Tuesday, July 5, 2011

MSAFIRI ZAWOSE ALIVYOITANGAZA TANZANIA BARANI ULAYA


MSAFIRI ZAWOSE akiwakilisha vizuri UTAMADUNI wetu


Hicho kifaa kinaitwa ILIMBA(moja ya vitendea kazi vyake)


Hapo akiwa kazini na kikundi chake kinaitwa CHIBITE

Mwanamuziki mahiri wa Muziki asilia mwenye soko barani ulaya, MSAFIRI ZAWOSE ambae alikuwa na ziara ndefu katika nchi mbalimbali huko ULAYA amerejea BONGO akiwa na mafanikio makubwa sana.

Akizungumza na AFROBEAT ya EATV mwishoni mwa wiki ZAWOSE amesema katika ziara yake hiyo amepata mafanikio makubwa sana ikiwa ni pamoja na kujitangaza yeye mwenyewe, MILA NA UTAMADUNI wa KIAFRIKAna pamoja na Taifa kwa ujumla.

Mbali na ziara yake hiyo iliyomchukua miezi kadhaa ameweza kutembelea katika nchi nyingi kama vile SWEDEN na DENMARK ambako ndiko amejizolea umaarufu mkubwa sana lakini pia ataendele na SHOW za kawaida hapa BONGO katika kumbi mbalimbali ambapo ijumaa iliyopita alikuwa SWEET EAZY ambapo alitoa burudani kwa kushirikiana na wanamuziki wengine akiwemo KAROLA KINASHA

No comments:

Post a Comment