Wednesday, July 20, 2011

HAPPY BIRTDAY 2ME

Jamani leo ni Siku yangu muhimu na ya historia kwa Familia ya bwana na marehemu bibi YUNUS MOHAMED kwa kuwa siku kama ya leo miaka kadhaa iliyopita ndipo nilizaliwa mimi.. Naomba kuchukua nafasi hii kuwashukuru wazazi wangu kwa kunileta hapa duniani na kunilea katika maadili mema ambayo yamenijenga na kunifikisha hapa nilipo.. Sina cha kuwalipa zaidi ya kusema ahsante sana wazazi wangu na ninawapenda sana, lakini nasikitika pia kuifurahia siku hii bila ya mama yangu ambae ndiye alikuwa msingi mkuu wa maisha yangu katika kila hatua niliyoipitia kwa kuwa sasa hatuko naye tena duniani ametangulia mbele za haki... MAMA nakuombea kila kukicha MWENYEZIMUNGU AIWEKE ROHO YAKO MAHALI PEMA PEPONI, AMINA
Nilipofika ofisini watu wengi walinipongeza na tukapiga picha za ukumbusho kama unavyoona(hapo juu nikiwa nimepozi na HALIMA FRED Producer wa SKOOOOOONGAAAAAA)

Mutoto muzuri na BASILISA JOHN Presenter wa ujenzi 


             Jamani sitokuwa na fadhila nisipomshukuru MUPENZI sababu yeye ndo alinikumbusha kuwa leo ni siku yangu ya kuzaliwa maana mwenyewe mambo mengi na nilishasahau kabisaaaa, nikashangaa naambiwa ukifika Posta nisubiri baada ya kukutana naambiwa Hapi b'day bby nikasenma loh kumbe ndo tarehe 20 imeshafika hivyooo... lol!!! Thanx much baby.... LUV UUUUUUUUUU.

No comments:

Post a Comment