Thursday, July 14, 2011

BOB JUNIOR KUJIKITA KWENYE FILAMU

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya nchini BOB JUNIOR a.k.a Rais wa Masharobaro (Pichani) amesema ameamua kujichanganya na kufanya vitu vingine tofauti tofauti kama vile kucheza Filamu.

Bob Junior amesema katika kudhihirisha hilo ameanza na Filamu inayoitwa CANDY mali ya JACQUELINE WOLPER (Pichani) ambayo amekamua vilivyo katika kuwaonyesha mashabiki wake kuwa habahatishi ila amejaaliwa vipaji vingi ukiachilia mbali kuimba na kutengeneza ngoma mbalimbali ikiwamo ya mwanamuziki mwenye jina kubwa  ndani na nje ya Nchi  LADY JAYDEE (WANGU) ambayo amemshirikisha Mr BLUE


Akizungumzia Sakata lake la kumfikisha Mahakamani kwa kosa la kumshambulia kwa Matusi Mrembo WEMA SEPETU (Pichani), amesema Pamoja na yote ambayo yametokea lakini kwa sasa anamshukuru mungu kwa kuwa mambo hayo yamemalizika salama kutokana na yeye kuamua kumsamehe Mrembo huyo baada ya kukiri Kosa na kuomba Msamaha mara kadhaa na kuahidi kuwa yuko tayari kufanya nae kazi kama itatokea.

No comments:

Post a Comment