Friday, August 12, 2011

JE UNAJIVUNIA CHA KWAKO WEWE KAMA MTANZANIA??????



Jamani tujifunze kujivunia, kuvithamini  na kuvijali vya kwetu hasa sisi Watanzania maana wengi wetu wana tabia ya kupenda vya nje tu na kuvidharau vya hapa kwetu.


Huwa napata simanzi sana mara kadhaa ninapotembelea kijiji cha Makumbusho pale vikundi vyetu vya ngoma za asili vinapotumbuiza unakuta wageni (watu weupe) kibaaaooooo lakini wabongo wenyewe wa kuhesabu, khaaa!!! hii inasikitisha kwa kweli na tunawakatisha tamaa ndugu zetu hawa waliojitolea kutupa burudani kwa style ya kwetu.


Mi nawaambia hamjui tu pale kuna burudani jamani hebu tujaribu hata mara moja au mbili kwa mwezi tujenge utamaduni wa kupita pale ili tuwape Support ndugu zetu hawa wanaoukuza na kuutangaza utamaduni wetu..


PICHA: Kwa Hisani ya Ankal Michuzi

No comments:

Post a Comment