Tuesday, July 5, 2011

MARIAM WA BSS KUIBUKIA 5 STARS MODERN TAARAB!!



Mshindi wa Kinyang'anyiro cha Bongo Star Search (BSS) 2010 MARIAM MOHAMED, ambae aling'ara kwa Umahiri wake katika uimbaji wa nyimbo za Muziki wa TAARAB hatimaye ameibukia katika kundi la FIVE STARS MODERN TAARAB "Watoto wa Pwani"

MARIAM ataungana na wasanii wenzake wapya ambao wataongeza nguvu katika kundi hilo ambalo lilipata pigo kwa kupoteza wanamuziki wake 13 katika ajali ya gari Mwezi Machi mwaka huu.

Kiongozi wa kundi hilo ALLY JAY amewataja wasanii wengine wapya kuwa ni Mwimbaji MUSSA ALLY KIJOTI (Mdogo wa marehemu ISSA KIJOTI), MFLOO MZUBYA Mpiga Gitaa la Solo na JUMA HAMIS Mpiga Gitaa la BASE.

No comments:

Post a Comment