumbe ambao humgusa mtu yeyote ambae atapata nafasi ya kusikiliza nyimbo hizo.

Akitolea mfano wimbo wa MWANAMEKA ambao ni moja kati ya nyimbo za Marijani Rajab amesema  wimbo huo umebeba ujumbe mzito wa Mapenzi ambao humgusa kila mtu na wenye Rika tofauti tofauti na ndio maana ulikuwa ukipigwa wakati huo kila mtu anafurahi kuusikia.

"MWANAMEKA ni moja kati ya nyimbo nyingi za MARIJANI RAJABU ambazo zimebeba ujumbe mzito wa mapenzi na ulikuwa ukipigwa wakati huo kila mtu anafurahi kuusikia, kwa kweli Tanzania imepoteza mtu muhimu sana ambae alikuwa ni nguzo kubwa ya muziki wa Dansi hapa nchini"

Kwa mengi zaidi, usikose kufuatilia AFROBEAT Jumamosi hii.... USIKOSEEEEE!!!

No comments:

Post a Comment