Thursday, July 28, 2011

CHIDY BENZ AIKACHA BANGI

CHIDY BENZ
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya CHIDY BENZ, ambae pia ni Star wa kipindi cha Chidy Show kinachorushwa na EATV ameweka wazi kuwa ameachana na uvutaji wa bangi a.k.a kijiti au majani.

Akiongea na Blog hii leo asubuhi Chidy Benz amefunguka kuwa ameamua kuachana na kilevi hicho kwa kuwa hakina faida yoyote kwake zaidi ya hasara inayotokana na ukorofi wake kila anapotumia kilevi hicho.

Chidy aliendelea kuweka wazi kuwa alianza kutumia bangi tangu akiwa mdogo wakati akiwa shuleni ambapo alikuwa akivuta kwa wingi na mpaka leo hajawahi kuona faida yake na akaongeza kuwa mara nyingi amekuwa akichelewa kwenye vikao na wasanii wenzake lakini chanzo kikuu ni utumiaji wa Bangi, hivyo amegundua kuwa kilevi hicho kinamuharibia mipango yake mingi ndipo akaona ni busara kuachana nacho.

Hata hivyo ameahidi kuwa hivi karibuni atatangaza kuachana na ulevi wa Pombe, ingawa ameweka wazi kuwa bado hajafanya maamuzi kwa kuwa uamuzi huo anahisi kuwa ni mgumu japokuwa anaendelea kuufanyia kazi taratibu.

No comments:

Post a Comment