Friday, July 15, 2011

NURU MBIONI KUTOA ALBUM YAKE

Baada ya kutoka na ngoma yake MUHOGO ANDAZI ambayo inakimbiza katika vituo mbalimbali vya Redio na Televisheni hapa Bongo akiwa amemshirikisha BOB JUNIOR,  Mwanamuziki wa Kizazi kipya NURU (Pichani) amesema kwa sasa anajipanga ili aweze kutoa Album yake mwishoni mwa mwaka huu.

Akizungumza na E-NEWS ya EATV, NURU amesema mpaka sasa tayari ngoma sita zimekwishakamilika anachosubiri kwa sasa ni kukamilisha ngoma zilizosalia ili kukamilisha Album hiyo ambayo itakuwa na nyimbo kumi katika Ladha tofauti tofauti, ambayo amepanga kuidondosha mwishoni mwa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment