Tuesday, January 31, 2012

MASHAUZI CLASSIC YAACHIA SI BURE UNA MAPUNGUFU

Kundi la muziki wa Taarab linalotikisa anga ya muziki huo nchini Tanzania "Mashauzi Classic" limeachia wimbo mpya walioupa jina la "Si bure una mapungufu

Akizungumza na Eatv kupitia kipindi cha Afrobeat Mkurugenzi wa kundi hilo Isha Ramadhani a.k.a Isha Mashauzi amesema Katika wimbo huo, wamemzungumzia mtu mwenye majivuno anayejiona anajua kila kitu, asiyependa maendeleo ya wenzake, asiyependa kukosolewa na mwenye kupenda kutukuzwa siku zote lakini hastahili hayo yote.

Na haya ni baadhi ya mashairi yaliyomo kwenye wimbo huo “Tulivyokuzoea tofauti na ulivyo, tuna wasiwasi ni mwezi mchanga, mambo yako sera zako sasa hivi ni ovyo, mara karudi tena kwa waganga, si bure una mapungufu tunakuhurumia, umekuwa kama fukufuku kila shimo waingia” 

Aidha Isha amefafanua kuwa kama ilivyo kawaida ya nyimbo zake, kwenye mashairi ya wimbo huo hakumlenga mtu yeyote isipokuwa amesimama kama msanii ambae ni mwakilishi wa wale wote wanaokerwa na watu wenye tabia kama hizolakini hawana nafasi ya kuzifikisha kero zao hivyo litakayemgusa basi linamhusuuu.....

Monday, January 30, 2012

BATA LA WEEKEND @SAVANNAH LOUNGE

Baada ya mambo meengi ya mchana kutwa nikasema inabidi sasa kurefresh Mind, sehemu sahihi kwangu ilikuwa ni Savannah Lounge Quality Centre pamoja na kampan yangu kubwa  Andrew, huyu jamaa ndo rafiki yangu mkubwa na ndo huwa natoka nae mara zote
Hapo kikapigwa kitu cha Facebook nikaanza kuimba mwenyewe
Huyu jamaa cjui anawaza nn maana anaonekana yuko mbaaaliii
Jamaa nahisi anahakikisha kama hiyo ni kweli Windhoek
Muda wa kucheza ukafika, mimi na Glory a.k.a pacha maana kuna watu walituambia tunafanana ikabidi nianze kumuita pacha bt mmh cna hakika maana mwenzangu kafungasha mashaallah
Ma boy Andy nae akiyarudi
Andy na Ally
Kijah na Ally
One luv
Balaa inakuja pale unapokuwa umechoka unatamani ukapumzike halafu mwenzako ndo kwanza mzuka umepanda, matokeo yake huwa kama hivi, unaganda kwnye gari weee.... Mwisho wa siku wote tulienjoy kiukweli na Weekend ilikuwa pouwah


SIKU ZA WEEKEND HUWA NI KAZI TU KWA KWENDA MBELE


Kama nilivyoeleza hapo juu kuwa siku za Weekend zinakuwa ni siku za kazi zaidi kwa Team ya Afrobeat hivyo baada ya kutoka Dar Live tulielekea Temeke Davis Corner kwa ajili ya Interview na kiongozi wa Coast Modern Taarab Omary Tego(na hicho ndicho kiti alichokitumia Tego) kitu cha vidole vitano, Halla Five Nyalifa umeiona hiyoooo???
Hapo Omary Tego akijibu maswali niliyokuwa nikimuuliza
Mahojiano yakiendelea kikubwa hasa ambacho tulitaka kufahamu ni kuhusu Kundi lake maana inasemekana kuwa baada ya baadhi ya wanamuziki wake kuondoka, kundi hilo limeyumba sana na linaelekea kufa kabisa ambapo mwenyewe amekanusha madai hayo na kudai kuwa kundi lake bado liko fresh kwa sababu bado lina wanamuziki wengi tu ambao ni wakali na wanafanya kazi nzuri kama ilivyokuwa mwanzo
Crew ikiwajibika kama kawa Cameraman Rajab Kimanyo sambamba na Soundman Jacob
Baada ya mahojiano mazungumzo na story za hapa na pale ziliendelea, kushoto ni Producer wa Afrobeat, Mussa kondo na Omary Tego
Omary akijiachia na Mutoto muzuri
Tukaambiwa aah mbona mnaogopana jamani?? ikabidi tusogeleane kidogoo.. hhahahahahhaa ni picha tu jamani msije mkazusha mengine maana wale ndugu zetu tunawajua wenyewe.
My Producer nae akasema aah mbona mwajipendelea!!! akasogea na yeye tukajifotoaa.. Endelea kuangalia Afrobeat ili usipitwe na mambo haya mazuri jamani, only on Eatv the no. 1 Youth Channel

DAR LIVE PART II

Ukiingia tu Dar Live mbele yako unakutana na hili jengo, kama hupendi kukaa chini basi wapanda zako huko unakula upepo mwanana kabisa

Hii nayo ni moja kati ya vivutio vilivyopo Dar Live
Unapoingia tu maeneo ya mlangoni kabisa unakutana na warembo ambao hiyo unayoiona ndo kazi yao
Hapo dogo tayari ameshafanyiwa Makeup na watoto wanaenjoy wenyewe gharama yake ni buku tu(Tshs 1000)
Hii ndiyo Stage sasa na pia kuna Projector tatu kama unavyoziona
Nilikuwa na mdogo wangu wa mwisho pia, anaitwa Rahma

Hii sehemu watu wengi sana inawavutia niliona watu wengi sana hasa wadada wakipiga katika eneo hilo
Mmoja kati ya marafiki zangu wa karibu sana anaitwa Salma a.k.a Diva wa ukweliiii
Kuna mambo mengi sana ya kufurahia pande hizo za Dar Live hasa kwa watoto, michezo mbalimbali kama unavyoona kwenye picha
Kitu cha Dar Live hichoooooooo, dogo akishuka kwenye ndege na huo ndiyo mwisho wa safari yetu kutoka  Dar Live Mbagalaaaaaaa



Sunday, January 29, 2012

AFROBEAT NDANI YA DAR LIVE-MBAGALAA

Hapo ni kabla ya kuanza kipindi, nikipata maelekezo kutoka kwa Producer wangu (Mussa Kondo) na huyo dogo hapo ni mtoto wangu Harison a.k.a Obama akifuatilia mama yake anavyopewa maelekezo
Kazi ikiendelea na kama unavyowaona hao watoto nao wakitaka waonekane kwenye kipindi na hii ni moja ya Changamoto kubwa sana ambayo tunakabiliana nayo tunapokuwa kwenye Location kama hizi zenye hadhara ya watu hasa watoto.
Hapo dogo nae aking'ang'ania Mic ikabidi tumpe kidogo ili tumridhishe nasi tuweze kuendelea na kazi, maana bila hivyo hapo anaangusha kilio mpaka kazi yenyewe unaiona chungu
Hapo sasa kazi imeanza na hii sehemu ndo niliitumia kwa kufungua na kufungia kipindi
Hapo kazi ikiendelea na kama unavyoona hapo juu ni mama akipiga mzigo na chini ni dogo Herry  nae katulia akimfuatilia mother wake kwa umakini mkubwa
Hii ndiyo Crew nzima ambayo imeweza kukamilisha Show hiyo ambayo utaiona Jumamosi hii huyo mwenye Bag ni Soundman anaitwa Jacob anaefuata ni Producer Mussa Kondo na anayeonekana kidogo ni Rajab kimanyo (Cameraman) wakiwajibika.





Thursday, January 26, 2012

KUNA TOFAUTI KUBWA SANA UNAPOKUWA NA UHUSIANO WA KIMAPENZI NA WAZUNGU NA UNAPOKUWA NA UHUSIANO NA WABONGO

Mange na Devotha a.k.a wake ya wazunguu
Wakifunguka
Mange, Devotha na Super Woman Joyce Kiria
Devotha na Joyce
Kuna mambo mengi sana ambayo watu hasa wa jinsia ya kike tukiakaa pamoja huwa tunajadiliana na kila mmoja akielezea uzoefu wake katika mambo mbalimbali aliyopitia katika maisha yake hususan katika suala la mapenzi.
Leo tunaangalia suala la tofauti kati ya walio katika uhusiano wa kimapenzi na wenzetu kutoka mataifa ya ulaya almaarufu kama wazungu na wale walio na uhusiano na waafrika hasa Watanzania.

Kupitia Wanawake Live ya Joyce Kiria utawasikia wake wa wazungu ambao ni Mange Kimambi ambaye pia ni mmiliki wa Blog ya U-turn,Devotha Chuwa aliyewahi kuwa mke wa Marehemu James Dandu ambaye kwa sasa ameolewa na mzungu pia watafunguka kuhusiana na Experience yao katika mahusiano na kukubwa wakizungumzia kuhusu tofauti waliyoiona pale walipokuwa na wabongo na sasa hivi ambapo wapo na wazungu.

Kwa kukudokezea tu ni kwamba tofauti kubwa ambayo wao wameizungumzia ni kuhusu suala la tamaduni, kwa mfano sisi watanzania tuna utamaduni wa kutake Responsibilities kwa ukoo mzima let say shangazi ni mgonjwa utawajibika kumhudumia mpaka au mtoto wa shangazi hana ada ya shule pia utawajibika kumsaidia ili aende shule kitu ambacho ni tofauti kubwa na wenzetu ambao wao wanajali mke/mume na watoto tu, hivyo wanapata Challenges kubwa sana pale wanapokutana na masuala hayo ya kusaidia ndugu.

Kitu cha pili ni kuhusu maisha ya kawaida ya Familia kama mke na mume wenzetu unaambiwa mara nyingi wanafanya mambo yao pamoja, mfano wakitaka kutoka basi wanatoka pamoja, wakati wa chakula kila mmoja muda ukifika basi atakuwa mezani tofauti na sisi ukumuuliza baba ataluambia nyie kuleni tu mimi leo nitachelewa kurudi au katika suala la kutoka mama utapigiwa tu simu kuwa leo nitachelewa kurudi nitakuwa na marafiki zangu sehemu, swali ni kwamba kwa nini msiende wote na mkeo huko kwa marafiki au mna siri gani ambayo mke wako hapaswi kuifahamuuu?

Mengi sana yalizumgumzwa lakini kikubwa ambacho mimi kilinivutia ni kuhusu hiyo tofauti ya kati ya wale walio na uhusiano na hao wazungu na sisi tulio na wabongo wenzetu.. Endelea kuangalia Eatv ting'a namba moja kwa vijana ili uweze kufahamu mengi ambayo yamezungumzwa kwenye hicho kipindi.

MAUZO PIA INARUHUSIWA JAMANI

Me and Meena



Nikiachia upepo upite kidogo

Picha ina raha yake... mweh!!

Hapo tukakosa mtu wa kutufotoa tukaanza kujifotoa wenyewe
Aaah kushangaa pia imo!!!!!

TAMASHA LA TISA LA SAUTI ZA BUSARA


I AM BACK

Kwanza kabisa naomba niwatakie Kheri ya mwaka mpya 2012 wadau wote popote mlipo, naamini kuwa sijachelewa sana coz ndo kwanza bado tuko January... Kubwa zaidi naomba mniwie Radhi wale wote ambao mlitembelea Blog hii na kukuta hamna jipya kwa takribani mwezi mmoja sasa, hii ilitokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wangu, lakini kwa uwezo wa Mungu kuanzia leo tutaendelea kuhabarishana kama kawa kama dawa hivyo endelea kutembelea Blog hii bila kuchoka!!!! Ahsante na karibu sana.