Tuesday, August 30, 2011

KALUNDE BAND WANAKUJA STYLE YA MDUARA

Bendi ya Muziki wa Dansi nchini, "Kalunde Band" inatarajia kutambulisha wimbo wake mpya wa mduara katika maonyesho yake yote ya Sikukuu ya Eid El-fitri, ambao umetungwa na na mpiga kinanda wa bendi hiyo Mwakichui Saleh.

Kiongozi wa Bendi hiyo Bob Rudala (Pichani) amesema wimbo huo umepewa jina la "Imebaki Story" ambao ni miongoni mwa nyimbo mpya zilizokamilika hivi karibuni kwa ajili ya Album yao ya pili.
Ameongeza kuwa wimbo huo utatambulishwa siku ya Eid Mosi katika Onyesho lao la ukumbi wa Trinity uliopo Oysterbay jijini Dar Es Salaam na kisha kutambulishwa Eid pili katika ukumbi wa New kunduchi Beach Hotel.

No comments:

Post a Comment