Thursday, September 26, 2013

Tanzania hatarini kuvamiwa na Al shaabab

WAKATI wananchi wa Afrika Mashariki wakijawa na hofu ya mashambulio yanayopangwa kufanywa na vikundi vya ugaidi vya Al Qaeda na Al Shabab, imebainika kuna Watanzania waliopewa mafunzo ya ugaidi wanaojiandaa kufanya maovu.

Hayo yamebainika siku chache baada ya wanamgambo wa kundi la Al Shabab kufanya mashambulio katika Jengo la Biashara la Westgate mjini Nairobi na kuua watu zaidi ya 70 na kuacha mamia wengine wakiwa wamejeruhiwa.

Mkuu wa Interpol Tawi la Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Gustav Babile aliyasema hayo jana katika mahojiano maalumu na MTANZANIA.

Alikuwa akizungumzia kauli ya hivi karibuni iliyotolewa na Msemaji wa Al Shabab, Sheikh Abdulaziz Abu Muscab aliyetoa tahadhari kwamba kundi lake linapanga mashambulio mengine Tanzania na Uganda.

Babile alisema taarifa zinaonyesha vijana wa Tanzania waliojiunga na mafunzo ya ugaidi yanayotolewa na vikundi vya Al Qaeda na Al Shabab, wamefanya hivyo baada ya kushawishiwa watapata utajiri wa haraka.

Alisema hali hiyo imevifanya vyombo vya ulinzi na usalama nchini kutoipuuza kauli hiyo ya Sheikh Abdulaziz Abu Muscab.

“Tunajua wapo Watanzania wanapewa dozi za ugaidi, na sisi siyo kisiwa, watu ni hao hao… tumejipanga kuyakabili haya na kuushirikisha umma katika ulinzi,” alisema.

Babile alisema kauli ya msemaji wa kundi la Al Shabab ya kuivamia Tanzania siyo ya kupuuza na kusisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini viko tayari kukabiliana na lolote litakalotokea.

“Tumeisikia kauli yake kwenye mitandao ya jamii, imetufanya kuwa alert (macho) vya kutosha, imetuweka sawa na imetukumbusha kuwa tunaweza kuvamiwa wakati wowote.

“Hatuja-relax hata kidogo, tumejiweka sawa kwenye human resources zetu, materials resource na hata frontline officers wetu wako makini mno.

“Mfano kwenye viwanja vya ndege ambako ni muhimu, kuna mitambo inayoweza kugundua hati za kusafiria za washukiwa wa uhalifu wanaotafutwa kimataifa na tutawakamata tu.

“Lakini hata kwenye mipaka yetu yote hatuko peke yetu, tumepanua wigo wa kupata taarifa za kiintelijensia na katika kufanya kazi hii tunashirikiana na vyombo vyote vya ulinzi na usalama,” alisema.

Baada ya kufanya mashambulio mjini Nairobi Jumamosi iliyopita, Msemaji wa Al Shabab, Sheikh Abdulaziz Abu Muscab, aliripotiwa kwenye mitandao ya jamii akisema shambulio hilo lilikuwa ni la kulipiza kisasi baada ya majeshi ya Kenya kuvamia kundi hilo lenye makazi yake mjini Kismayu, Somalia.

Mitandao ya jamii pia ilimnukuu Sheikh Abu Muscab akijigamba kuwa wakati wowote mashambulio ya kikundi hicho yataelekezwa Uganda na Tanzania.

Wakati huohuo, Babile amesema Mtanzania mmoja alikamatwa Kenya akishukiwa kuwa ni mmoja magaidi waliovamia jengo la Westgate.

Bila kumtaja jina, alisema mtu huyo ni mkazi wa Arusha na alikamatwa muda mfupi baada ya kuingia Kenya akitoa Tanzania, akitumia usafiri wa mabasi ya abiria.

“Walipomkamata wakatuletea taarifa sisi, tukatafuta kwenye database zetu na information za ndani zikatuonyesha hakuwa mtu hatari, tukamuachia.

“Kilichowatia hofu na kumshuku mtu huyu ni muda alioingia Kenya na muda wa tukio lilipotokea… lakini tumeangalia taarifa zote tukagundua hakuwa na shaka,” alisema Babile.Maombi yasababisha aibe maiti ya baba yake.

Mtu mmoja aliyeiba maiti ya baba yake kutoka makaburi ya Detroit amewekwa chini ya uangalizi jana na kuamriwa kuhudhuria tiba ya akili ama atafungwa jela.

Vincent Bright, miaka 49, alinusurika hukumu ya kifungo jela. Alipatikana na hatia Agosti ya kufukua mwili huo.Bright lazima aendelee kupatiwa tiba ya afya ya akili na kumwonesha ofisa wake uangalizi kwamba anatumia dawa, Jaji wa Mahakama ya Wayne County James Chylinski

"Kama hufanyi hivyo, nitalazimika kukufunga jela," alisema jaji huyo. Mnamo Januari, mwili wa Clarence Bright mwenye umri wa miaka 93 ulitoweka kutoka kwenye makaburi ya Gethsemane, muda mfupi baada ya msiba wake lakini kabla jeneza halijafukiwa. Wanafamilia waliwaongoza polisi kuelekea kwenye mwili huo katika jokofu nyumbani kwa Vincent Bright huko Detroit.
Bright alikamatwa pale polisi walipomkamata ndani ya gari akiwa na jeneza tupu nyuma ya gari hilo.

Polisi wakati huo walisema Bright alikuwa mfuasi wa dini na alikuwa na matumaini baba yake atafufuka na kuishi tena kutokana na maombi.

Aligundulika hakuwa na akili timamu kuweza kukabili mashitaka, lakini afya yake ya kiakili ikaimarika baada ya wiki kadhaa za matibabu na uchunguzi kwenye hospitali za serikali.
"Alipitia kipindi kibaya, misongo mingi ya mawazo. ...Anaendelea vema. Yuko kwenye matibabu," wakili anayemtetea Gerald Karafa alisema nje ya mahakama, akizungumzia vifo vya wazazi wa Bright.

Alisema ilikuwa 'ushahidi binafsi' ambao afya ya kiakili ya Bright ilitawala katika wizi huo.

Bright alikataa kuzungumzia suala hilo nje ya mahakama. Baada ya kukamatwa kwake, alitumikia siku 225 jela au mahabusu katika hospitali za serikali.

Dhamana yake ilipangwa kuwa Dola za Marekani 75,000 hivyo mchanganuo wa afya ya akili unaweza kukamilika, ambao utaweka kumkuta akiwa tayari kukabili mashitaka.

Endapo atapatikana na hatia ya kufukua mwili, Vincent Bright anaweza kukabiliwa na kifungo cha hadi miaka 10 jela, kama hangekuwa amewekwa chini ya uangalizi kwa matatizo ya akili.

Wednesday, September 25, 2013

50 CENT aanza kufulia

Miaka mitatu kama sio miwili iliyopita 50 Cent alikuwa akishikilia nafasi za juu kabisa huku akinyemelea nyao za Jay Z na P Diddy.

Kwenye mtiririko ambao unatolewa na Forbes, 5o Cent ameshika nafasi ya 19 kwenye list ya wasanii wa hip hop wanaoongoza kuwa na hela nyingi.

Nafasi ya kwanza inashikiliwa na P Diddy wakati Jay Z akishilia nafasi ya pili, Dr Dre nafasi ya tatu, Nick Minaj nafasi ya nne wakati boss wake Birdman anashika nafasi ya tano, sita ni Kanye West, Saba ni Lil Wayne.

50 Cent amepitwa na wasinii ambao wamechipukia kwenye game kama Kendrick Lamar na Macklemore.

Bongo Movie inashikiliwa naye JB na Wema

Baada ya utafiti uliyofanywa umebahatika kuwapata wasanii wa Bongo muvi wanaongoza kwa kupendwa na mashabiki hapa Tanzania kutokana na kazi zao za Filamu.

JB ni mmoja wa wasanii kwa upande kiume anaeongoza kwa kupendwa na mashabiki wake kutokana na uwezo wake katika uigizaji wa muvi.

Funga kazi kwa mwanadada Wema Sepetu ndiyo msanii wa pekee wa Bongo muvi anaeongoza kwa kupendwa na mashabiki lukuki wa mjini na vijijini, licha kuwa na skendo zake kibao ila Watanzania wana-show love kwake.

Tuesday, September 24, 2013

Nje kwa mechi 3, yamemkuta Baloteli

MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amefungiwa mechi tatu kufuata kumvaa refa katika mchezo ambao timu yake, AC Milan ilichapwa mabao 2-1 na Napoli Jumapili.

Balotelli, ambaye alikosa na kufunga bao zuri la kufutia machozi kwa timu yake, alionyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya mechi kwa kumvaa refa.

Mshambuliaji huyo wa Italia sasa atakosa mechi tatu zijazo kwa kosa hilo.
Balotelli, ambaye alifunga penalti zake zote 21 za awali katika mechi rasmi, mkwaju wa Jumapili uliokolewa na kipa wa Napoli, Pepe

Kadi hiyo nyekundu ya utata, inamaanisha Super Mario atakosa mechi na Bologna, Sampdoria na Juventus, ingawa Milan inaweza kukatia rufaa adhabu hiyo. Chanzo: binzubeiry

Anamlalamikia mkewe, hebu mpe ushauri

Habari,
Mimi nimeoa na ndoa yangu ina miaka 7 sasa na tuna watoto wa 2. Nlimuoa mwanamke aliyekuwa kamaliza degree ambaye alikuwa home tu at the time anatafuta ajira. Toka nimuoe hajawahi kufanya kazi yoyote ile yaani Goalkeeper mpaka leo na kutafuta kazi alisha acha. Mpaka leo hii mke wangu hajabadilika. Namlipa mshahara mwisho wa mwezi ambao ni sawa na kama 10k per day yaani (300k).

Kila ninapojaribu kumtafutia kazi anafanya kidogo tu anaacha. Huwezi amini hata umlazimishe vipi ajishughulishe mzito ile mbaya. Mi ni mfanyabiashara(Magari Makubwa) nimemuanzishia vimiradi through the years vyote kala mtaji. Kuna kipindi alijaribu kusoma masters ya bussiness administration nkamlipia ada, nunua vitabu vyote alafu yeye akaamua kuacha baada ya mwezi tu Eti kuamka alfajiri hawezi. Nkaja nkamuomba basi asome chuo ambacho atakuwa anaingia mchana nacho alishindwa.

Tatizo rafiki yake mkubwa ni mama yangu mzazi hivo kuna kipindi nlikata mshahara wake ili kumlazimisha afanye kazi akakimbilia kulia manyanyaso nikalazimishwa hela yake isiguswe na wazazi wangu. Nkienda kazini namuacha nyumbani na home kwenyewe hafanyi chochote anaita tu housegirl. Yaani yupo yupo tu siku hadi siku. Nifanyaje ili hata nikianguka leo au kesho awe ni mama atakayeweza kusomesha watoto.

Alafu matumizi yake ya hela mabaya yaani hela yake mwenyewe ukimpa mwanzo wa mwezi kwenye tarehe 1 hiv basi ikifika tarehe 8 ujue alikuwa anaumwa. Ila ni hela yake na hainunui hata nguo ya mtoto hivyo hainihusu. Nifanyaje ajishughulishe?

Thursday, September 12, 2013

Rado asema Bongo movie wanasubiri ufariki ndio wajitokeze

MSANII wa filamu na mtayarishaji pia wa filamu Bongo Simon Mwakipagata ‘Rado’ amelishutumu na kulilaumu kundi la filamu la Bongo Movie Unity kwa kukosa upendo na kushindwa kusaidia katika matatizo, Rado aliyasema hayo kufuatia hivi karibuni kupata ajali ya gari na kujikuta akijiuguza pekee yake bila kupata faraja kutoka kundi hilo wakati yeye ni katibu wa kundi hilo.

“Siku zote mimi upenda kuwa mkweli hata kama mwingine atachukia hivi karibuni wakati narudi kutoka Location nilipata ajali na kuumia sehemu ya kifua ilikuwa ni ajali mbaya namshukru Mungu kuniponya lakini rafiki zangu wa Bongo movie hakuna hata mmoja aliyejitokeza kunijulia hali wakati walikuwa na taarifa, lakini tu hao hao wangesikia nimekufa wangekuwa wa kwanza kuunda kamati ya mazishi,”anasema Rado.

Msanii huyo nyota anadai kuwa tukio hilo ni la pili kwake kupata ajali lakini mara zote hizo amekuwa jirani na wasanii ambao alikuwa akiigiza nao katika kundi la Jumba la Dhahabu ambao ni Niva, Baga, Wema Sepetu na wasanii wengine ambao kila awapo na tatizo uwa mbele katika kumsaidia na kumfariji katika ugonjwa lakini si kundi ambalo yeye ni kiongozi pia kama katibu