Monday, August 15, 2011

MAPACHA WATATU WABANWA NA MKATABA

MAPACHA WATATU

KHALID CHOKORAA
Bendi ya Muziki wa Dansi nchini, "Mapacha watatu" imelazimika kuendelea na Show zake katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kutokana na kubanwa na mkataba ambao wamesaini na moja ya kumbi ambazo hutumia katika kupiga show zao.

Akizungumza na kipindi cha Afrobeat kinachorushwa na kituo cha Eatv, mmoja wa wakurugenzi wa bendi hiyo KHALID CHOKORAA amesema, wamelazimika kuendelea na Show katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kutokana na kubanwa na mkataba wa mwaka mzima ambao wamesaini na Club ya Mzalendo.
Aidha Chokoraa amesema kuwa hata hivyo, wanapiga Show moja tu kwa wiki badala ya tatu kama ambavyo ilikuwa imezoeleka na mashabiki wao.

Wakati huohuo Bendi hiyo inatarajia kuzindua album yao ya pili ambayo bado hawajaipatia jina mwishoni mwa mwaka huu, ambapo nyimbo nne zimekwishakamilika na wanatumia muda huu wa Ramadhani katika kukamilisha nyimbo mbili zilizosalia na ndipo watatangaza rasmi siku ya uzinduzi.

Amezitaja nyimbo ambazo zimekwishakamilika kuwa ni mtoto wa paka utunzi wa Kalala Jr, Wosia wa babu uliotungwa na Josee Mara, Mjasiriamali na Sumu ya mapenzi Remix za kwake Khalid Chokoraa.


Kwa mengi zaidi kuhusiana na habari hii fuatilia AFROBEAT jumamosi hii saa moja jioni!!!!! USIKOSEEEE...

No comments:

Post a Comment