Friday, July 27, 2012

SHIGONGO AFUNGUKA KUHUSU ISHU YA CHAMELEONE

Mkurugenzi wa kampuni ya Global Publishers Erick Shigongo Pichani juu, amefunguka kuhusu tuhuma zilizokuwa zinamkabili za kushikilia Passport ya mwanamuziki kutoka nchini Uganda Jose Chameleone.Akizungumza na kipindi cha HOTMIX kinachorushwa na EATV jana jioni, Shigongo amesema alifikia hatua hiyo kwa lengo la kumuonyesha Chameleone na wanamuziki wengine kutoka Nchi zingine za Afrika Mashariki kuwa watanzania si wa tu wajinga na wanajua wanachakifanya. Katika mengi aliyoongea pia ameeleza kukerwa kwake na kitendo alichokifanya Chameleone jana cha kwenda katika ubalozi wa Tanzania nchini Uganda na kubamiza mlango na kuongeza kuwa hiyo ilikuwa ni ishu ya biashara ya wao wawili hivyo hakupaswa kulifikisha huko ila walipaswa kumalizana wao wawili.. Hata hivyo Shigongo amekiri kushikilia Passport hiyo na hadi jioni hiyo tayari alikuwa ameshairudisha sehemu husika.

Monday, July 23, 2012

NIMEIPENDA HII KUTOKA KWA ROMA

SOMETIME TUKUBALI CHANGES!!! TAZAMA MTU ALIKUWA ANAISHI MAISHA FULANI ZAMANI KUTOKANA NA SABABU FULANI!! MFANO ALIKUWA ANAKAA MASKANI SANA NA MACHIZI WAKE AU MASHOSTI ZAKE WAKIPIGA UMBEA...LAKINI LEO YULE MTU KAPATA KAZI AU OFISI AU KAENDA KUSOMA NA MENGINEYO THN AKIRUDI ANAKUWA HANA MUDA AU HADHI YAKE HAIMRUHUSU KUKAA MASKANI NA VIJIWENI!! THN WALE MARAFIKI ZAKE WANAMPONDA JAMAA KATOKA KIMAISHA SAIVI ANATUTUPA ANATUPITA NA GARI HATA MASKANI HAKAI ANASALIMIA TU ANAPITA!!!MFANO MTU KAMA HASHIM THABIT LABDA ZAMANI ALIKUWA ANAKAA MASKANI SINZA PALE BUT NWDAYZ U THINK NI VEMA YY KUKAA PALE TENA?? ANAHITAJI ULINZI, NCHI NYINGI ZINAMTEGEMEA IMAGINE!! MSANII ANATAKIWA ALINDE IMAGE YAKE NA SIO KUONEKANA KILA MARA BUT MASHABIKI WANATAKA TUKAE NAO MDA WOTE KAMA ZAMANI NA TUSIPOFANYA HIVO WANATUKATAA!!! INANICHOSHA SANA HII HALI AISEE!! SAWA PATA PESA TUJUE TABIA YAKO..NA HAITAKIWI UCHANGE TO THE MAXIMUM BUT TUJIFUNZE KUKUBALI CHANGES!!! NILISOMA NA MTU ZAMANI NA TUKAWA TUNATANIANA SANA!! LEO NIMEMIT NAE KANIKUTA KWENYE SHOW NIPO NA MASHABIKI WALE WANAONIHESHIMU NA KUNITHAMINI AAAF YY ANANIITA JINA LA UTANI LA SHULE ZAMANI HUKU AKIJISIFU AAAH MI NAMJUA HUYO KWANZA ALIKUWA HIVI NA HIVI NA HIVI SAIVI KATOKA ANAJISIKIA!!HAHAHAHAH MIMI NIKAPOTEZEA...JAMAA AKAONDOKA NA JIBU KUWA JAMAA ANAJISIKILIZIA WAKATI YY HAKUJUA KAMA ILE NI KAZI YANGU HATA MM NIKIENDA OFISI YAKE ANAYOWORK NISINGEMTOA HESHIMA VILE....SO ACCEPT CHANGES MARAIA AAAF TUELIMIKE NA KUHESHIMU KAZI ZA WATU.. Source:http://djchoka.blogspot.com/

KESI YA LULU YAENDELEA KUPIGWA DANA DANA

Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu  Kanda ya Dar es Salaam Amiri Msumi leo asubuhi  ameahirisha kesi  inayomkabili msanii wa Filamu nchini, Elizabeth Michael(Lulu) anayetuhumiwa kumuua aliyekuwa msanii nyota wa filamu nchini Steven Charles Kanumba Aprili 7,2012.

Akiahirisha kesi hiyo Msajili huyo alisema kutokana na sababu za Jaji anayesikiliza kesi hii katika Mahakama Kuu Jaji Dk. Fauz Twaib kutokuwepo Mahakamani amelazimika kuahirisha kesi hiyo hadi Agosti 20.

"Kwa kuwa Jaji Dk. Fauz Twaib ni mwalimu katika chuo cha  Sheria hivyo yuko katika mitihani naahirisha kesi hii hadi tarehe hiyo niliyoitaja ambapo itakuja kutajwa".

Thursday, July 19, 2012

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YATANGAZA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO KUFUATIA AJALI YA MELI

Na Juma Mohammed, MAELEZO Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia Julai 19 hadi Julai 21 kufuatia maafa ya ajali ya Meli ya Mv. Skagit  iliyozama karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein akitangaza maombolezo hayo, alisema bendera zote zitapepea nusu mlingoti na kwamba shughuli za sherehe na burudani zimefutwa kwa muda wa siku tatu za maombolezo.

Dk. Shein alisema shughuli za Serikali zitaendelea kama kawaida. Katika taarifa yake aliyoitoa Ikulu usiku wa kuamkia Julai 19, Rais Dk Shein amewahakikishia wananchi na hasa waliopoteza jamaa zao kuwa Serikali itabeba gharama zote za mazishi na pia kugharamia huduma za matibabu kwa majeruhi.

“Nimesikitishwa sana na msiba huu, Katika wakati huu si vema tukaanza kulaumiana jambo la muhimu hivi sasa  ni kuokoa maisha ya watu” Alisema Rais Dk. Shein.

Mbali ya taarifa hiyo, Rais Dk Shein aliungana na wananchi, viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, Viongozi wa dini katika kutambua maiti zilizofikishwa katika eneo maalum la viwanja vya Maisara Suleiman.

Mbali ya kwenda katika viwanja hivyo, pia alifika katika eneo la bandari ya Zanzibar kufuatilia taarifa za tukio hilo. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana lilisitisha shughuli zake kufuatia maafa hayo ambapo wakati wa jioni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Nchimbi alitarajiwa kufanya majumuisho ya bajeti yake.

Baadhi ya Wabunge wakiongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Jeshi la Polisi walitembelea majeruhi katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja pamoja na eneo la viwanja vya Maisara ambapo maiti hufikishwa kwa ajili ya utambuzi.

Mbali ya Bunge, pia Baraza la Wawakilishi Zanzibar jana lilisitisha kwa muda shughuli zake ili kutoa nafasi kwa Wawakilishi hao wa wananchi kushiriki katika shughuli  za uokozi ambapo wengi walifika bandarini kusaidia kazi mbalimbali ikiwemo kuwafariji waliopoteza ndugu zao.

Taarifa kutoka Mamlaka za Serikali zinaeleza kwamba hadi asubuhi hii maiti 30 zilipatikana ambapo 20 kati ya hizo zimetambuliwa na kuchukuwa na jamaa zao huku wananchi wengine wakiendelea na kuzitambua maiti zinazofikishwa katika eneo la Maisara.

Aidha, katika taarifa hiyo, watu 145 wameokolewa wakiwa hai, wengi wao wapo katika hali nzuri wameruhusiwa kuungana na familia zao baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar.

Meli ya Mv. Skagit ilizama  Julai 18,2012 saa 7:50 mchana ikitokea Bandari ya Dar es Salaam kwenda Zanzibar ikiwa imebeba abiria 250 watu wazima, watoto 31 na mabaharia 6.

Kazi ya  utafutaji na uokoaji zinaendelea asubuhi hii  katika eneo la tukio ilikozama meli hiyo umbali wa maili sita Kusini mwa Kisiwa cha Yasin karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.

BAADHI YA MATUKIO YA UOKOAJI WA WATU WALIOZAMA NA MELI YA STAR GATE KATIKA BAHARI YA CHUMBE HUKO VISIWANI ZANZIBAR

Picha kwa hisani ya http://www.kajunason.blogspot.com/

Wednesday, July 18, 2012

HAPPY BIRTHDAY NELSON MANDELA

Rais wa zamani wa Afrika kusini ambaye pia ni Rais wa kwanza mweusi kwa Nchi hiyo Mzee Nelson Mandela a.k.a Madiba leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo ametimiza miaka 94 tangu kuzaliwa kwake. Kwa upande wake ataisherehekea siku hii pamoja na Familia yake pamoja na ndugu, jamaa na marafiki zake wa karibu, wakati huo huo kutokana na heshima aliyonayo nchini humo(Afrika Kusini) shughuli mbalimbali zinaendelea kuandaliwa katika kusherehekea naye kwa pamoja katika siku hii muhimu

MASHUJAA MUSICA WATAMBULISHA VIDEO MPYA YA RISASI KIDOLE

Meneja wa Bendi ya mashujaa Musica Martin Sospeter (kushoto) akiwa pamoja na Rais wa bendi hiyo Charlez Baba wakionesha CD ya video ya wimbo wao uliobeba jina la albamu ya bendi hiyo 'Risasi Kidole' wakati wa utambulisho kwa waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa Business Park ambao ndiyo ukumbi wao wa Nyumbani, uliopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

WOLPER AJIANDAA KUUPOKEA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN

MUIGIZAJI nyota wa filamu nchini Jacqueline Massawe amesisitiza kwamba amebadili dini na na kuwa Muislam na kwa sasa anajiandaa kwa kuupokea na kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza jijini DSM Wolper amesisitiza kwamba yeye kwa hivi sasa ni muislamu na amejitayarisha kufunga na kujizuia kufanya shughuli za kisanii ambazo zitamsababishia kutengua saum yake hivyo kwa kipindi hicho cha muda wa mwezi mmoja atakuwa akijishughulisha na kazi zake zingine.

"Unajua dini ni imani na hii iko ndani ya moyo wangu hivyo nachukizwa kwa kitendo cha baadhi ya ndugu zangu wa karibu kuniita MALAYA na hukumu kwa mambo mbalimbali mimi ndiyo najua nafanya nini katika maisha yangu"alisema.

Aidha amewatupia dongo wale wote wanao mtupia maneno ya kumdhihaki kwamba hatoweza kufunga na kuswali , "Unajua tumepewa miezi 11 ambayo tuko huru kufanya mambo mbalimbali ya starehe za kidunia kwanini nishindwe kujizuia ndani ya mwezi mmoja tu, mimi nasema hivi  nitasali sitakuwa na makucha , manywele  na mambo mbalimbali ambayo hayapendezi katika ibada "

Tuesday, July 10, 2012

MZIGO MPYA KUTOKA RJ COMPANY(THE GLORY OF RAMADHAN)

Kama ambavyo unaona hapo juu watu wakiwa busy mzigoni, huo ndiyo mzigo mpya kutoka RJ Company unaitwa The Glory of Ramadhan na Dullah mjukuu wa Ambua ndani, kaa tayari kuupokea.. Zaidi zama humu

Monday, July 9, 2012

WEMA, WOLPER WALIVYOPAMBA USIKU WA MATUMAINI


Wolper akiingia uwanjani kwa ajili ya pambano na Wema
Wema naye akiingia uwanjani kwa makeke
Mpambano ukaanza
Baada ya pambano wakakumbatiana kama ishara ya kuonyesha watu kuwa hamna Bifu kati yao na mwisho tukatangaziwa matokeo kuwa wametoka droo hamna aliyeshinda
Mpambano kati ya Cheka na Kaseba haukufanyika kwa sababu Cheka alikataa kupigana kwa madai kwamba anayetaka kupigana nae hana kiwango cha kupigana na yeye
Umati wa watu waliojitokeza kwenye Tamasha hilo amablo liliandaliwa kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya wasichana vijijini.
Tukishow Luv Kutoka kushoto ni mimi(Kijah), Millard Ayo, Maulid Kambaya, Patrick Nyembera na Thabit Zakaria, Picha kwa hisani ya Millardayo.com