Thursday, August 4, 2011

HII MAMBO HAILEWEKI KWELI KWELI!!!!????

TOTOO ZE BINGWA akizungumza na waandishi kabla ya uzinduzi


 Rapa wa Bendi ya Akudo Impact EMMANUEL KALONJI a.k.a TOTOO ZE BINGWA amelalamikia hali iliyotokea siku ya uzinduzi wa Album yake binafsi ya "hii mambo haieleweki" kwa kusema hakuamini na hakutarajia kitu kilichotokea cha watu kuwa wachache wakati wa uzinduzi wa Album yake hiyo July 23 mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Akiteta nami kupitia mtandao wa kijamii wa FACEBOOK, Totoo amesema tangu aanze muziki hajawahi kufanya Show na watu wasiitikie kama ilivyotokea siku hiyo, hivyo anaamini kulikuwa na hujuma imefanyika na hata hivyo ameahidi kutokata tamaa na amechukulia hizo ni kama Changamoto ambazo watu hupitia pale wanapoelekea mafanikio.

"Najua kuna watu wasiopenda maendeleo yangu wamenifanyia hujuma, lakini mimi nawaahidi kuwa hakuna kukata tamaa kwani hizi ni changamoto ndogo tu ambazo kila anaetafuta mafanikio lazima akutane nazo"

No comments:

Post a Comment