Thursday, August 25, 2011

HII NDIYO LINDI YETU TWAJIDAIA WENYEWE

Hapa ndo City Center jengo linaloonekana ni CRDB Bank na kwa upande wa pili ni Soko kuu la Lindi wenyewe twaita Soko kubwa

Huu mtaa upo maeneo ya Posta ukiinyoosha huko mbele unakuta Stand kuu ya Mabasi

Hapa ni maeneo ya Police Linena hii inayoonekana kwa mbele ni karakana yao

Hapa ni Ofisi ya Posta sehemu ya kuingilia

Huu mtaa upo maeneo ya sokoni na hii ni barabara ya kuelekea Hospitali ya Mkoa yaitwa Sokoine na Kwa mbali namuona Rama Kindamba ni Mgonjwa wa akili maarufu kule Lindi (Huu mtaa ndio kwao swaiba wangu Sada Kadhi)

Hapa mitaa ya Uhindini yaani maeneo haya wanaishi wahindi sana waswahili ni wachache tu wa kuhesabu na ukinyoosha kule mbele unaelekea Stand kuu ya Mabasi pia

Jengo hili maarufu sana na hadi haya maeneo tulikuwa tunayaita kwa TAHFIF lakini pia ukivuka tu barabara upande wake wa pili ni Soko kuu(Nakumbuka hapa palikuwa maarufu sana kwa kinywaji Togwa maana wauzaji walikuwa wanajipanga hapo mida ya mchana hadi jioni, I mic Togwa jamaniiii)
Hapa wapi vileeeeeeee mbona sikumbukii
Hii ni ofisi ya TTCL na iko maeneo ya Posta
Ahsante kaka OTHMAN MICHUZI wa Blog ya mtaa kwa mtaa kwa kuikumbuka Lindi yetu, yaani nimefurahi sana kuona Mandhari ya Lindi yetu kwenye Blog yako ila mbona hujafika maeneo ya kwetu Wailes jamaniii?? Ila nimekumbuka mbali saaaanaaaa naamini wana Lindi wenzangu kama Sada Kadhi, Joseph Mahundu, Mwl Mussa Utaly, Shaibu Bao na wengineo mtakuwa mmefurahia pia.


                                              I LUV LINDIIIIIIIIIIII!!!!!



No comments:

Post a Comment