Tuesday, August 30, 2011

AUAWA KIKATILI AKIDAIWA KUIBA KUKU

Kijana aliyefahamika kwa jina la Xavery Naseeb maarufu kama Mkemia akiwa amechomwa moto katika eneo la Viwanja vya shule ya msingi mwenge jijini Mbeya kwa tuhuma za kuiba kuku

Marehemu Xavery akiwa amelala pembeni mwa kuku aliodaiwa kuiba

Marehemu Xavery

Askari wa Jeshi la polisi wakiwa katika eneo la tukio kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya kuupeleka Hospitali ya Rufaa Mbeya.
 Kutoka kwa afrokija: Ni kosa kujichukulia sheria mkononi hata kama kuna ushahidi wa Tukio kama hilo, ni vema kutumia vyombo vya Dola kwa kuwa vyombo hivyo vipo kwa kazi hiyo. Hebu fikiria kama huyo aliyefanyiwa hicho kitendo hiki angekuwa ni ndugu yako ungejisikia vipi?? hupaswi kumtendea mwenzako jambo ambalo usingependa kutendewa.. Pia iwe fundisho kwa vijana wenye tabia hizo za wizi kwani vina madhara makubwa, na tujifunze kwa haya yaliyompata ndugu yetu Xavery.. 

Blog hii inatoa pole kwa ndugu, jamaa na Marafiki wa marehemu Xavery na mwenyezimungu aiweke mahali pema roho ya Marehemu, Ameen.

Picha: kwa Hisani ya Mbeya yetu blogspot

No comments:

Post a Comment