Saturday, August 20, 2011

HUSSEIN JUMBE ATOA WOSIA KWA MKURUGENZI WA MASHAUZI CLASSIC

Mwanamuziki nguli wa dansi nchini Hussein Jumbe amemtaka mmiliki na mkurugenzi wa Bendi mpya ya muziki wa Taarab nchini "Mashauzi Classic" Aisha Ramadhani a.k.a Isha Mashauzi kutojibweteka na kujiona amefika baada ya kuanzisha bendi hiyo na badala yake aone kama huo ndio mwanzo, hivyo aongeze juhudi zaidi ili kulifanya kundi hilo liwe tishio na mfano wa kuigwa kwa makundi mengine.

Jumbe ameyasema hayo leo wakati wa utambulisho wa Kundi hilo la "Mashauzi Classic" katika kambi yao iliyopo kinondoni mkwajuni.
Jumbe ambaepia ni mmiliki wa "Talent Band" ameendelea kumsihi Isha kuwa awajali na kuwathamini wanamuziki wake wote bila kuwabagua ili kujenga umoja na ushirikiano ili kuliboresha kundi hilo.

Endelea kufuatikia Blog hii ili uweze kufahamu yale yaliyojiri kwenye uzinduzi huo wa "Mashauzi Classic".

No comments:

Post a Comment