Thursday, August 4, 2011

JAHAZI MODERN TAARAB KUTOA KIBAO CHA SHUKRANI KWA MASHABIKI

MZEE YUSUF

Baadhi ya waimbaji wa Jahazi Modern Taarab
 Kundi la Muziki wa Taarab hapa nchini, (Jahazi Modern Taarab) linaandaa wimbo kwa ajili ya kuwashukuru mashabiki wake kwa Sapoti waliyoitoa tangu kundi hilo lilipoanzishwa December 2007 mpaka kufikia sasa.


Akizungumza na Blog hii, kiongozi wa kundi hilo MZEE YUSUF amesema, katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani watapumzika kwa kutofanya onyesho lolote  kama ilivyo kwa Vikundi vingi, ambapo ndani yake watakuwa wakitengeneza nyimbo ambazo zitakamilisha Album yao ukiwemo wimbo maalum walioutunga kwa ajili ya kuwashukuru mashabiki, vyombo vya habari na Bendi zingine ambazo zimekuwa zikiwapa sapoti, album hiyo itazinduliwa Dec 24 mwaka huu wakati wa Birthday Party ya JAHAZI kutimiza miaka mitano itakayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Ameongeza kuwa sambamba na utengenezaji wa nyimbo watafanya pia video za nyimbo hizo ili kuwaridhisha mashabiki wao ambao wamekuwa wakilalamikia ucheleweshwaji wa Video za nyimbo zao mbalimbali.

Baadhi ya nyimbo ambazo zimekwishakamilika ni pamoja na Utaniona hivihivi, Sina muda huo na Uhondo wa ngoma.

No comments:

Post a Comment