Tuesday, July 12, 2011

MSECHU ATIKISA TUSKER PROJECT FAME "ALL STARS"

Mwakilishi kutoka TANZANIA katika shindano la Tusker Project Fame "All Stars" 2011, PETER MSECHU amewateka mashabiki wake kwa kuimba nyimbo za zamani kwa umahiri mkubwa na kuwaacha mashabiki wake wasiamini kilichotokea.
Msechu ambae ameingia kwenye mashindano hayo kwa mara nyingine baada ya kung'ara vilivyo katika mashindano ya TPF mwaka jana 2010, aliwaacha hoi mashabiki wake na wafuatiliaji wa Mashindano hayo kwa ujumla pale alipouimba kwa umakini mkubwa wimbo SHIDA wa MBARAKA MWINSHEHE katika usiku huo uliopewa jina la AFRICA REMIX THEME NIGHT.
Katika usiku huo washiriki walitakiwa kuimba nyimbo za wanamuziki wa zamani kama OLIVER MTUKUDZI, BRENDA FASSIE, MBARAKA MWINSHEHE na wengineo.... Hata hivyo PETER MSECHU yupo kikaangoni wiki hii ambapo anahitaji kura yako wewe Mtanzania ili aweze kubaki kwenye mashindano hayo... Mpigie KURA sasa kwa kuandika namba yake ya ushiriki mbayo ni TISA(9) halafu tuma kwenda namba 15522

No comments:

Post a Comment