MENGINEYO

MENEJA WA BIA YA KILIMANJARO GEORGE  KAVISHE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI HAWAPO PICHANI.
                      
Dar es Salaam, Leo Jumatano 08 2012: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia
yake ya Kilimanjaro Premium Lager kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa Tanzania
(BASATA) leo wametangaza rasmi wateule wa vinyang’anyiro 22 vya Tuzo za Muziki

Tanzania (Kilimanjaro Tanzania Music Awards).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Meneja wa bia ya
Kilimanjaro Bwana George Kavishe alisema “Academy ilikaa mwisho wa wiki iliopita na
kufanya kazi ngumu na nzuri ya kuteua wasanii wa muziki waliofanya kazi nzuri na
zilizopendwa na kukubalika zaidi na wengi kwa mwaka 2011”.

Mchakato wa Academy ulisimamiwa na wasimamizi wa mahesabu na utawala INNOVEX
ili kuhakikisha zoezi linafanywa kwa uhuru na haki muda wote. George Kavishe aliongeza
“Kama tulivoahidi mwaka juzi na mwaka jana kwamba tuzo zitaendeshwa kisasa na
kitaalum ili kuzipatia haki na kutengeneza mazingira ya uwazi kwa wapenzi wa muziki
nchini. Tunaendeleza ahadi hii na ndio maana INNOVEX wameendelea kusimamia zoezi
hili la Academy pamoja na kura zote kwa mwaka huu tena.”

Kura za wana Academy ni siri na majibu ya wateule watano kwa kila kinyang’anyiro
hubaki siri ya INNOVEX hadi kutangazwa, halikadhalika na majibu ya kura za wananchi
za washindi.
Hatua zifwatazo:
1. Semina ya Wasanii:
Wasanii wateule wa tuzo mbalimbali watapata semina elekezi kuhusu tuzo hizi na
kupata nafasi kuuliza maswali juu ya mchakato mzima wa kupata wateule na
taratibu zitakazofwata.

2. Kura.
Kura zitapigwa kwa muda wa wiki 7 kuanzia tarehe 13/ Feb - 06/ Apr Maelekezo
ya upigaji kura yatapatikana katika tovuti ya Kilimanjaro www.kilitimetz.com na
mitandao mingine pamoja na kwenye matangazo ya magazeti na vipindi mbali
mbali ya redio na TV.

3. Usiku wa utoaji Tuzo.
Kilimanjaro Tanzania Music Awards zatarajia kufanyika tarehe 14. Aprili. 2012
katika ukumbi wa Mlimani City. Taarifa zaidi zitafuata kupitia mitandao, redio na
TV mbali mbali.

Walioteuliwa majina na kundi la Mtumbuizaji Bora wa Kike Khadija Kopa, Isha Mashauzi, Queen Darleen, Dayna na Shaa.Mtumbuizaji Bora wa Kiume, Diamond, Ally Kiba, Bob Junior, Dully Sykes na Mzee Yussuf.
Mwimbaji Bora wa Kiume Ally Kiba, Diamond ,Barnaba, Belle 9 na Mzee Yussuf. Mwimbaji Bora wa Kike Lady Jaydee, Khadija Kopa, Isha Mashauzi, Dayna na Linah.

Wimbo Bora wa Taarab Full Stop ulioimbwa na Khadija Kopa, Mamaa Mashauzi wa Isha Mashauzi,Hakuna Mkamilifu wa Jahazi, Nilijua Mtasema, Wimbo Bora wa Mwaka jina na aliyeucheza katika mabano ni Hakuna (Suma Lee), Dushelele (Ally Kiba), Moyo Wangu (Diamond), Mathematics (Roma), Nilipe Nisepe (Belle 9) na Riz One (Izzo B).

Katika kundi la kuwania tuzo ya Wimbo Bora ya Kiswahili uliopigwa na bendi waniwa na Dunia Daraja (The Africa Stars), Hukumu ya Mnafiki (Mashujaa Band), Falsafa ya Mapenzi na Mtenda zote (Extra Bongo) na Usia wa Babu (Mapacha Watatu).

Wimbo Bora wa R&B unawaniwa na nyimbo za My Number One Fan (Ben Pol), Maumivu (Ben Pol ft One), Nilipe Nisepe(Belle 9), Napta Raha (Jux) na Usiniache (Hemed). Wimbo Bora wa Hip Hop wanaowania ni Famous (Jay Mo ft P Funk), King Zila (Godzilla ft Marco Chali), Mathematics (Roma), Riz One (Izzo B), Kilimanjaro (Joh Makini ft Lady Jaydee, G Nako),Wimbo Bora wa Reggae Mazingira (Malfred ft Lutan Fyah),Arusha Gold (Worrior from the East), Give it Up to me(Delyla Princess), Nia Yao (20%), Ni Wewe (Nakaaya).

Wimbo Bora wa Ragga/Dancehall unawania wan a Goo Look (A.Y ft Miss Trinity), Maneno Maneno (Queen Darleen ft Dully Sykes), Ganja Man (Dabo), Kudadeki na Poyoyo (Malfred). Rapa Bora wa mwaka bendi wamo Kalidjo Kitokololo, Khalid Chokoraa, Msafiri Diouf na Totoo Ze Bingwa, Msanii Bora wa Hip Hop ni Godzilla, Roma, Izzo B, Joh Makini na Fid Q.

Kwa upande wa tuzo ya Wimbo Bora wa Afrika Mashariki inawaniwa na Kigeugeu (Jaguar)Chokoza (Avrill na Marya), Mulika Mwizi (Kidumu ft Sana), Coming Home (Nameless) , 4sho4shizzle (Prezzo) na Valuvalu (Jose Chameleon).

Tuzo ya Mtunzi Bora wa Mwaka inawaniwa na Diamond, Ali Kiba, Mzee Yussuf, Barnaba na Belle 9.Huku tuzo ya Mtayarishaji Bora (Producer) wa mwaka inawaniwa na Marco Chali,Pancho Latino, Bob Junior Maneck na Man Walter.

Video Bora ya Muziki ya Mwaka zinazochuana ni Moyo Wangu (Diamond), Hakunaga (Suma Lee), Wangu (Lady Jaydee ft Mr. Blue), Ndoa Ndoana (Kassim Mganga ft Mr. Blue) na Bongo Fleva (Dully Sykes).

Wimbo Bora wa Afro PopHakunaga (Suma Lee),Bongo Fleva (Dully Sykes), Moyo Wangu na Mawazo (Diamond) na Nai Nai (Ommy Dimples).Wimbo Bora wa Zouk/ Rhumba Daima Milele (Barbanaba), Dushelele (Ally Kiba), Nivute Kwako (Dyna ft Barbanaba),Wangu Lady Jaydee ft Mr. Blue) na Kizunguzungu (Recho).

Wimbo Bora wenye vionjo vya Kiasili unawaniwa na Bao la Kete (AT),Kidudu Mtu (Offside Trick ft Baby J), Vifuu Tundu (A.T ft Mwanne), Mwanadamu (Ashimba) na Tunapeta (Young Dee ft Kitokololo na Mataluma).Msanii Bora Anayechipukia Ommy Dimpoz, Darasa, Recho, Abdul Kiba na Beatrice a.k.a Nabisha. Wimbo Bora wa Kushirikiana ni Famous (Jay Moe ft P-Funk Majani), King Zilla (Godzilla ft Marco Chali), Wangu (Lady Jaydee ft Mr. Blue), Kama ni Ganster (Chegge, Tembaft Ferouz) na Nai Nai (Ommy Dimpoz ft Ally Kiba).