Wednesday, August 3, 2011

AISHA MADINDA AVUNJA UKIMYA

AISHA MADINDA
Mnenguaji mkongwe na anaesumbua Bongo AISHA MADINDA ambae hivi karibuni aliihama Bendi yake ya siku nyingi ya African Stars International (Twanga Pepeta ) na kutimkia Bendi pinzani ya Extra Bongo amevunja ukimya baada ya kimya cha muda mrefu na kusema kuwa, tofauti na watu wanavyofikiri kuwa ameihama Bendi hiyo kwa kushawishiwa, na badala yake amesema amehama Twanga na kujiunga na Extra Bongo kwa hiyari yake kwa kuwa aliipenda bendi hiyo kwa muda mrefu.

Amesema watu wameongea vitu vingi sana ambavyo havina ukweli wowote hivyo sasa ameamua kuvunja ukimya na kuwaambia mashabiki wake wasifuate maneno yanayosemwa na baadhi ya watu wenye lengo la kuharibu jina lake badala yake wasikilize kile anachosema yeye kwa kuwa ni yeye pekee mwenye ukweli kuhusu mambo yake.
"Watu wameongea sana lakini leo nasema hivi waliyoongea yote ni ya uongo mimi ndiyo msema ukweli, sasa hivi niko fiti na najiamini kwa kila kitu pia nafanya kazi kwa uwezo wote na mashabiki wanaona ninachofanya Extra Bongo, hivyo wapenzi wangu wasisikilize maneno ya watu wanaotaka kuharibu jina langu"

No comments:

Post a Comment