Sunday, August 28, 2011

MERCY JOHNSON SASA NI PRINCESS

Katika ndoa ya kimila Prince & princess Okojie wakiwa na furaha

Mambo yakanoga zaidi kwa ndoa ya kanisani

Kuolewa raha jamani

Mambo ya makeup hayo

Mercy ndani ya Shella

Hayawi hayawi sasa yamekuwa, baada ya vikwazo vya hapa na pale viliwavyotia mashaka baadhi ya watu wakiwemo mashabiki wa Mercy wakihofia kutofungwa kwa ndoa ya Mercy Johnson na Prince Odianosen Okojie hatimaye ndoa hiyo tayari imefungwa.

Kikwazo kiliibuka baada ya mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Lovely Okojie kujitokeza na kudai kuwa yeye ni mke halali wa Prince huyo ambapo siku chache baadae ikathibitishwa kuwa ndoa ya Mercy na Prince Okojie itafungwa kama kawaida kwa kuwa mwanamke huyo mwenye watoto wawili tayari alikwishaachika miaka kadhaa iliyopita.

 Ndoa ya Mercy Johnson na Prince Okojie imefungwa juzi jumamosi katika kanisa la Christ Embassy Church lililopo jijini Lagos nchini Nigeria baada ya kufungwa kwa ndoa ya kimila siku ya Ijumaa hukohuko jijini Lagos.

No comments:

Post a Comment