Monday, July 18, 2011

JENNIFER LOPEZ "J.LO" NA MARC ANTHONY WAVUNJA NDOA YAO

Baada ya ndoa yao kudumu kwa muda wa miaka saba, Mwanamuziki JENNIFER LOPEZ maarufu kama J.LO na mume wake ambae pia ni mwanamuziki na muigizaji MARC ANTHONY sasa ndoa hiyo imefikia tamati

J.LO na MARC ANTHON ambao walifunga ndoa June 2004 na kubahatika kupata watoto wawili mapacha MAX na EMME wenye umri wa miaka mitatu, kila mmoja kwa upande wake amekiri kuwa pamoja na kwamba uamuzi wa kutengana ni mgumu na unaoumiza sana lakini inapobidi kila mmoja anapaswa kuheshimu maamuzi ya mwingine kama walivyofanya wao.

No comments:

Post a Comment