Thursday, September 26, 2013

Tanzania hatarini kuvamiwa na Al shaabab

WAKATI wananchi wa Afrika Mashariki wakijawa na hofu ya mashambulio yanayopangwa kufanywa na vikundi vya ugaidi vya Al Qaeda na Al Shabab, imebainika kuna Watanzania waliopewa mafunzo ya ugaidi wanaojiandaa kufanya maovu.

Hayo yamebainika siku chache baada ya wanamgambo wa kundi la Al Shabab kufanya mashambulio katika Jengo la Biashara la Westgate mjini Nairobi na kuua watu zaidi ya 70 na kuacha mamia wengine wakiwa wamejeruhiwa.

Mkuu wa Interpol Tawi la Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Gustav Babile aliyasema hayo jana katika mahojiano maalumu na MTANZANIA.

Alikuwa akizungumzia kauli ya hivi karibuni iliyotolewa na Msemaji wa Al Shabab, Sheikh Abdulaziz Abu Muscab aliyetoa tahadhari kwamba kundi lake linapanga mashambulio mengine Tanzania na Uganda.

Babile alisema taarifa zinaonyesha vijana wa Tanzania waliojiunga na mafunzo ya ugaidi yanayotolewa na vikundi vya Al Qaeda na Al Shabab, wamefanya hivyo baada ya kushawishiwa watapata utajiri wa haraka.

Alisema hali hiyo imevifanya vyombo vya ulinzi na usalama nchini kutoipuuza kauli hiyo ya Sheikh Abdulaziz Abu Muscab.

“Tunajua wapo Watanzania wanapewa dozi za ugaidi, na sisi siyo kisiwa, watu ni hao hao… tumejipanga kuyakabili haya na kuushirikisha umma katika ulinzi,” alisema.

Babile alisema kauli ya msemaji wa kundi la Al Shabab ya kuivamia Tanzania siyo ya kupuuza na kusisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini viko tayari kukabiliana na lolote litakalotokea.

“Tumeisikia kauli yake kwenye mitandao ya jamii, imetufanya kuwa alert (macho) vya kutosha, imetuweka sawa na imetukumbusha kuwa tunaweza kuvamiwa wakati wowote.

“Hatuja-relax hata kidogo, tumejiweka sawa kwenye human resources zetu, materials resource na hata frontline officers wetu wako makini mno.

“Mfano kwenye viwanja vya ndege ambako ni muhimu, kuna mitambo inayoweza kugundua hati za kusafiria za washukiwa wa uhalifu wanaotafutwa kimataifa na tutawakamata tu.

“Lakini hata kwenye mipaka yetu yote hatuko peke yetu, tumepanua wigo wa kupata taarifa za kiintelijensia na katika kufanya kazi hii tunashirikiana na vyombo vyote vya ulinzi na usalama,” alisema.

Baada ya kufanya mashambulio mjini Nairobi Jumamosi iliyopita, Msemaji wa Al Shabab, Sheikh Abdulaziz Abu Muscab, aliripotiwa kwenye mitandao ya jamii akisema shambulio hilo lilikuwa ni la kulipiza kisasi baada ya majeshi ya Kenya kuvamia kundi hilo lenye makazi yake mjini Kismayu, Somalia.

Mitandao ya jamii pia ilimnukuu Sheikh Abu Muscab akijigamba kuwa wakati wowote mashambulio ya kikundi hicho yataelekezwa Uganda na Tanzania.

Wakati huohuo, Babile amesema Mtanzania mmoja alikamatwa Kenya akishukiwa kuwa ni mmoja magaidi waliovamia jengo la Westgate.

Bila kumtaja jina, alisema mtu huyo ni mkazi wa Arusha na alikamatwa muda mfupi baada ya kuingia Kenya akitoa Tanzania, akitumia usafiri wa mabasi ya abiria.

“Walipomkamata wakatuletea taarifa sisi, tukatafuta kwenye database zetu na information za ndani zikatuonyesha hakuwa mtu hatari, tukamuachia.

“Kilichowatia hofu na kumshuku mtu huyu ni muda alioingia Kenya na muda wa tukio lilipotokea… lakini tumeangalia taarifa zote tukagundua hakuwa na shaka,” alisema Babile.



Maombi yasababisha aibe maiti ya baba yake.

Mtu mmoja aliyeiba maiti ya baba yake kutoka makaburi ya Detroit amewekwa chini ya uangalizi jana na kuamriwa kuhudhuria tiba ya akili ama atafungwa jela.

Vincent Bright, miaka 49, alinusurika hukumu ya kifungo jela. Alipatikana na hatia Agosti ya kufukua mwili huo.Bright lazima aendelee kupatiwa tiba ya afya ya akili na kumwonesha ofisa wake uangalizi kwamba anatumia dawa, Jaji wa Mahakama ya Wayne County James Chylinski

"Kama hufanyi hivyo, nitalazimika kukufunga jela," alisema jaji huyo. Mnamo Januari, mwili wa Clarence Bright mwenye umri wa miaka 93 ulitoweka kutoka kwenye makaburi ya Gethsemane, muda mfupi baada ya msiba wake lakini kabla jeneza halijafukiwa. Wanafamilia waliwaongoza polisi kuelekea kwenye mwili huo katika jokofu nyumbani kwa Vincent Bright huko Detroit.
Bright alikamatwa pale polisi walipomkamata ndani ya gari akiwa na jeneza tupu nyuma ya gari hilo.

Polisi wakati huo walisema Bright alikuwa mfuasi wa dini na alikuwa na matumaini baba yake atafufuka na kuishi tena kutokana na maombi.

Aligundulika hakuwa na akili timamu kuweza kukabili mashitaka, lakini afya yake ya kiakili ikaimarika baada ya wiki kadhaa za matibabu na uchunguzi kwenye hospitali za serikali.
"Alipitia kipindi kibaya, misongo mingi ya mawazo. ...Anaendelea vema. Yuko kwenye matibabu," wakili anayemtetea Gerald Karafa alisema nje ya mahakama, akizungumzia vifo vya wazazi wa Bright.

Alisema ilikuwa 'ushahidi binafsi' ambao afya ya kiakili ya Bright ilitawala katika wizi huo.

Bright alikataa kuzungumzia suala hilo nje ya mahakama. Baada ya kukamatwa kwake, alitumikia siku 225 jela au mahabusu katika hospitali za serikali.

Dhamana yake ilipangwa kuwa Dola za Marekani 75,000 hivyo mchanganuo wa afya ya akili unaweza kukamilika, ambao utaweka kumkuta akiwa tayari kukabili mashitaka.

Endapo atapatikana na hatia ya kufukua mwili, Vincent Bright anaweza kukabiliwa na kifungo cha hadi miaka 10 jela, kama hangekuwa amewekwa chini ya uangalizi kwa matatizo ya akili.

Wednesday, September 25, 2013

50 CENT aanza kufulia

Miaka mitatu kama sio miwili iliyopita 50 Cent alikuwa akishikilia nafasi za juu kabisa huku akinyemelea nyao za Jay Z na P Diddy.

Kwenye mtiririko ambao unatolewa na Forbes, 5o Cent ameshika nafasi ya 19 kwenye list ya wasanii wa hip hop wanaoongoza kuwa na hela nyingi.

Nafasi ya kwanza inashikiliwa na P Diddy wakati Jay Z akishilia nafasi ya pili, Dr Dre nafasi ya tatu, Nick Minaj nafasi ya nne wakati boss wake Birdman anashika nafasi ya tano, sita ni Kanye West, Saba ni Lil Wayne.

50 Cent amepitwa na wasinii ambao wamechipukia kwenye game kama Kendrick Lamar na Macklemore.

Bongo Movie inashikiliwa naye JB na Wema

Baada ya utafiti uliyofanywa umebahatika kuwapata wasanii wa Bongo muvi wanaongoza kwa kupendwa na mashabiki hapa Tanzania kutokana na kazi zao za Filamu.

JB ni mmoja wa wasanii kwa upande kiume anaeongoza kwa kupendwa na mashabiki wake kutokana na uwezo wake katika uigizaji wa muvi.

Funga kazi kwa mwanadada Wema Sepetu ndiyo msanii wa pekee wa Bongo muvi anaeongoza kwa kupendwa na mashabiki lukuki wa mjini na vijijini, licha kuwa na skendo zake kibao ila Watanzania wana-show love kwake.

Tuesday, September 24, 2013

Nje kwa mechi 3, yamemkuta Baloteli

MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amefungiwa mechi tatu kufuata kumvaa refa katika mchezo ambao timu yake, AC Milan ilichapwa mabao 2-1 na Napoli Jumapili.

Balotelli, ambaye alikosa na kufunga bao zuri la kufutia machozi kwa timu yake, alionyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya mechi kwa kumvaa refa.

Mshambuliaji huyo wa Italia sasa atakosa mechi tatu zijazo kwa kosa hilo.
Balotelli, ambaye alifunga penalti zake zote 21 za awali katika mechi rasmi, mkwaju wa Jumapili uliokolewa na kipa wa Napoli, Pepe

Kadi hiyo nyekundu ya utata, inamaanisha Super Mario atakosa mechi na Bologna, Sampdoria na Juventus, ingawa Milan inaweza kukatia rufaa adhabu hiyo. Chanzo: binzubeiry

Anamlalamikia mkewe, hebu mpe ushauri

Habari,
Mimi nimeoa na ndoa yangu ina miaka 7 sasa na tuna watoto wa 2. Nlimuoa mwanamke aliyekuwa kamaliza degree ambaye alikuwa home tu at the time anatafuta ajira. Toka nimuoe hajawahi kufanya kazi yoyote ile yaani Goalkeeper mpaka leo na kutafuta kazi alisha acha. Mpaka leo hii mke wangu hajabadilika. Namlipa mshahara mwisho wa mwezi ambao ni sawa na kama 10k per day yaani (300k).

Kila ninapojaribu kumtafutia kazi anafanya kidogo tu anaacha. Huwezi amini hata umlazimishe vipi ajishughulishe mzito ile mbaya. Mi ni mfanyabiashara(Magari Makubwa) nimemuanzishia vimiradi through the years vyote kala mtaji. Kuna kipindi alijaribu kusoma masters ya bussiness administration nkamlipia ada, nunua vitabu vyote alafu yeye akaamua kuacha baada ya mwezi tu Eti kuamka alfajiri hawezi. Nkaja nkamuomba basi asome chuo ambacho atakuwa anaingia mchana nacho alishindwa.

Tatizo rafiki yake mkubwa ni mama yangu mzazi hivo kuna kipindi nlikata mshahara wake ili kumlazimisha afanye kazi akakimbilia kulia manyanyaso nikalazimishwa hela yake isiguswe na wazazi wangu. Nkienda kazini namuacha nyumbani na home kwenyewe hafanyi chochote anaita tu housegirl. Yaani yupo yupo tu siku hadi siku. Nifanyaje ili hata nikianguka leo au kesho awe ni mama atakayeweza kusomesha watoto.

Alafu matumizi yake ya hela mabaya yaani hela yake mwenyewe ukimpa mwanzo wa mwezi kwenye tarehe 1 hiv basi ikifika tarehe 8 ujue alikuwa anaumwa. Ila ni hela yake na hainunui hata nguo ya mtoto hivyo hainihusu. Nifanyaje ajishughulishe?

Thursday, September 12, 2013

Rado asema Bongo movie wanasubiri ufariki ndio wajitokeze

MSANII wa filamu na mtayarishaji pia wa filamu Bongo Simon Mwakipagata ‘Rado’ amelishutumu na kulilaumu kundi la filamu la Bongo Movie Unity kwa kukosa upendo na kushindwa kusaidia katika matatizo, Rado aliyasema hayo kufuatia hivi karibuni kupata ajali ya gari na kujikuta akijiuguza pekee yake bila kupata faraja kutoka kundi hilo wakati yeye ni katibu wa kundi hilo.

“Siku zote mimi upenda kuwa mkweli hata kama mwingine atachukia hivi karibuni wakati narudi kutoka Location nilipata ajali na kuumia sehemu ya kifua ilikuwa ni ajali mbaya namshukru Mungu kuniponya lakini rafiki zangu wa Bongo movie hakuna hata mmoja aliyejitokeza kunijulia hali wakati walikuwa na taarifa, lakini tu hao hao wangesikia nimekufa wangekuwa wa kwanza kuunda kamati ya mazishi,”anasema Rado.

Msanii huyo nyota anadai kuwa tukio hilo ni la pili kwake kupata ajali lakini mara zote hizo amekuwa jirani na wasanii ambao alikuwa akiigiza nao katika kundi la Jumba la Dhahabu ambao ni Niva, Baga, Wema Sepetu na wasanii wengine ambao kila awapo na tatizo uwa mbele katika kumsaidia na kumfariji katika ugonjwa lakini si kundi ambalo yeye ni kiongozi pia kama katibu

Lulu apokea vitisho kisa kufunika uzinduzi wa Foolish Age

KUFANIKIWA kwa uzinduzi wa filamu ya Foolish Age ya msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, kumemfanya kinda huyo anayetingisha katika tasnia hiyo kupata vitisho kutoka kwa mastaa wenzake.

Habari kutoka vyanzo mbalimbali ndani ya fani hiyo zinasema katika uzinduzi huo, msanii huyo alifunika na kuonyesha dalili zote za kuwazima mastaa wenzake ambao kwa muda mrefu wamekuwa juu.

Taarifa hizo zinasema staa huyo wa Bongo Muvi anatafutwa kwa kila namna, usiku na mchana ili kuhakikisha nyota yake inafifia.

Madai hayo yamekuja zaidi baada ya uzinduzi huo kufana kwani pamoja na mambo mengine, hata jinsi alivyokuwa amejipanga kwa walinzi wake, lilikuwa ni jambo kubwa ambalo linafanana na inavyotokea katika shughuli za mastaa mbalimbali wa majuu.


Mwandishi: Mambo vipi Lulu?

Lulu: Salama tuu za kwako?

Mwandishi: Salama, vipi umesikia vitisho vyako kutoka kwa mastaa wa Bongo Muvi wanaodai kuwa umekuja kuwapita kisanii?

Lulu: Hapana sijasiki, lakini kama wanatoa vitisho lazima wakubaliane na ukweli kwamba lazima awepo wa kwanza na wa mwisho, wakaze buti.

Mwandishi: Umejipangaje kukabiliana na hilo?

Lulu: Najipanga kufanya kazi mimi kama mimi na wao wafanye kama wao, wakijifanya kuwa kama mimi haiwezi kuwa hivyo, mbona mastaa wa ughaibuni kama Beyonce na Rihanna wako tofauti? Lazima awepo wa kwanza mpaka wa 10 hatuwezi kulingana.

Mwandishi: Kuna lolote la kuongeza juu ya hilo ama wito kwa wasanii?

Lulu: Wajipange kufanya kazi kwa nguvu zote, wasifanye kama mimi wafanye kama wao,

Mwandishi: Asante Lulu nakutakia siku njema
Lulu: Ok, sawa kazi njema

Wednesday, September 11, 2013

Baby Madaha ala Bingo la mkataba mpya

Mwanadada anayefanya vizuri sana kwenye muziki na filamu,baby Madaha amelamba bingo ya uhakika na kampuni ya Candy n’ Candy Records Label ya jijini Nairobi iliyomsainisha mkataba msanii mwingine wa Tanzania Mr.Nice hivi karibuni.

Akizungumza kwa simu na bongomovies leo meneja wa msanii huyo  Joe Kariuki amesema kuwa  pamoja na msanii huyo kupewa mkataba huo wa million hamsini (50) pia wamempa mwanadada huyo gari ya kutembelea ya kisasa aina ya AUDI TT (pichani) na nyumba  kali mitaa kijitonyama jijini  Dar es salaam.

Pamoja na hayo pedeshee huyo wa Mr.Nice ambaye ndio mmiliki wa studio hiyo amesema wanataka kumuhamishia msanii huyo jijini Nairobi nchini Kenya kwa kipindi cha mwaka mmoja ili afanye nao kazi huko kwani wamegundua kuwa anakubalika sana nchini humo na wapenzi wa muziki.

Baby madaha ambaye  anatarajia kutua nchini leo akitoka Nairobi pamoja na meneja wake kwa ajili ya kuachia video ya  wimbo wake wa kwanza aliofanya na Label hiyo uitwao (Summer Holiday) ambao umefanywa huko huko jijini Naironi

'Niko single na sihitaji mpenzi sasa' Baby Madaha

Baby Madaha ambaye hivi karibuni amesaini mkataba mnono na kampuni ya Candy n’ Candy Records Label ya jijini Nairobi nchini Kenya tumeweza kugundua mambo ambavyo mashabiki wa mwanadada huyu watakuwa hawajui kumhusu yeye.

Katika interview hii baby ametaja mambo matano ambayo anasema mashabiki wake wanahitaji kuyafahamu kumhusu yeye. Mambo hayo ni haya yafuatayo

1. I’m single and I’m not searching (Nipo single na sitafuti mpenzi)

Mwanadada huyu amesema kuwa kwa sasa yupo single na haitaji kuwa na uhusiano na mwanaume yoyote kwa  kwani mume wake ni “kusaka mahela”

2. Anasoma degree ya sanaa kwenye sayansi ya siasa na historia (B.A- Political science and History) kwenye chuo kikuu huria jijini Dar es Salaam

3. Mama yake mzazi ndio rafiki yake mkubwa maishani

4. Ni mpenzi wa soka na ni mshabiki wa Chelsea na anavutiwa na  Kevin-Prince Boateng wa club Schalke 04 ambaye ndiye alisababisha akanyoa nywele staili aliyonayo baby madaha kwa sasa.

Jokate akanusha kumegana na Lucci


Mwanamitindo ambaye pia kw saa amejikita katika tasnia ya muziki akijulikana kama Jokate Mwegelo au maarufu kama Kidoti ambae kwa sasa anatamba zaidi na ile ngoma ambayo amefanya na Producer Lucci inayoitwa Kaka Dada.

Kutoka mtandao wa instagram kupitia ukurasa wa Kidoti ameonekana kufunguka juu ya mahusiano yake ya producer huyo.

 Maana tangu waachie video ya ngoma hiyo kumekuwa na story nyingi tofauti katika mitandao tofauti ikidai kuwa wawili hao ni wapenzi.

Cheki huu ndio ujumbe alioandika msanii Jokate masaa machache kutoka Instagram...

Soma hapa..

Tuesday, September 10, 2013

Msanii Angel aolewa kimya kimya



Msanii wa filamu nchini anayekuja kwa kasi katika anga za muziki na filamu ajulikanae kwa jina la Sabby Angle ambae makazi yake ni nchini uingereza amefunga ndoa ya siri na mchumba wake wa siku nyingi

Wakizungumza  kwa nyakati tofauti baadhi ya wasanii bao hawakutaka kuandikwa majina yao walimuambia muandishi wa habari hizi kuwa wamesikitishwa na msanii mwenzao kuwa mchoyo kwa kufanya harusi yake kimya kimya bila kuwapa taarifa huku wakieleza kuwa hizo ni dalili za uchoyo.

Msanii huyo amefunga ndowa iliyohudhuriwa na masta wachache sana na ameolewa na jamaa aliyejulikana kwa jina la Dr. Mohamed raiya wa uingereza pia Kama utakuwa hujamjua msanii huyu amecheza katika movie ya ray inayojulikana kwa jina la Hard Price pia katika filamu ya Dk Cheni inaitwa Nimekubali Kuolewa Baada ya habari hizi kufika katika dawati letu  kwa siri tulimtafuta Sabby Angle kwa simu kutaka kujua ambapo alianza kwa salamu na kusema

 ...Salaam.yeah nimeshaolewa.. Na Dr.Mohamed Osman. Kutoka england. Harusi ilikuwa tareh 1. September na kwasasa Tuko hapa..ila nina mpango wa kwenda UK baada mda mchache...

Muandishi wetu alimuuliza pia kutaka kujua idadi ya filamu alizocheza hadi sasa ambapo msanii huyo mkali awapo mbele ya camera alizitaja kwa kusema kwa sasa nimeshacheza
Hard Price. ya kampuni ya Rj chini ya ray na johari.. Na Coincidence.. Na Nimekubali kuolewa...ya Mahsen Awadh Dk cheni

Na  hivi karibuni naanza kucheza kwenye filamu ya Hunters ya Bond ambaye alichukua Director bora wa filamu ZFF

Dully Syakes, amfananisha Diamond na Kanumba

Baada ya kuachia video yake mpya iliyofanywa kwa gharama ya  takribani milioni arobaini na tano za kitanzania, mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz amefananishwa na marehemu Steven kanumba kwa jinsi anavyothubutu kufanya mambo makubwa kukuza Sanaa na kipaji chake tofauti na wasanii wengine wenye majina makubwa nchini.

Hayo yameongelewa na Msanii dully sykes katika mahojiano yake hii leo... Katika interview hiyo Dully amemuelezea marehemu kanumba kama ni mtu aliyethubutu kutumia nguvu, hali na mali, kwa ajili tuu ta kukuza jina lake kitu ambacho ni nadra sana kwa wasanii hasa wa Tanzania.

“Kanumba alikuwa ana uwezo wa hata kuchukua nauli yake ya kwenda sehemu kama Ghana kwenye tamasha la movie lakini ilimradi kujitengenezea status yake. Kwahiyo Diamond ni mtu ambaye tayari ameshajitolea kwaajili ya kuutetea muziki wetu.” Alisema Dully sykes

Lulu na Ray wawa mabalozi wa Tamsha la filamu (DFF)

Waigizaji Elizabeth Michael (LULU) na Vicenti Kigosi (Ray) wamechaguliwa kuwa mabalozi wa wasanii wenzao katika tamasha la filamu la Dar filamu Festival litakalofanyika kuanzia tarehe 24 – 26. Katika press Release iliyotolewa na kampuni inayoandaa tamasha hilo imesema kuwa pamoja na mambo mengi, tamasha hilolitatoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa Filamu Tanzania.



PRESS RELEASE YENYEWE HII HAPA!

 Kampuni ya Haak Neel Production kwa kushirikiana na mtandao wa habari za filamu wa filamucentral inapenda kutambulisha kwenu Tamasha la filamu linaloitwa Dar Filamu Festival (DFF) 2013 litalofanyika katika uwanja wa CoICT- UDSM- Posta Kijitonyama, kuanzia tarehe 24- hadi 26, September,2013 Tamasha litaambatana utoaji wa Semina kwa wadau wa filamu, kuonesha filamu za kitanzania kwa watu wote bure kwa siku tatu.Kutakua na filamu nne kwa siku kuanzia saa kumi na mbili jioni mpaka saa tano usiku.



Tamasha hilo limelenga kutoa hamasa kwa watanzania kuziona filamu za kitanzania na zile zinazotumia Lugha ya Kiswahili pekee ili kutoa fursa ya ajili kwa vijana na jamii husika kwa ujumla, filamu zitakazoonyeshwa ni zile zinazotengenezwa na hapa nchini katika kutangaza Lugha yetu nzuri ya Kiswahili kupitia kazi zao ikiwa kampeni ya filamucentral kuitangaza lugha hiyo na kuwa ni bidhaa muhimu Ulimwenguni.

Kwa tamasha hili la awali tutaonyesha filamu za hapa Tanzania pekee ikiwa ni utambulisho wa Dar Filamu Festival kwa mara ya kwanza kwenu wanahabari, miaka ijayo Tamasha litahakikisha linashirikisha filamu kutoka sehemu mbalimbali zinazotumia Lugha ya Kiswahili kutoka popote Ulimwenguni.

Akiongea na Waandishi wa Habari mratibu wa Tamasha hilo Staford Kihore pia amesema kuwa katika kuzingatia maendeleo ya tasnia ya filamu siku tatu hizo kila siku imepewa jina kwa filamu zitakazoonyeshwa Tarehe 24th September, 2013 siku ya Jumanne ambayo ndio siku ya ufunguzi utakuwa ni usiku wa Bongo Movie Classics, 25th September, 2013 ni usiku wa Quality Nights.

Na ile siku ya mwisho tarehe 26th September, 2013 itakuwa ni Stars Nights siku ambayo kutakuwa na wasanii wetu mbalimbali ambao wanajenga soko hilo la Bongo movie filamu, Tamasha hili linapambwa na wasanii wote wakiwakilishwa na wasanii wenzao wawili ambao ni Vincent Kigosi ‘Ray’ kama Official Producer and Director for DFF 2013 na Elizabeth Michael ‘Lulu’ kama Official Actress for DFF 2013.

Pia tamasha litaambatana na utoaji wa semina kwa wadau wa filamu kwa asubuhi ambapo madarasa yataendeshwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sanaa tarehe 24 September, 2013 masomo ya Uandishi wa Muswada, Uigizaji na Uongozaji wa filamu yatafundishwa kwa washiriki, 25th September 2013 Siku nzima Makapuni ya Utengenezaji filamu yataonyesha na kutangaza kazi zao kwa wadau mbaliambali.

Tarehe 26th September 2013 ni siku muhimu sana kwani Taasisi kama vile TRA, Bodi ya Ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza, Wasambazaji wa filamu na taasisi nyingine watakutana katika jukwaa la majadiliano kuhusu mustakabali wa tasnia ya filamu, pia filamu kadhaa zitaonyeshwa na kujadiliwa na wadau watakaokuwepo matukio yote ya asubuhi yatafanyika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Idara ya Sanaa.

Pia tunatoa shukrani kwa taasisi za Serikali kutuunga mkono katika ufanikishaji wa tamasha hilli la Dar Filamu Festival (DFF) 2013, taasisi kama Bodi ya Filamu na ukaguzi wa michezo ya kuigiza Tanzania, Fine Perfoming Art – Udsm, Tanzania Film Federation (TAFF), MFDI, Swahiliwood na makapuni ya usambazaji wa filamu Steps Entertainment Ltd, Leo Media na kampuni mpya ya usambazaji ya Proin Promotion ambayo imeanza hivi karibuni na kuonyesha dhamira ya kusaidia tasnia ya filamu, pia leo tunazindua mtandao wa www.dff.or.tz

Kwa kutambua mchango wako kama mwanahabari tunaamini utaungana nasi katika kuhakikisha DFF inakuwa ni chachu ya maendeleo ya tasnia ya filamu Tanzania, huku tukisema kuwa Dar Filamu Festival2013 kwa kauli mbiuya ‘Ubora wa Filamu Zetu’ ikiwa ni njia ya kuwakutanisha wadau wote kwa pamoja na kuwa jukwaa linalojenga tasnia ya filamu inayokua kila siku. Pia tunaomba ushiriki wako katika kufanikisha hili.



Imetolewa na Mratibu wa Tamasha la DFF 2013 Staford Kihore.

Sheikh abaka mtoto wa miaka 8

KIONGOZI wa msikiti wa Masjid Maftah ulioko Misufini katika manispaa ya Morogoro, Alhaj Abdul Wazir, maarufu kama Sheikh Koba, anashikiliwa kwa mahojiano mkoani hapa kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka nane, mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Sabasaba.

Taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, zilisema mtuhumiwa huyo, anadaiwa kutenda tukio hilo chumbani kwake, Septemba tatu, majira ya saa mbili usiku, huko Mbuyuni katika manispaa ya Morogoro.

Mashuhuda wa tukio hilo wakizungumzia mazingira ya tukio hilo, walidai kuwa Alhaj Koba, amekuwa akiishi nyumba tofauti na mkewe na kwamba siku ya tukio mke wake alimtuma mtoto wa nduguye kupeleka chakula kwa mumewe, lakini alichelewa kurudi, hivyo kuamua kumfuatilia kujua kulikoni.

“Alipofika kwenye nyumba anayoishi mumewe, aligonga na kumuulizia binti huyo, lakini alielezwa kuwa alishaondoka eneo hilo, lakini mtoto alijitokeza na kudai alikuwa bado ndani ya nyumba hiyo, na alipohojiwa kuhusiana na uchelewaji wake, alikiri alikuwa amebakwa hivyo tukio hilo kuripotiwa polisi,” kilieleza chanzo chetu cha habari.

Polisi walithibitisha kupokea taarifa za tukio hilo, na kwamba uchunguzi zaidi bado unaendelea ili kumfikisha mtuhumiwa mahakamani.

Monday, September 9, 2013

JK uso kwa uso na CHADEMA jijini Mwanza

RAIS Jakaya Kikwete jana alipata wakati mgumu, baada ya kukutana na nguvu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jijini Mwanza katika ziara yake, huku Waziri wake wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, naye akijikuta akizomewa mbele yake.

Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje, alivunja mwiko baada ya kujiunga katika msafara huo wa raia akiwa na gari lenye alama za Movement for Change (M4C) lililokuwa limefungwa bendera mbili za CHADEMA.

Hata hivyo maofisa usalama walipata wakati mgumu kulizuia gari hilo lisiwepo katika msafara huo, jambo lililozua tafrani kidogo katika uwanja wa Furahisha ambapo Kikwete alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara.

Awali wakati wa uzinduzi wa wodi ya wazazi iliyoko eneo la Butimba, Rais alilazimika kumpa Wenje nafasi ya kuwasalimia wananchi baada ya Mkuu wa Mkoa, Evarist Ndikilo, kutaka kufanya hila ya kumnyima haki hiyo kama mbunge wa jimbo husika.

Baada ya viongozi wote kutambulishwa bila Wenje kutajwa, wananchi walianza kupaza sauti wakitaka mbunge wao naye atambulishwe.

Wenje baada ya kusimama alimshukuru Rais Kikwete kwa kumpa nafasi hiyo lakini akamwomba amvumilie kidogo atoe salamu maalumu ya wana Mwanza.

Kama kawaida ya CHADEMA kwenye salamu yao, Wenje aliwaomba wananchi wakunje ngumi kisha akawasalimu kwa kibwagizo cha peoples… nao wakamwitikia power!

Akiwa katika viwanja vya Furahisha ambapo Rais Kikwete alichelewa kuanza mkutano wake, Wenje alifika hapo na kushangiliwa kwa nguvu na wananchi huku polisi wakiwazuia bila mafanikio.

Ilipofika saa 12 jioni kabla Rais hajaingia uwanjani, wananchi hao walimtaka Wenje awahutubie huku wakidai bendera ya taifa ishushwe kwani muda wake ulikuwa umefika.

Kikwete aliingia uwanjani hapo saa 12:10 akiongozana na viongozi mbalimbali wa chama na serikali lakini wananchi hawakuonyesha kumshangilia badala yake walikuwa wakimwonyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na CHADEMA wakiimba ‘peoples…power’.

Katika hatua ya kushangaza wananchi hao walimshangilia kwa nguvu mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia, aliyekuwa ameongozana na Rais huku wakiwazomea Meya wa Manispaa ya Ilemela, Henry Matata, ambaye hakufika kabisa mkutanoni hapo.

Matata alionekana mapema wakati Rais Kikwete akisomewa taarifa ya maendeleo makao makuu ya wilaya hiyo lakini hakufika uwanjani kabisa katika viti vya mbele alionekana naibu wake, Swila Dede.

Baadhi ya wananchi hao walisikika wakisema chini kwa chini kuwa Matata ni mwizi hawataki kumsikia lakini shangwe na nderemo zikajiri pale walipotambulishwa Wenje na Kiwia.

Rais Kikwete akiwa wilaya ya Ilemela, wananchi wengi waliokuwa wamesimama njiani walimwonyesha vidole viwili ikiwa ni alama CHADEMA.

Hata hivyo, hali hiyo ilionekana kumkera kiongozi huyo wa nchi pamoja na maofisa wa usalama, ambapo wana usalama wakiwemo polisi walionekana wakiwatisha na kuwazuia wananchi kunyoosha vidole viwili.

Magufuli azomewa

Waziri wa Ujenzi, Dk. Magufuli, alikumbana na jinamizi la kuzomewa mbele ya Rais baada ya kusimama jukwaani na kutaja jina la Matata, ambapo wananchi wengi walimzomea kwa miluzi huku wakimnyooshea vidole viwili.

Adha Magufuli alizomewa pia aliposema wabunge wa Ilemela na Nyamagana jijini hapa ni wana CHADEMA lakini ndani ya roho zao ni wana CCM.

Pia aliendelea kuzomewa aliposema kuwa iwapo Rais angehitaji kupokea kadi za CHADEMA zilizorudishwa angepokea nyingi.

“Mheshimiwa Rais, nampongeza Meya Matata (akazomewa), lakini pia wabunge wa Ilemela na Nyamagana wanachapa kazi vizuri, nje CHADEMA lakini ndani wao CCM (akazomewa).”

Akizungumza katika mkutano huo, Rais Kikwete alimpongeza mbunge wa Nyamagana kwa uchapakazi mzuri hasa kusimamia sekta ya elimu na kwamba wabunge wa namna hiyo wanastahili kuigwa.

Hata hivyo, alisema serikali yake imejipanga vizuri kuhakikisha usafiri wa reli, ndege, majini na barabara za lami vinaboreshwa maradufu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

“Serikali yangu imeweka nguvu kubwa katika kuboresha sekta ya uchukuzi, ujenzi na nyinginezo. Hii ni kutaka kuwaletea wananchi wetu maendeleo ya kisekta,” alisema.

Baadhi ya mawaziri walioongozana na Rais mbali na Magufuli ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Kitwanga, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, Naibu Waziri wa Ujenzi na Dk. Charles Tizeba.

Sunday, September 8, 2013

Ajifungua mtoto chooni, kisha amuua

Mwanamke mmoja anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu, amefanya kitendo cha kinyama baada ya kujifungua msalani na kukiua kichanga chake. Tukio hilo limetokea hivi karibuni maeneo ya Mazizini, Ukonga Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam baada ya mwanamke huyo ambaye jina lake halikupatikana kukitumbukiza kichanga hicho chooni. 

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mwanamke huyo ni mkazi wa Ukonga Moshi Bar alidaiwa kunywa dawa kwa ajili ya kuutoa ujauzito aliokuwa nao wa miezi minane  na baada ya kuona hali imebadilika alitoka nyumbani kwake Moshi Bar na kukimbilia Ukonga Mazizini kwa ajili ya kutaka msaada kwa mama yake mdogo.

Baada ya kufika kwa mama yake mdogo aliomba maji kwa ajili ya kwenda chooni, hata hivyo alizunguka nyuma ya choo kwa ajili ya kujipa msaada wa siri lakini hali ilivyokuwa mbaya zaidi, aliamua kuingia ndani ya choo hicho na kujifungua kichanga hicho na kukidumbukiza ndani  ya shimo la choo.

 Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa walimuona  mwanamke huyo akibebwa kwenda ndani kwa mama yake mdogo ili aweze kupatiwa msaada zaidi lakini hali ilizidi kuwa mbaya kwa kuanza kuvimba mwili  kutokana na kutokwa na damu nyingi.

Waandishi wetu walifanikiwa  kuzungumza na mama mdogo wa mwanamke huyo ambaye alijitambulisha kwa jina la mama Athony alikiri binti huyo kukumbwa na mkasa huo wakati yeye akiwa kwenye shughuli zake.

“Kweli nafahamu, alikuwa ni mjamzito na alifika nyumbani kwangu saa tano asubuhi, alichokifanya hapa si kitu cha bahati mbaya ni makusudi,” alisema mama huyo.

Mama Antony alisema kuwa  wakati anarudi  nyumbani aliukuta umati wa watu na alipoingia ndani ndipo alipopewa habari za tukio hilo.

Alipotakiwa kutaja jina la binti huyo,  mama huyo alianza kuangua kilio  na kuwafanya waandishi wetu washindwe kuendelea na mahojiano naye.

Mwakilishi wa mjumbe na shina namba 34 Ukonga Mazizini, Bi Mtende alisema kuwa tukio hilo limewashangaza kutokana na mwanamke  huyo kwenda kutupa kichanga chooni kwa makusudi.
Bi Mtende alisema kwanza mwanamke huyo siyo mkazi wa maeneo hayo, hivyo hakuna aliyeweza kumjua kwa jina.

Kikosi cha zimamoto na uokoaji kilifika katika eneo hilo majira ya saa saba mchana kwa ajili ya kutimiza wajibu wao Kikosi hicho kikiwa kimesheheni zana za uokoaji kilikuta  kichanga hicho kikielea chooni na kwa kutumia mbinu zao za uokoaji na walifanikiwa kukitoa kichanga hicho kikiwa kikiwa maiti.  
 
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, ACP Marietha Minangi alikiri kutokea kwa tukio hilo ambalo yeye aliliita ni la kikatili  na mwanamke huyo amepelekwa katika Hospitali ya Amana kwa matibabu na mwili wa kichanga hicho kimepelekwa  Hospitali ya Taifa ya  Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

Waandishi wetu walifika katika Hospitali ya Amana kwa ajili ya kupata mahojiano na mama huyo Jumanne iliyopita, hata hivyo.

Friday, September 6, 2013

Mme amwambia mke wake ajiuze wapate hela ya kuishi

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, hivi karibuni mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Aisha (26), mkazi wa Tabata, Dar es Salaam alinaswa akifanya ukahaba na kudai kwamba ana ruhusa kutoka kwa mumewe ambaye hakumtaja jina.

Tukio hilo la aibu lilitokea Afrika Sana, Sinza jijini Dar ambako Aisha alisema ndiko anakofanyia biashara yake hiyo licha ya kuishi na mumewe mbali.

Mwanamke huyo ambaye hakuweka wazi kama ana watoto au la, alisema hayo kufuatia kuzuka kwa varangati la nguvu baada ya wanahabari  kumkuta yeye na mwanaume kwenye jumba moja bovu lililopo mbele kidogo ya Kituo cha Afya cha Kijitonyama, jijini Dar.

Baada ya kumulikwa na mwanga wa kamera na kubaini wameingiliwa , ndipo mwanamke huyo alikurupuka kwa hamaki na kusema:

“Pigeni hizo picha mnadhani nani ana wasiwasi. Kwa taarifa yenu mimi nina mume na mume wangu ndiye aliyeniruhusu nijiuze ili tupate pesa ya kula.


“Sasa nyinyi kama mnadhani mume wangu akiona picha zangu ataniacha mmenoa. Mume wangu yeye anajua niko wapi saa hizi, hata nikichelewa kuja huku usiku yeye ndiye hunihimiza ili nije kupata pesa.”


Mwanamke huyo aliyatoa maelezo hayo kwa ujasiri mkubwa na bila kujali kwamba anapigwa picha huku akiwa ameshikilia upande wa khanga.

Baadhi ya majirani waliposikia mkwara wa mwanamke huyo walitoka kushuhudia lakini walipokutana na mwanga mkali wa kamera   walirudi majumbani mwao na kujifungia milango huku wakidai hayawahusu .

Thursday, September 5, 2013

Daktari feki akamatwa hospitali ya KCMC, moshi



HALI ya wasiwasi imetanda kwa baadhi ya wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya mjini Moshi baada ya uongozi wa hospitali hiyo kumkamata mtu mmoja anayedaiwa kujifanya ni daktari wa watoto akiwa kwenye wodi ya upasuaji.

 Daktari huyo feki aliyefahamika kwa jina la , Alex Sumni Massawe alikamatwa jana majira ya saa 5 asubuhi na kuwekwa chini ya ulinzi mkali wa makachero wa Jeshi la Polisi waliokuwa wamevalia nguo za kiraia baada ya kukutana na mmoja wa wagonjwa ambaye alimuahidi kumfanyia mwanae wa kiume upasuaji wa ngozi.

 Kabla ya kukamatwa kwa Alex, mama mzazi wa kijana aliyekuwa akitakiwa kufanyiwa upasuaji, Pamvelina Shirima alikutana na daktari huyo katika baa moja maarufu mjini hapa iliyopo eneo la Dar Street (jina limehifadhiwa) na kumtoza sh.200,000 akidai zitatumika kuharakisha mwanae afanyiwe vipimo vya upasuaji.

Alex anadaiwa alitaka kumfanyia upasuaji kijana, Makasi Tipesa, mkazi wa Manispaa ya Moshi ambaye amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi kwa muda mrefu sasa.

 Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya KCMC, Bw. Gabriel Chisseo alisema daktari huyo aliwekewa mtego na uongozi wa hospitali ya KCMC kutokana na baadhi ya wagonjwa kuripoti kutapeliwa na mmoja wa madaktari ambaye amekuwa akijinasibu kwamba anafanya huduma hiyo kutokana na wito alionao katika fani hiyo.

 “Leo asubuhi(jana) mteja wetu ambaye amekuwa akitibiwa hapa alitapeliwa na huyu Alex , tulimkamata akiwa wodi ya upasuaji baada ya kupokea kiasi cha sh.200,000 kutoka kwa Pamvelina Shirima ambaye alimleta mwanae afanyiwe upasuaji wa ngozi”, alisema Chisseo.

Uongozi wa Hospitali ya KCMC umethibitisha kwamba mtu huyo aliyekamatwa ndani ya Hospitali hiyo, si mwajiriwa wao na wala hakukutwa na sare wala kitambulisho kinachomtambulisha kitengo chake cha kazi.

 Hivi karibu kumeibuka matukio ya watu kadhaa kujivika kuwa na taaluma mbalimbali ambazo si za kweli huku jeshi la polisi likifanikiwa kuwakamata wengine wakijifanya kuwa ni maofisa wa jeshi hilo ,wengine usalama wa taifa huku wengine wakijifanya asakri wa kikosi cha usalama barabarani.

Denti darasa la 2 abakwa na wanafunzi wenzake

Matukio ya uvunjifu wa maadili kwenye shule mbalimbali hapa nchini yameendelea kushamiri baada ya wanafunzi wanne wa Shule ya Msingi Lulanzi wilayani Kibaha mkoani Pwani kutuhumiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili na kumsababishia maumivu yaliyopelekea kulazwa Hospitali ya Tumbi kwa matibabu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana babu wa mtoto huyo, Jacob Mrope alisema tukio hilo lilitokea Septemba 2 saa 6 mchana ambapo mjukuu wake ambaye ni yatima alikuwa akitoka shuleni huku akiwa na wenzake wawili wakike, walikimbizwa na watuhumiwa hao ambapo yeye alishindwa kukimbia kutokana na kuumia mguu na kujikuta akibakwa.

Mrope alisema kuwa wanafunzi wenzake aliokuwa nao walisema kuwa baada ya watuhumiwa hao kumkamata walimziba mdomo kisha wakaanza kumuingilia kwa zamu ambapo mwanafunzi huyo hakuweza kupata msaada wowote hadi watuhumiwa hao kutimiza haja zao.

"Wenzake waliokuwa nao walitoa taarifa nyumbani kwa mlezi wake ambaye ni dada yake ambapo alikwenda na kumkuta akitokwa na damu nyingi na alipomuuliza alisema kuwa wenzake wamembaka ndipo alimchukua na kumpeleka shuleni kutoa taarifa," alisema Mrope.

Kwa upande wake dada yake Lwiza alisema kuwa yeye alipata taarifa kupitia kwa wanafunzi hao ambao alikuwa nao wakati wanatoka shule na kukimbizwa na watuhumiwa hao, ambapo walisema kuwa ilibidi warudi na kumkuta mwenzao akitokwa damu, wamkokota mwenzao hadi nyumba iliyojirani na kumjulisha.

"Alikuwa kwenye hali mbaya kwani alikuwa akitokwa na damu nyingi na nilipomuuliza alisema kuwa amebakwa na mtuhumiwa ambaye alimtambua na kumtaja jina mwenye umri wa miaka 10 akiwa na wenzake watatu," alisema Lwiza.


Lwiza alisema kuwa baada ya kuona hali ile walimpeleka shule na uongozi wa shule ukamwelekeza kufuata taratibu za kisheria ambapo walikwenda Serikali ya mtaa kisha kwenda polisi na baadaye Hospitali ya Tumbi kwa matibabu zaidi ambapo hadi juzi mwanafunzi huyo alikuwa bado kalazwa na hali yake inasemekana kuwa ni mbaya.

Naye Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Lulanzi, Anna Bilali alisema kuwa wao kama uongozi wa shule hawawezi kusema lolote kwani suala hilo liko kwenye vyombo vya sheria pamoja na kitabibu na watakuwa tayari kusema mara taarifa zitakapokamilika.


"Ni kweli tukio hili limetokea lakini bado haijathibitishwa kama ni kweli au la na pia lilitokea nje ya shule na muda wa shule kwa wanafunzi wa madarasa ya chini walisharuhusiwa kurudi nyumbani mara baada ya masomo kwisha," alisema Bilali.

Akizungumzia tukio hilo mjumbe wa mtaa wa Lulanzi, Rasul Shaban alisema kuwa walipata taarifa hiyo na kushangazwa na kitendo hicho ambapo tukio hilo ni la mara ya kwanza kutokea katika shule hiyo ambayo iko kwenye mtaa huo na pia walitoa barua za kuwadhamini wanafunzi wanaotuhumiwa kufanya tukio hilo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Ulrich Matei alisema kuwa hadi sasa wanawashikilia wanafunzi wanne wenye umri kati ya miaka 10 na 13 kuhusiana na tukio hilo.

Hemedy PHD atangaza kuacha kuvaa hereni

Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii mwigizaji Hemedy Suleiman maarufu kama Hemedy au Fernando (a.k.a yake mpya) amesema kuwa hatavaa tena hereni kwenye kuigiza kwani ameshakuwa mtu mzima sasa.

Hemedy ambaye hivi majuzi alisherehekea kutimiza miaka 27 ya kuzaliwaameandika kuwa kama mtu mzima, hata vaa tena hereni katika movie zake.

Hatujaweza kujua kama ataacha kabisa kuvaa hereni au ni kwenye uigizaji tu.


Ila hapo nyuma mwezi uliopita wakati msanii huyo akichat EATV katika kipindi cha KIKAANGONI LIVE aliweza kusema kuwa amejifunza mengi na moja ya jambo alilojifunza ni kuwa mashabiki zake hawapendi yeye avae hereni wakati anaigiza, kwahiyo hiyo inaweza ikawa sababu ya Hemedy kuamua kuacha kuvaa hereni

Wednesday, September 4, 2013

Mkono wa Aunt Ezekiel hatarini kuoza

INASIKITISHA! Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson ‘Gwantwa’ yupo hatarini kukatwa mkono kutokana na jeraha la chupa alilolipata hivi karibuni.

Tukio la Aunt kupigwa chupa na mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Yvonne nje ya Club Bilicanas, Posta jijini Dar, lilitokea Agosti 26, mwaka huu wakati staa huyo alipokwenda kujiachia na mshosti zake.

Baada ya kupigwa chupa siku hiyo, Aunt alikimbizwa katika Hospitali ya Aga Khan lakini bahati mbaya alikosa daktari wa kumtibu hivyo akalazimika kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Dk. Mvungi, Kinondoni ambapo alishonwa nyuzi sita pamoja na dawa za kukausha kidonda.

ALIKATISHA DOZI
Kwa mujibu wa chanzo makini, Aunt ni muoga wa dawa na wakati kidonda kikiwa bado hakijapona vizuri aliacha kumeza dawa alizopewa.

Chanzo hicho kilisema tatizo la staa huyo kukatisha dozi lilisababisha kidonda kishindwe kupona na badala yake kikaanza kutengeneza usaha na taratibu mkono ukaanza kuoza.

“Mkono ulifikia hatua ukaanza kuoza kwani licha ya kushonwa lakini kilibadilika rangi ndipo alirudi hospitali.

ASAFISHWA UPYA
Imeelezwa kuwa mapema wiki hii, Aunt alirudi tena katika Hospitali ya Dk. Mvungi na kusafishwa upya kidonda baada ya madaktari kugundua tatizo lilizidi kuongezeka.

MKONO ULIANZA KUOZA
Kwa mujibu wa nesi wa hospitali hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake, hali ya Aunt ilimshtua daktari, akamwambia aombe Mungu kwani kidonda kilichimbika sana na tatizo kama hilo huweza kusababisha mtu kukatwa mkono.

 “Iligundulika mkono ulikuwa unaoza, daktari alimwambia amuombe Mungu kwani hatua iliyokuwa imefikia ni mbaya hivyo asipokuwa makini tatizo hilo litamfanya akatwe mkono,” alisema nesi huyo.

CHANZO CHA UGOMVI NI NINI?
Licha ya kuhusishwa na ugomvi wa kimapenzi baina yake na mpenzi wa Yvonne anayejulikana kwa jina la Joff, Aunt alisema ugomvi wao uliisha zamani na kila mmoja ana maisha yake.

“Yale mambo yalipita, yeye ana maisha yake na mimi nina yangu,” alisema Aunt.

Wakati huohuo, taarifa ambazo Amani limezipata kuhusu mtuhumiwa wa Aunt, Yvonne ambaye alifikishwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar siku ya tukio, anahaha kukwepa kifungo kwani uchunguzi ukikamilika atapelekwa mahakamani kisha gerezani.

AY achaguliwa katika tuzo za muziki za Channel O


Kwa mwaka mwingine tena, AY ametajwa kuwania tuzo za muziki za Channel O.Msanii huyu pekee kutoka Tanzania ndiye aliyeingia kwenye tuzo hizo za CHOAMVA 2013 ambazo zinafanyika kwa mara ya 10. AY ametajwa kuwania vipengele viwili kwenye tuzo hizo ambavyo ni MOST GIFTED MALE VIDEO ambapo Video yake iliyoingia inaitwa PARTY ZONE ambayo amemshirikisha MARCO CHALI, pamoja na kipengele cha MOST GIFTED AFRICA EAST na Video yake hiyo hiyo.

VIPENGELE VYOTE KWA UJUMLA

MOST GIFTED DUO/GROUP FEATURING VIDEO
TEAR GAS – Wake Up
XTATIC/AKA & PRIDDY UGLY -Hit Em Up
MI CASA – Can’t Get Enough
EME – Baddest Boy
NAETO C FT D’BANJ – Tony Montana (Bad Pass) Remix

MOST GIFTED NEWCOMER VIDEO
MONEOA – Is’bhanxa
LOLA RAE – Watch My Ting Go
KHAYA MTHETHWA – Move
VICTORIA KIMANI – Mtoto
BURNA BOY – Tonight

MOST GIFTED FEMALE VIDEO
ZONKE – Feelings
LIZHA JAMES FT ANSELMO RALPH – Vais Rochar
STL – Stella Stella Stella
TIWA SAVAGE ft DON JAZZY – Without My Heart
TOYA DELAZY – Heart

MOST GIFTED MALE VIDEO
DONALD – Over The Moon
Zeus FT AKA & TUMI – #DatsWasup
WIZKID – Azonto
AY/MARCO CHALI – Party Zone
IYANYA – Flavour

MOST GIFTED RAGGA/DANCEHALL VIDEO
BUFFALO SOULJAH – Basawine
KAAKIE – Too Much
JESSE JAGZ – Murder Dem
P-UNIT FT COLLO – You Guy (Dat Dendai)
RADIO AND WEASEL – Can’t Let You Go

MOST GIFTED HIP HOP VIDEO
AKA – Jealousy
JAYSO & SARKODIE – Pizza & Burger
REASON – Do It Like I Can
IFANI FT BLAKSUGA – Chocolate Vanilla
EL/M.aNIFEST – Hallelujah

MOST GIFTED R&B VIDEO
BANKY W – Yes/No
ANSELMO RALPH – Curticao
DANNY K – Brown Eyes
CHASE – Lonely
VICTORIA KIMANI/M.I – Oya

MOST GIFED AFRO POP VIDEO
THE SOIL FT ZAKWE – Linkomo
SAUTI SOL – Money Lover
2FACE IDIBIA – Ihe Ne Me
THE MUFFINZ – Umsebenzi Wendoda
DAVIDO – Gobe

MOST GIFTED DANCE VIDEO
KCEE – Limpopo
MAFIKIZOLO – Khona
FUSE ODG FT WYCLEF JEAN – Antenna (Remix)
DJ MALVADO FT PETTY – Jamaica
DJ GANYANI FT FB – Xigubu

MOST GIFTED KWAITO VIDEO
L’VOVO DERRANGO FT PROFESSOR – Palesa
PROFESSOR FT OSIKIDO & CHARACTER – Finger Prints
EES – Woza December
KABELO – Impilo
DJ TIRA FT BIG NUZ & JOOCY – Summer Time

MOST GIFTED AFRICAN (WEST) VIDEO
D’PRINCE – Goody Bag
ICE PRINCE – Aboki
R2BEES – Life (WALAAHI)
DBLACK FT JOEY – Vera
CHIDINMA FT ILLBLISS & SUSPECT – Emi Ni Ballar
P-SQUARE – Alingo

MOST GIFTED AFRICAN (EAST) VIDEO
AY/MARCO CHALI – Party Zone
P-UNIT FT COLLO: You Guy (Dat Dendai)
RADIO & WEASEL – Can’t Let You Go
SAUTI SOL – Money Lover
NAVIO – Kata

MOST GIFTED AFRICAN (SOUTH) VIDEO
DAMA DO BLING – My Eish
OSKIDO – Tsa Mandebele
BLACK COFFEE FT ZAKES – Take it All Off
PAUL G FT FABULOUS – Get Control
DJ DIMPLEZ ft L-TIDO & ANATii – We Ain’t Leaving
KHULI CHANA – Hazzadazmove

Tuesday, September 3, 2013

Watambue matajiri 10 nchini Tanzania

KATI ya miaka ya 1960 hadi 1980, mtu kuwa tajiri alionekana ni hatari kwa taifa, tena mali zake alizimiliki kwa kificho, vinginevyo angeitwa mhujumu uchumi. Lakini kwa sasa mambo yamebadilika, taratibu sera za kibepari zinatawala, ujamaa unapewa kisogo.

Mtu kama ni mbunifu, ana nidhamu ya kutofuja pesa na anafanya kazi sana kwa nini asiwe tajiri? Utandawazi unasaidia ndiyo maana leo tunaweza kuwatambua mabilionea wakubwa ambao wanastahili pongezi kwa hatua walizopiga. Tusisahau kuwa wanaibeba nchi kwa ulipaji kodi.

1. SAID BAKHRESA
Jina lake kamili ni Said Salim Awadh Bakhresa. Jarida la Forbes mwaka jana, lilimuorodhesha miongoni mwa matajiri 40 Afrika kwamba anamiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 620 (karibu shilingi trilioni moja). Hata hivyo, inadaiwa kuwa tabia ya usiri wa Bakhresa inafanya mali zake zisijulikane sana, ila ni tajiri zaidi ya kiwango hicho.

Ndiye mmiliki wa makampuni ya Bakhresa yanayotoa bidhaa zenye chapa ya Azam ambazo zinauzwa nchi mbalimbali Afrika. Ana viwanda vya nafaka na vinywaji, vyombo vya usafiri wa majini, uuzaji wa chakula, bidhaa za plastiki na kadhalika. Ndiye mmiliki wa Klabu ya Azam FC.

2. GULAM DEWJI
Huyu ni baba wa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji ‘Mo’. Jarida la Forbes mwaka jana lilimtaja kuwa na utajiri wenye thamani ya dola milioni 560 (karibu shilingi bilioni 900). Mafanikio yake kibiashara yalianza mwaka 1970. Kiwanda chake cha 21st Century Textiles, kinatajwa kuwa moja ya viwanda vikubwa vya nguo Afrika.

3. ROSTAM AZIZ
Inadaiwa anamiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 420 (shilingi bilioni 672). Anamiliki karibu asilimia 40 ya hisa Kampuni ya Vodacom Tanzania. Ni mmiliki wa Kampuni ya Caspian inayohusika na uchimbaji wa madini na ukandarasi nchini Tanzania, nchi kadhaa za Afrika na Asia.

4. DK. REGINALD MENGI
Anatajwa kumiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 280 (karibu shilingi bilioni 450). Ni mmiliki wa kundi la makampuni ya IPP, yanayomiliki vyombo vya habari, viwanda, migodi ya dhahabu, Tanzanite na kadhalika.

5. ALI MUFURUKI
Utajiri wake unatajwa kuwa na thamani ya dola milioni 110 (shilingi bilioni 176). Ni mmiliki wa kundi la makumpuni ya Infortech Investment, inayomiliki maduka yanayouza vitu vya rejareja Tanzania na Uganda. Vilevile ana vitega uchumi vingine.

6. MUSTAFA SABODO
Ni mfayabiashara mkubwa sana nchini anayemwaga mamilioni kwa misaada. Wakati wa kuanzishwa kwake, aliipa Taasisi ya Mwalimu Nyerere shilingi milioni 800, akasaidia shilingi milioni 100 katika mradi wa kustawisha mimea jamii ya kunde. Vilevile alikipa Chadema shilingi milioni 300. Inadaiwa kuwa utajiri wake unazidi shilingi bilioni 100. Kampuni yake ya Khoja Shia Itnasheri Jamat (KSIJ), ndiyo yeye tenda ya kujenga maeneo ya maegesho ya magari Posta, Dar es Salaam, mradi wenye thamani ya shilingi bilioni 5.6.

7. ABDUL-AZIZ ABOOD
Kiwango chake cha utajiri hakiwekwi sana wazi lakini anatajwa kuwa miongoni mwa mabilionea 10 wanaotikisa nchi kwa sasa. Anamiliki viwanda kadhaa mkoani Morogoro, vyombo vya habari, Abood Radio na TV. Anamiliki mabasi ambayo yanafanya safari zake kati ya Morogoro, Mbeya na Dar es Salaam. Ni Mbunge wa Morogoro Mjini (CCM).

8. MICHAEL SHIRIMA
Ni mmiliki mkuu wa Shirika la Ndege la Precision ambalo linafaya safari zake ndani ya Tanzania pamoja na nchi mbalimbali za Afrika. Ana asilimia tano ya hisa katika Beki ya I&M (Tanzania), vilevile ni memba katika bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo yenye thamani ta shilingi bilioni 200. Hisa zake Precision ni asilimia 42.91.

9.  YUSUF MANJI
Kiwango halisi cha utajiri wake bado hakifahamiki lakini anafahamika kama mmoja wa mabilionea wakubwa nchini Tanzania. Ni mmiliki wa makampuni ya Quality Group na majengo ya Quality Centre, Quality Plaza na kadhalika. Ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga na utajiri wake umeifaya timu kutotetereka tangu alipoanza kuiongoza.

10. MOHAMMED DEWJI
Baba yake anashika nafasi ya pili katika orodha hii. Dewji au Mo kama anavyoitwa na wengi, anatajwa kuwa bilionea nambari moja katika orodha ya mabilionea vijana Afrika (orodha hiyo tuliitoa wiki iliyopita). Ni mmiliki wa makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL) ambayo inatengeneza faida ya shilingi bilioni 136 kwa mwaka

Malinzi na Nyamlani wameteuliwa rasmi leo kugombea urais TFF.


Wagombea wawili, Athumani Nyamlani na Jamal Malinzi wamepitishwa kuwania nafasi ya Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Malinzi na Nyamlani ambaye anashikilia nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, wamepitishwa baada ya usaili uliofanyika jijini Dar es Salaam.

 Upinzani kati ya Nyamlani na Malinzi umekuwa mkali sana tokea walipotangaza tu kugombea.

Katika nafasi hiyo kulikuwa na wagombea wanne na wawili kati yao hawakupita ambao ni Omary Mussa na Richard Lukambula.

Kwa upande wa umakamu wa urais, Wallace Karia na Iman Madega, mwenyekiti wa zamani wa Yanga, ndiyo waliopitishwa kuwania nafasi hiyo.

 Wakati huohuo, usaili huo pia umemng’oa Shaffi Dauda aliyekuwa nawania ujumbe.

Monday, September 2, 2013

Diamond ampiga vijembe tena Wema

Jana video ya muziki ya Msanii Diamond platnumz ya wimbo wa My Number one imetoka rasmi kwenye Television na mitandao mbalimbali ya kijamii na kusema ukweli ni moja ya video nzuri sana za muziki hapa nchini na sio siri kijana huyu wa bongofleva amefanya kazi kubwa sana na anastahili pongezi.

Baada ya kuisikiliza kwa makini nyimbo hii yenye mahadhi flani ya kiafrika zaidi tulifika kwenye dakika ya 2 na sekunde 50 (2:50) ya nyimbo hii na ndipo ukatokea “ubishi” ambao tukaona sio mbaya tukiupeleka kwa wasomaji wetu ili kupata maoni Zaidi.

Katika sehemu hii ya mwisho ya nyimbo hii Diamond anatamka maneno ambayo baadhi ya watu tuliokuwepo katika mabishano hayo tunasema kuwa yanamlenga mwanadada wetu muigizaji, Wema sepetu kama “vijembe” kwakwe, diamond anamalizia wimbo wake kwa kusema “TUACHE TULALE” maneno amabyo kwa wale wanafuatilia habari za watu hawa wawili yalioongewa na mpenzi wa diamond wa sasa VJ penny kwenye tukio la wapenzi hao kumrekodi mwanadada Wema Sepetu kwenye simu alipokuwa akimbembeleza mpenzi wake wa zamani (Diamond Platnumz) warudiane, tukio liliotokea miezi kadhaa iliyopita.

Swali likawa, Je maneno haya yatakuwa yanamlenga Wema??? Kama siyo kwanini Diamond ayatamke sehemu ambayo hata haihusiani nayo kwenye wimbo???

The Chocolate waibuka washindi wa Dance 100, 2013



Shindano la kucheza linalo fahamika kama DANCE 100% jijini dar-es salaam limekamilisha mpambano wake katika uwanja wa DONBOSCO OYSTEBEY siku ya tar:31-08-2013.

Mashindano hayo yalianzia(USAILI) katika uwanja wa DONBOSCO UPANGA,TTC CHANG”OMBE na kumaliziwa DONBOSCO OYSTEBEY jana.

Ylikuwa makundi mengi sana ila kati ya hayo yaliofanikiwa kuingia hadi fainali ni makundi matano 5 tu nayo ni :D DI,WT(watoto wa Tanzania),WAKALI SISI,THE CHACOLETE na THE WINNERS pia kulikuwa na mizunguko miwili ambao wa kwanza walicheza wimbo walio chagua (wahusika wa kuu wa kundi husika ) na mzunguko wa pili ilikuwa wimbo uliochaguliwa kwa bahati na sibu na wahusika wa kuu wa kundi husika kwa kuokota CD ambozo waandaaji  waliziandaa

Yalio kuwa yanahitajika ni makundi matatu tu,THE WINERS wakatoka na kubaki yale yalio kidhi vigezo kwa maksi za majaji:WAKALI SISI walishika namba 3.walipata zawadi ya shilingi 500,000 za kitanzania,DDI wakashika namba 2 walipata zawadi ya shilingi 1,500,000 za kitanzania na THE CHOCOLETE ndio walio ibuka namba 1, na kuchukua kitita cha zawadi ya shilingi 5,000,000 za kitanzania toka Vodacom Tanzania.

Henry Joseph kutambulishwa rasmi

KIUNGO mpya wa klabu ya Simba, Henry Joseph, leo anatarajiwa kuwemo katika kikosi cha timu hiyo kitakachomenyana na Mafunzo ya Zanzibar, katika mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Joseph amesajiliwa na Simba akitokea klabu ya Kongsvinger ya Norway.

Mechi hiyo itawapa fursa mashabiki wa klabu hiyo kuwaona wachezaji wake wapya wakiwemo, Amisi Tambwe na Gilbert Kaze ambao wote wanatoka katika klabu ya Vital O ya Burundi.


Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, mechi hiyo ambayo ni ya kwanza kwa Simba kucheza katika uwanja huo itakuwa ni kujiweka sawa kabla ya kucheza na Mtibwa Sugar kwenye uwanja huo, Septemba 14.

Kamwaga alisema mbali ya kutazama mechi hiyo, pia mashabki watapata fursa ya kumuaga mchezaji Kiggi Makasi anayekwenda nchini India kwa ajili ya matibabu ya goti na ataondoka Septemba 9.

My Number 1 - Diamond


Thursday, August 29, 2013

Mapacha waliozaliwa wameungana Zenji, wafanikiwa kutenganishwa

Jopo la Madaktari Bingwa Saba wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Mifupa ya hospitali hiyo (Moi), wamefanikiwa kuwatenganisha pacha waliokuwa wameungana kiwiliwili.

Iliwalazimu mabingwa hao kutumia saa nne kufanikisha upasuaji huo. Mmoja wa watoto hao waliotenganishwa, amelazwa kwenye Wodi ya Uangalizi Maalumu (ICU) Taasisi ya Mifupa Moi wakati kiwiliwili kingine kilifariki.(P.T)

Jopo la madaktari waliofanikisha upasuaji huo ni; bingwa mstaafu wa watoto ambaye aliitwa maalumu kwa kazi hiyo, Petronila Ngiloi, Dk Robert Mhina (mifupa) na Profesa Karim Manji aliyekuwa akifuatilia kwa karibu mapigo ya moyo.

Wengine ni Dk Karima Khalid aliyekuwa akiratibu dawa ya usingizi, Dk Hamis Shaaban (ubongo na uti wa mgongo), Dk Zaitun Bokhary (bingwa upasuaji watoto) na Dk Nyangasa (moyo na mishipa ya fahamu).

Akizungumza baada ya upasuaji huo, Dk Shaaban alisema walimfanyia vipimo mtoto ambaye hakuwa amekamilika na kugundulika kuwa hakuwa amekamilika viungo vyote achilia mbali kutokuwa na kichwa na macho pia hakuwa na moyo, figo, tumbo, maini ila alikuwa na uti wa mgongo.

"Uti wa mgongo ulikuwepo na ndio uliokuwa umeshikana na mwenzake na kuna mshipa mmoja wa fahamu ulikuwa unafanya kazi ndio maana alikuwa ukimgusa anachezesha mguu."

Alisema kinachoratibiwa kwa sasa ni kuangalia dawa ya usingizi aliyopewa mtoto ambaye anaendelea kupumua na kwamba ndani ya saa 24, dawa ya usingizi waliyomuwekea mtoto huyo itakuwa imeisha na ataanza kunyonya kama kawaida.

Upasuaji
Kazi ya upasuaji huo ilianza saa mbili asubuhi kwa mtoto huyo wa jinsi ya kike aliyetimia kuchukuliwa vipimo mbalimbali ikiwemo CT Scan, MRI, Ultra sound na vingine vingi kabla ya upasuaji kamili kuanza saa tano asubuhi.

Dk Shaaban alisema ni mara ya kwanza kwa Moi kufanya upasuaji wa aina ile na kwamba mara nyingi wamekuwa wakifanya upasuaji wa watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa pamoja na mgongo wazi ambao tatizo hilo linasababishwa na upungufu wa madini ya folic acid.

Kabla ya upasuaji kuanza, mama wa mtoto huyo Pili Hija (24) alitumia muda wa nusu saa kufanya maombi maalumu ya kumwombea mtoto wake kisha kuwaruhusu madaktari kuendelea na upasuaji huo.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuruhusiwa kumwona mtoto wake, Hija alisema: "Ninamshukuru Mungu kwa yote na nazidi kumwomba amjalie mwanangu apone kabisa, nawashukuru na nitazidi kuwaombea madaktari wanaomtibu mwanangu."

Alijifungulia nyumbani Agosti 18 maeneo ya Jang'ombe, Zanzibar watoto pacha walioungana mmoja akiwa amekamilika viungo vyote na mwingine akiwa na kiwiliwili.

Kahaba ala kichapo baada ya kujiuza karibu na msikiti

Kahaba  mmoja   alijikuta akiambulia kichapo kikali toka kwa vijana wa kiislamu baada ya kunaswa akijiuza karibu na msikiti wao..

 Kutokana na kukerwa na vitendo hivyo, vijana hao wanaofanya ibada katika msikiti huo, waliamua  kuwatafuta vijana wa ulinzi shirikishi na kuwapa kazi hiyo ya kuwakamata na kuwacharaza bakora kisha kuwapeleka katika kituo hicho cha polisi.

“Tumeamua kuwakamata na kuwacharaza bakora, hawana ustaarabu wala busara hawa, wanakojoa na kutupa kondomu  hovyo, “ alisikika mmoja wa vijana hao.
Mmoja wa vijana hao aliyekuwa akisimamia kwa karibu zoezi hilo, aliwaambia waandishi wetu kuwa wameamua kufanya hivyo na litakuwa zoezi endelevu kutokana na wanawake hao kutokuwa wasikivu kwani kila wanapoambiwa juu ya kukaa mbali na nyumba hiyo ya ibada hawasikii.

Alisema kuwa siku moja wanawake hao walimtoa udhu muumini mmoja ambaye alikuwa akienda kuswali alfajiri baada ya kumshika na kusababisha akose kuhudhuria swala siku hiyo.


Hata hivyo, wakati mahojiano yanaendelea, mmoja wa askari waliokuwa zamu aliamuru mwanamke huyo aingizwe lokapu kusubiri kesho yake aunganishwe na wenzake kisha wapelekwe mahakamani.

Habari zilizotufikia  ni kwamba baada ya kufikishwa mahakamani na kukutwa na kosa la uzururaji, wakahukumiwa kifungo cha miezi sita jela au faini ya shilingi elfu hamsini ambapo walilipa kiasi hicho na bado wanaendelea na biashara hiyo maeneo hayo.



Wednesday, August 28, 2013

Hemedy PHD aendelea vizuri

Muigizaji Hemedy Suleiman ambaye pia ni mwanamuziki wa Bongofleva amefunguka kuwa anaendelea vizuri baada ya kupata ajali mbaya ya gari na gari hilo kudaiwa kuharibika.

 Hemedy alikuwa akimsindikiza Gerry Wa Rhymes ambaye pia ni msanii maarufu nyumbani kwake Sinza na kupata ajali baada ya kugonga kalivati. Kupitia mtandao mmoja wa kijamii Hemedy ameandika

"Namshukuru mungu naendelea vizuri baada ya kupata ajali mbaya iliyonikuta..ahsanteni kwa dua zenu, kifua tu ndiyo kimeumia na mkono"

Get well soon Hemedy

Friday, August 23, 2013

Mwakyembe, magufuli na Lukuvi wakumbwa na tuhuma nzito

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema itawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu kwa kulidanganya Bunge.

Hatua hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe baada ya kumhoji Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka wa fedha 2011/2012.

Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo kiasi cha Sh348,075,000,000 fedha za ndani zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililotajwa kuwa ni la mradi maalumu (Special Road Construction Project) hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni.

“Ni vizuri leo uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. Tunajua kwamba fedha hizi zilipunguzwa kiasi cha Sh95 bilioni na kupelekwa Wizara ya Uchukuzi, zilibakia Sh252.975bilioni katika kifungu hicho lakini kuna bilioni 100 zimetumika visivyo,” alisema Zitto, ambaye pia ni Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini (Chadema).

Alisema katika majumuisho ya Bajeti ya wizara hiyo, Dk Magufuli na Dk Mwakyembe wakati huo akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Lukuvi walitoa maelezo yasiyo ya kweli bungeni kuhusu fedha.

Alikariri maneno yaliyorekodiwa kwenye Hansard ya Bunge yaliyosemwa na viongozi hao watatu.

“Tunaomba fedha Sh252 bilioni kwa ajili ya kuanzia kazi za ujenzi wa barabara,” Zitto alisema akikariri maneno ya Dk Magufuli wakati anawasilisha bajeti.

“Fedha hizi zitachangia miradi ya wafadhili,” haya yalikuwa maneno ya Dk Mwakyembe wakati akifanya majumuisho.

“Hizi ni fedha kwa ajili ya counterpart fund,” alimkariri Lukuvi wakati akichangia hotuba ya wizara hiyo.

Zitto alisema CAG alihoji mwaka huu kuhusu matumizi ya fedha hizo na alitoa taarifa akidai kuwa fedha hizo zilikuwa miradi hewa na kasma kivuli.

Zitto alisema kuwa Dk Magufuli na Katibu Mkuu wake walipohojiwa walidai kutumia fedha hizo kulipa madeni.

“Kwa nini mlidanganya Bunge? Mliomba fedha za kuanza miradi maalumu. Hamkuomba fedha za madeni. Kwa nini mliunda kasma kivuli na kuifuta baada ya pesa kulipwa?” Zitto alimhoji Balozi Mrango.

Katika majibu yake, Balozi Mrango alisema kwa nia njema, fedha hizo zilitumika kuwalipa makandarasi waliokuwa wamechachamaa, huku baadhi yao wakisisitiza kusitisha kuendelea na miradi. Hivyo wakalazimika kuomba fedha kwa njia hiyo ili miradi kuendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Zitto hakuridhishwa na majibu hayo akisema hapakuwa na haja ya kutumia fedha hizo kuwalipa makandarasi wakati kulikuwa na kasma yao ya awali. Alisema kama kulikuwa na haja hiyo, wizara isingeita mradi rasmi.

“Jambo hili siyo sahihi hata kidogo kulidanganya Bunge na hadi sasa wewe na waziri wako hamuonyeshi kukubali kosa hili, hata Waziri Lukuvi naye alisisitiza bungeni kwamba fedha hizo zinaombwa ili kutekeleza mradi maalumu lakini sasa imebainika sivyo, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge tutawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ili wahojiwe nao wajieleze kwa kulidanganya,” alisema Zitto.

Pia kamati hiyo imeitaka wizara hiyo kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu matumizi ya Sh100 bilioni zilizotumika kinyume na maombi yaliyowasilishwa kwenye Bajeti ya mwaka huo wa fedha.

CAG ameshauri madeni yote ambayo Wizara ya Ujenzi inadaiwa yaorodheshwe ili yawe wazi kuepuka migongano katika matumizi ya fedha.

Alipoulizwa kuhusu madai hayo, Lukuvi alisema haelewi chochote na kusisitiza kuwa akipata taarifa rasmi za Kamati ya PAC, atatoa ufafanuzi.



Halmashauri zinavyotafuna mabilioni

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAACc), imeeleza namna mamilioni ya fedha za Serikali zinavyoibwa kutoka Hazina kupitia halmashauri za wilaya huku Ilala ikitajwa kuongoza kwa ufisadi huo.

Mwenyekiti wa LAAC, Rajab Mbarouk Mohammed aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba Hazina imekuwa ikipeleka fedha kwenye halmashauri zikiwa zimezidi na kwamba kiasi kinachozidi hakirudishwi badala yake huliwa.

Alisema kamati hiyo imefanya uchunguzi kwenye halmashauri 43 na kubaini kwamba mtindo huo ndiyo unaotumika kuiba fedha za Serikali.

“Mwaka 2011/12 kiasi cha Sh1.5 bilioni zilipelekwa zikiwa zimezidi kwenye halmashauri hizo lakini hazikurudishwa Hazina kama inavyoonyesha kwenye ripoti ya CAG.

Alisema kati ya kiasi hicho, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilipewa ziada ya Sh213 milioni ikifuatiwa na Geita iliyopewa Sh129 milioni.

“Fedha hizo za mishahara zilipelekwa kwenye halmashauri hizo na Hazina kimakosa zikiwa zimezidi lakini watendaji wa hawakuzirudisha kama wanavyotakiwa kisheria badala yake zikayeyuka,” alisema.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa uchunguzi huo pia ulibaini kwamba katika halmashauri hizo 43 kiasi cha Sh693 milioni hulipwa mishahara hewa ambayo wafanyakazi wake walishakufa na wengine kustaafu.

Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ililipa mishahara hewa yenye thamani ya Sh79.4 milioni ikifuatiwa na Ukerewe iliyolipa Sh57.5 milioni.

Kwa upande wa fedha za miradi ya maendeleo, mwaka 2011/12, Hazina ilipeleka katika Halmashauri ya Mbarali, Mbeya Sh724 milioni kwa ajili ya Mradi wa Maendeleo ya Elimu Sekondari wakati mradi huo ulikuwa ukihitaji Sh70 milioni tu.

“Kiasi cha Sh654 milioni zilipelekwa kimakosa na Hazina lakini badala ya kurudishwa zilitumiwa katika mazingira ya kutatanisha,” alisema.

Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe ilipelekewa ziada ya Sh500 milioni na Mvomero ilipewa Sh85 milioni. “Kuna mtandao mkubwa wa Hazina na halmashauri ambao ukiachwa utaendelea kupoteza fedha nyingi za walipakodi,” alisema.

Hatimaye GK kurudi kwenye gemu rasmi


Hatimaye baada ya kimya cha muda mrefu Mwanzilishi wa kundi la East Coast Team (ECT) “Crazy Gk” aliyetamba na nyimbo kama sauti ya Manka, miko kumi ya rap, sister sister na simba wa afrika anamipango ya kurudi kwenye game la bongo flava.

Msanii huyo aliyepotea kwa muda mwingi akiwa masomoni sasa anataka kurudi tena kwenye game na atazindua wimbo wake mpya wiki ijayo kupitia radio station tofauti tofauti hapa Tz.

Tusubiri tuone ukimya wake uko vipi, Je ataweza kubamba na kukubalika kama ilivyokuwa hapo mwanzo au watoto wadogo wa sasa watampiga bao...karibu kakka mkubwa!!!

Ujenzi wa bweni la wanafunzi albino waanza chini ya Miss TZ Brigitte



MREMBO wa Tanzania, Brigitte Alfred ameonyesha mfano wa kuigwa nchini katika tasnia hiyo baada ya kuanza ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (albino) katika wilaya ya Shinyanga wanaoishi katika shule maalum ya Buhangija. Tayari mrembo ameweka jiwe la msingi na kupandisha ukuta sambamba na kukabidhi mabati 200 kwa ajili ya kujengea paa la bweni hilo la wavulana lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 50.

Makabidhiano hayo yalifanywa na mrembo huyo kwa katika hafla fupi iliyohudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi, afisa elimu wa manispaa ya Shinyanga Honoratha Ruhumbika na walimu wa shule hiyo wakiongozwa na mwalimu mkuu, Peter Ajali.

Briggite alisema kuwa ameamua kutimiza ahadi yake aliyoitoa mwezi Aprili mwaka huu alipotembelea Shinyanga kwa kazi za jamii na kuona changamoto za watoto wanaosoma katika shule hiyo.

Alisema kuwa mpango huo upo katika mpango wa Miss Tanzania ujulikano kwa jina la Urembo wenye malengo maalum (Beauty with Purpose) nay eye kuamua kufanya kwa vitendo.

“Ni faraja kwangu kuona kuwa ninatimiza ahadi yangu, nawashukuru wote walionisaidia ikiwa pamoja na familia yangu, na ninaomba wengine wanisaidie kwani badi kuna changamoto nyingi katika ujenzi na kazi za jamii kwa ujumla,” alisema Brigitte.

Alisema kuwa amepania kuweka historia katika fani hiyo kwani anaamini ujenzi au jingo hilo litakuwa kumbukumbu kubwa kwake tena kwa vizazi na vizazi.

Brigitte pia aliwataka wanafunzi hao kutokata tamaa hata kwa wale wasiokuwa karibu na familia zao na kwamba wamtegemee zaidi Mwenyezi Mungu kwa kuwa yeye ndiye mfariji kwa wanyonge huku akiwahimiza kuzingatia zaidi elimu kwani ndiyo msingi wa maisha yao.

 “Nilipata msukumo wa kuisaidia shule hii hususani katika ujenzi wa bweni hilo kutokana na ujio wake wa mwezi Aprili mwaka huu shuleni hapo na kujionea adha wanayopata watoto hao kutokana na msongamano mkubwa mabwenini,” alisema.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi alimpongeza Brigitte kwa moyo huo wa kujitolea na kuwataka warembo wengine kuiga mfano wake. Nyamubi alisema kuwa alichokifanya Brigitte ni jambo la kukumbukwa nan i msaada mkubwa kwa jamii hasa kwa watu wenye ulemabu wa ngozi.

Mkuu huyo wa wilaya aliwaomba wazazi wa watoto hao kuwa na tabia ya kuwatembelea watoto wao mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kuwachuku wakati wa likizo. Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo Peter Ajali alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo la msongamano mabwenini kwani kuna jumla ya watoto 247 huku mabweni yaliyopo yana uwezo wa kukaa watoto 148 tu.

Thursday, August 22, 2013

Tundaman akimbia uchi, kisa deni la laki 4


Msanii Tundaman amejikuta akiambulia aibu ya mwaka baada ya kujitosa nusu uchi mtaani akiwakwepa askari polisi ambao walivamia kwake leo asubuhi kwa lengo la kumkamata....

Chanzo cha Tunda man kusakwa na polisi ni deni la sh. laki nane ambazo alikopa mwanzoni mwa mwaka huu kwa mwanadada mmoja ( jina kapuni)....

Taarifa zinadai kwamba, baada ya kupewa hela hiyo, Tunda man aligeuka kisima cha matusi ya nguoni kwa mrembo huyo. Kila akipigiwa simu alikuwa hapokei, na akipokea ni matusi ya nguoni.....

Baada ya hali hiyo, mwana dada huyo aliamua kulifikisha swala lake polisi ambapo Tundaman alikamatwa. Akiwa mikononi mwa polisi, msanii huyo aliomba apewe nafasi ya kulilipa deni lake kwa awamu tatu kuanzia tarehe 12/8/2013

Baada tarehe hiyo, Tundaman hakuweza kulipa kiasi chochote na wala hakutoa ushirikiano wowote, hali iliyomfanya mwanadada huyo arudi kuripoti polisi....

Polisi walianza jitihada za kumsaka ambapo leo majira ya saa nne asubuhi walivamia kwake ( Tabata Savana ) kwa lengo la kumkamata.....

Bahati nzuri au mbaya, Tundaman alifanikiwa kuwatoroka polisi akiwa na bukta tu ( kwa mujibu wa mashuhuda) na kutokomea kusikojulikana...