|
Mlezi wa Mashauzi Classic JUMA MBIZO akizungumza na wanahabari |
|
Mkurugenzi ISHA RAMADHANI akiitambulisha rasmi timu ya Mashauzi Classic |
|
Wanamuziki wanaounda Mashauzi Classic |
|
Wanahabari busy na kazi yao |
Bendi mpya ya Muziki wa Taarab nchini, "Mashauzi Classic" imetambulishwa rasmi kwa wanahabari na wadau wa muziki huo kwa ujumla jumamosi iliyopita.
Mkurugenzi mtendaji wa kundi hilo Bi ISHA RAMADHANI a.k.a ISHA MASHAUZI amesema wameamua kutambulisha kundi hilo kwa wadau baada ya kuhakikisha kuwa wamejipanga vema na wako tayari kutoa burudani ya uhakika kwa mashabiki wake.
"Kundi hili limeanza muda mrefu kidogo na tulikuwa tukitoa burudani kimya kimya kwa mashabiki wetu lakini sasa tumaamua kujitambulisha baada ya kuhakikisha kuwa tumejipanga vizuri na tuko tayari kutoa burudani ya uhakika kwa mashabiki wetu na tutazindua rasmi siku ya Eid mosi katika ukumbi wa "Travel Tine Hotel" alisema Isha.
Isha aliongeza kuwa baada ya kutoa burudani ya nguzu siku ya Eid Mosi, Eid pili watakuwa Kigamboni, Eid tatu Kibaha, Eid nne watakuwa Kawe na Eid tano wataporomosha burudani kwa mashabiki wa Ukonga.
Aidha kundi hilo tayari limekamilisha Album mbili, Album ya kwanza ikiwa na vibao vinne ambavyo ni" nani kama mama" ambacho kimebeba jina la Album, baraka za baba, Mamaa Mashauzi mtoto kutoka Musoma na Umdhaniaye ndiye kumbe siyo na katika Album ya Pili kuna nyimbo tano ambazo ni Hakuna kati yenu wa kunirusha roho, La mungu halina muamuzi, Niacheni nimpende, Sitosahau kwa yaliyonikuta na anayejishuku hajiamini.
Kundi hilo linaundwa na wanamuziki 22 akiwemo Isha mashauzi ambaye ni mkurugenzi, Bi Rukia Juma (Mama mzazi wa Isha) Kaimu Mkurugenzi, Thabit Abdul Mkurugenzi wa mipango Juma Mbizo Mshauri na Mlezi wa kundi na Wanamuziki wengine wakiwemo wapiga vyombo na waimbaji.