Tuesday, August 2, 2011

DAR MODERN TAARAB NA MIPANGO YA MWEZI WA RAMADHANI

TWAHA -Muimbaji  Dar Modern Taarab

SIKUDHANI ALLY- Muimbaji

AMMAR - Muimbaji

SALHA - Muimbaji
Kundi la muziki wa Taarabu Bongo(Dar Modern Taarab) limeweka wazi mipango yake katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.


Akizungumza na Blog hii mmoja kati ya waimbaji wa Kikundi hicho anayefahamika kwa jina la Twaha, amesema kama inavyofahamika kuwa mwezi huu wa Ramadhani Mtukufu ambao unapaswa kuheshimiwa siyo tu kwa Waislam bali hata kwa wale wenye Imani tofauti, hivyo nao wanaungana na wale wote wanaoheshimu mwezi huu kwa kupumzika na kusitisha shughuli zao zote ikiwemo kutofanya maonyesho, isipokuwa katika kumi lamwisho wataanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya uzinduzi wa Album zao mbili ambazo watazitaja hapo baadae mambo yatakapokuwa tayari.

Aidha ameongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa mashabiki wao wa mikoani, wakati wa sikukuu ya IDD watakuwa na Show za mikoani wakianzia na Kahama mkoani Shinyanga.

No comments:

Post a Comment