Friday, June 29, 2012

VINCENT KIGOSI(RAY) AFANYA UZINDUZI WA FILAMU YA SOBING SOUND SAMBAMBA NA KUTOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA

Vincent Kigosi (Ray) na meneja wa Steps Ent. Ignas Kambarage wakiwa na Watoto Yatima wa kituo cha Maunga Centre kilichopo kinondoni DSM, baada ya kukabidhi msaada katika kituo hicho
Msanii wa filamu nchini, Vincent Kigosi(Ray) akikabidhi msaada kwa mlezi wa kituo cha Maunga Centre Bi. Zainab Bakari, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa filamu yake ya Sobbing Sound aliyocheza kwa kushirikiana na Mastaa wengine ambao ni Irene Uwoya na Haji Adamu(Baba Haji).. katika tukio hilo vyakula mbalimbali vimetolewa vikiwa na thamani ya shilingi milioni moja.

Friday, June 22, 2012

HUU NI ZAIDI YA UNYAMA

Mtoto huyu amekutwa ametupwa akiwa amefariki huko maeneo ya msikiti wa Soweto jijini Mbeya leo Asubuhi!! Tunaomba Radhi kwa picha mtakazoziona.
Picha hizo mbili zinamuonyesha mtoto huyo ambaye hakuweza kufahamika jina lake wala mama yake, akiwa ametolewa kwenye mfuko wa Salfet aliokuwa amehifadhiwa na kutupwa, hiyo khanga ni kutoka kwa msamaria mwema
Baadhi ya watu waliofurika kushuhudia tukio hilo la kinyama... Zaidi zama hapa

Thursday, June 21, 2012

MCHEZA SINEMA MAARUFU DUNIANI KUKIMBIA MBIO ZA KILA MWAKA ZA MOUNT KILIMANJARO MARATHON

Mcheza sinema maarufu duniani kutoka nchini Marekani Deidre Lorenz atakimbia mbio za kila mwaka za Mount Kilimanjaro Marathon zinazoanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 24 Juni mwaka huu kutoka Moshi Club mjini Moshi.
Mbio hizi zilizoanzishwa na mama Marie France kutoka katika mji wa Bethesda, Maryland nchini Marekani mwaka 1991 ni mbio zinazojulikana kama 7 continental Races na zimeshawahi kupata tuzo mbalimbali za kimataifa.

Ujio wa mcheza sinema huyu aliyecheza sinema nyingi kama vile Santorini Blue, Perfect Strangers, The Great Fight, na nyingine nyingi unaiweka Tanzania katika macho ya dunia na kuwavutia watalii wengi kutoka taifa hili tajiri duniani. Deidre Lorenz alizaliwa katika jiji la Oregon nchini Marekani lakini akahamia katika jiji la New York City linalijulikana kama "The Big Apple" nchini Marekani akiwa na kampuni yake ya kutengeneza sinema inayoitwa Thira Films LLS.


eidre Lorenz ameshawahi kuteuliwa zaidi ya mara tatu kugombe tuzo za wacheza sinema maarufu duniani zinazojulikana kama Grammy Awards. Mcheza sinema huyu ataambatana na Wamarekani wengine kuja nchini tarehe 21 Juni kukimbia mbio hizi ambazo zimetokea kuutangaza sana mji wa Moshi tangu mwaka 1991. Lorenz alipatikana katika bahati nasibu iliyochezwa wakati wa mbio za New York Marathon mwaka jana.


Naye mwanzilishi wa mbio hizi mama Marie Frances ana historia ya kuanzisha mbio na matamasha mbalimbali duniani. Alikuwa pia mwanzilishi wa mbio za Pyramid Marathon nchini Misri pamoja na Miss Universe Egypt matamasha yaliyojizolea sifa kemkem.Aliombwa kuja kuanzisha mbio za Marathon nchini Tanzania na balozi wa Tanzania wa wakati ule nchini Misri.Mbio za Mt. Kilimahjaro Marathon ni moja kati ya mbio tafauti za marathon zinazifanyika katika mji wa Moshi.


Mount Kilimanjaro Marathon zitaanzia Moshi Club mpaka Rau madukani na kurudi mara tatu ambazo zitakuwa kilimeta 42. Kutakuwa pia na mbio z akilometa 21, kilimeta 10 na kilometa 5 kwa watoto. Wakimbiaji hawahitaji kuwa na ujuzi wa kukimbia watu wote wanaweza kukimbia.

Wednesday, June 20, 2012

AZAM WASIKIA KILIO CHA WAZANZIBAR, WALETA MELI MPYA KWA USAFIRI WA ABIRIA NA MAGARI YAO

Meli hiyo inavyoonekana kwa pande zote
Meli hiyo inavyoonekana kwa nje

KUTOKA UTANGAZAJI MPAKA UIGIZAJI NA KOTE ANAKAMUA

Mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na kituo cha EATV, Abdallah Hamis Ambua a.k.a Mjukuu amefunguka kuwa pamoja na kufanya vizuri kwenye Utangazaji lakini pia ana vipaji lukuki ambapo kwa sasa ameibukia kwenye uigizaji.

HUU NI USHINDANI AU NI MAENDELEO TU

X6 inayotumiwa na Jack Wolper ambayo inadaiwa kuwa amenyang'anywa

Siku chache zilizopita Msanii wa filamu Bongo Jacqline Wolper aliutangazia Umma gari yake mpya anayoitumia aina ya X6 na tetesi nyingi tukazisikia huko mtaani na kwenye baadhi ya vyombo vya habari moja ya tetesi hizo ni kuwa gari hiyo si yake ila amepewa na mwanaume na lakini ghafla likaibuka jingine kuwa Wolper amenyang'anywa gari hiyo na huyo aliyempa


Kabla halijasahaulika hilo ghafla zikasikika habari katika vyombo mbalimbali vya habari kuwa Wema Sepetu kwa sasa anamiliki gari nyingine aina ya Mark X badala ya ile Lexus hapo juu pamoja na nyumba anayoishi sasa ambayo pia ni mali yake.
 Wakati hayo yakiendelea jana kwenye Website yake mwana bongo Flava Diamond Da Platinumz ametupia gari yake mpya na kuwaambia mashabiki wake wanaoitembelea Website hiyo kuwa waishuhudie kisha wakawasimulie wenzao.. Sasa jamani huu ni ushindani au Maendeleo maana kila mmoja akinunua gari, nyumba anakimbilia kwenye vyombo vya habari hawa watu wako kwenye mashindano au wanajaribu kutuonyesha kuwa sanaa bongo inalipa au ni njia ya kutuhamasisha vijana wenzao tujitume ili tupate maendeleo kama ya kwao? Sijui!!!!!

Tuesday, June 12, 2012

ODAMA NDANI YA HOTMIX YA EATV

Mamaa Odama akijiachia baada ya Interview kaliii
Katika pozi, kushoto ni Anna Mbajo na kulia ni Fatna Ramole HOTMIX Presenters na katikati ni Odama kutoka Bongo Movi! shukrani kwa Odama kwa kuja kwenye show.

Thursday, June 7, 2012

SIJAWAHI KUTEMBEA NA JACK PENTZEL WALA SHILOLE-TIMBULO

Timbulo
Msanii mchanga ndani ya Game la Bongo Flava na aliyepata kashfa kwa kucopy nyimbo za watu, Timbulo amekanusha uvumi uliopo kuwa ameshawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na dada zake, Jack Pentzel maarufu Jack wa Chuz pamoja na mwanadada anayekimbiza kwenye Game la muziki Bongo na Filamu za kitanzania.. Kabla ya kuibuka na kukanusha uhusiano huo huko nyuma kulikuwa na uvumi wa Dogo huyo kutoka na Shilole na baadae kuhamia kwa Jack na kwa nyakati tofauti wadada hao walikiri kuwa na uhusiano na mdogo wao huyo ambapo Jack alithibitisha kuwa wanaishi pamoja na wanapika na kupakua lakini ghafla zikasikika habari kuwa wawili hao tayari wamemwagana.  Cha ajabu Timbulo aliwekwa kati jana na kipindi cha HOTMIX cha Eatv na kukana hayo yote kwa kusema ni maneno ya uzushi yanayolenga kumharibia kisanaa.. (Picha ya chini inamuonyesha Timbulo akiwa na Jack katika pozi la kimahaba)

Monday, June 4, 2012

SAJENTI AKANA TUHUMA ZA CHARLES BABA

Mzazi mwenza wa Mwanamuziki Charles Baba, Husna Idd (Sajent) pichani, ameibuka na kukana tuhuma alizozitoa baba huyo wa mtoto wake wiki mbili zilizopita kuwa Sajent ana tabia ya kugombana na kila msichana anayeanzisha uhusiano na baba mtoto wake huyo. Akizungumza na Blog hii Sajent alisema kuwa amesikia madai hayo ya Charles Baba na kudai kuwa maneno hayo ni ya kizushi kwa kuwa yeye anatambua kuwa walishamwagana na Charles siku nyingi hivyo hawezi kugombana na mwanamke wa Charles kwa sasa kwa kuwa anamchukulia mwanaume huyo kama baba wa mtoto wake tu na si vinginevyo. Husna ameongeza kuwa Charles na wanawake wake huwa wanajishtukia kila wamuonapo kutokana na uzuri alionao nakukiri kuwa yeye ni mzuri hivyo huwapiga kwa kutumia uzuri alionao na si kwa ngumi.