Friday, July 22, 2011

MARY KHAMIS KUTIKISA KATIKA ONYESHO LA KUMCHANGIA GURUMO

Mshindi wa Shindano la manywele kimwana wa Twanga pepeta 2011 "MARY KHAMIS" kesho anatarajia kuungana na Bendi yake ya Twanga pepeta na Msondo Ngoma katika Onyesho la kumchangia Mwimbaji mkongwe MUHIDINI GURUMO ambae amekuwa akiugua kwa muda mrefu
Akizungumza na AFROBEAT ya EATV Mkurugenzi wa African Stars Entertainment(ASET) ASHA BARAKA, amesema lengo la onyesho hilo ambalo limeandaliwa na ASET kupitia Bendi yake ya Twanga pepeta ni kuchangisha pesa za kumsaidia Muimbaji huyo mwenye heshima kubwa hapa Nchini, kwa ajili ya Matibabu na Kujikimu katika matumizi yake ya kawaida.

No comments:

Post a Comment