Wednesday, July 6, 2011

VUMILIA NA TSHALA MUANA KUWANIA TUZO ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

VUMILIA kutoka TZ



Mwana mama MBILI ABEL kutoka DRC

Mwanamuziki kutoka Tanzania VUMILIA MWAIPOPO(Queen of the Night) anatarajia kupambana na Gwiji wa Muziki barani Afrika  kutoka DRC,  TSHALA MUANA katika TUZO za AFRIKA MASHARIKI NA KATI zitakazofanyika AGOSTI 20 mwaka huu jijini NAIROBI, KENYA.

Waandaaji wa Tuzo hizo GOLDEN DREAMS wamesema VUMI atapambana na TSHALA MUANA pamoja na mwanamuziki kutoka kenya MASHA MAPENZI katika Tuzo ya mwanamuziki bora wa muziki wa RHUMBA. VUMI ameingia kwenye kinyang'anyiro hicho kupitia wimbo wake wa"Tatizo umaskini" wakati TSHALA MUANA ameingia kwa wimbo wake unaoitwa "Malozi" na MASHA ameingia kwa kibao chake "Kala ulele"

No comments:

Post a Comment