Thursday, August 11, 2011

MWANAMUZIKI TWANGA PEPETA KINARA WA NIDHAMU BSS

HAJI RAMADHANI katika pozi

HAJI akionyesha umahiri wake wa kuimba


Madam RITHA Jaji Mkuu BSS
Mwanamuziki wa Twanga Pepeta kisima cha burudani ambae pia ni mshiriki wa "BSS Second Chance" 2011 HAJI RAMADHANI, ameibuka kinara anayeongoza kwa Nidhamu ya hali ya juu kati ya washiriki wa mashindano hayo.

Kwa mujibu wa baadhi ya Washiriki wa BSS, HAJI amekuwa akionyesha heshima na nidhamu ya hali ya juu kwa washiriki wenzake kiasi ambacho amekuwa kimbilio la washiriki wengi ndani ya Jumba hilo la BSS.


Hata hivyo Jaji Mkuu wa BSS RITHA PAULSEN ameunga mkono kauli za washiriki hao na kuongeza kuwa anafurahishwa na tabia ya  HAJI ambayo ni mfano mzuri wa kuigwa na wasanii wengine hapa nchini.


HAJI RAMADHANI ameingia kwenye shindano hilo mwaka huu baada ya kung'ara kwenye BSS 2010 na kulamba ajira kwenye bendi inayotikisa kwa burudani hapa bongo ya Twanga Pepeta.



No comments:

Post a Comment