Tuesday, July 19, 2011

MANYWELE KIMWANA WA TWANGAPEPETA 2011 "MARY KHAMIS" KUZIBA PENGO LA AISHA MADINDA

MARY KHAMIS (katikati) akiwa na mshindi wa pili wa shindano (kushoto) na pamoja na mshindi wa tatu



AISHA MADINDA akiwa na Mkurugenzi wa EXTRA BONGO, ALLY CHOKI

Muda mfupi baada ya Mnenguaji mahiri bongo AISHA MADINDA kuihama Bendi yake ya Twanga Pepeta na kutimkia Extra Bongo, Mkurugenzi wa Twanga pepeta ASHA BARAKA amemtangaza MARY KHAMIS mshindi wa Manywele kimwana wa Twanga Pepeta 2011 kuziba pengo hili lililoachwa na AISHA, ASHA BARAKA amesema uamuzi wa kumchukua MARY umekuja baada ya kuvutiwa na kuridhishwa na umahiri alioufanya Kimwana huo wakati wa shindano hilo na hatimaye kuibuka mshindi... Wakati huohuo Mkurugenzi wa Extra Bongo ALLY CHOKI jana amemtambulisha rasmi AISHA MADINDA kuwa ni mnenguaji mpya wa bendi yake hiyo


No comments:

Post a Comment