Tuesday, August 2, 2011

MARIAM AAHIDI MAKAMUZI KWA MASHABIKI WAKE

MARIAM MOHAMED akifanya mambo yake
Staa anayekuja kwa kasi ya ajabu kupitia Muziki wa Taarabu hapa Nchini MARIAM MOHAMED a.k.a MARIAM wa BSS kama wengi walivyozoea kumuita kutokana na kung'ara kupitia mashindano hayo na hatimaye kuibuka mshindi mwaka 2010, amewaahidi mashabiki wake na mashabiki kuwa amejipanga kufanya maajabu zaidi ya yale aliyoyafanya ndani ya BSS hivyo wasikose kuhudhuria Show zake.

Akizungumza na blog hii MARIAM ambae kwa sasa anafanya kazi na Kundi la Five Stars Modern Taarab la jijini DSM, amesema yale waliyoyaona mashabiki kwenye BSS ni madogo sana ila kwa sasa amejipanga zaidi na amekuja kuwashika Mashabiki hivyo wasikose kuhudhuria Show za kundi lake ili wajionee maajabu.

Kama utakumbuka kundi la Five Stars lilikuwa kimya kwa miezi takribani minne baada ya kuwapoteza wanamuziki wake 13 kutokana na ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Mikumi mkoani Morogoro, hivyo wamekuja upya baada ya kuajiri wanamuziki wapya akiwemo MARIAM, MUSSA KIJOTI mdogo wa Marehemu ISSA KIJOTI na wengineo.

No comments:

Post a Comment